2025.09.07 Kutangazwa Watakatifu wenyeheri Beati Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis kuwa watakatifu. 2025.09.07 Kutangazwa Watakatifu wenyeheri Beati Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis kuwa watakatifu.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Mungu anataka amani.Ushindi wa silaha ni kushindwa

Katika salamu zake mara baada ya Misa Takatifu ya kuwatangaza Frassati na Acutis kuwa Watakatifu,Papa alizikumbuka nchi zilizokumbwa na vita na kuziomba serikali kusikiliza sauti ya dhamiri,kwa sababu Mungu huwaunga mkono wale wanaojitolea kujinasua kutoka katika chuki na kufuata njia ya mazungumzo.Mawazo yake kwa waliotangazwa wenyeheri huko Estonia na Hungaria,Septemba 6:Mjesuit Profittlich na Maria Maddalena Bódi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Misa takatifu na kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, katika fursa ya Kuwatangaza kuwa Watakatifu Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis, Dominika tarehe 7 Septemba 2025, kwa waamni waliounganisha katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,  Baba Mtakatifu alikuwa na ya kusema: “Ndugu wapendwa, kabla ya kuhitimisha sherehe hii iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, napenda kuwasalimu na kuwashukuru wote mliojitokeza kwa wingi kusherehekea watakatifu wawili wapya. Ninawasalimu kwa upendo maaskofu na mapadre, na ninawakaribisha kwa heshima wajumbe rasmi na mamlaka mashuhuri.

Misa ya kutangazwa mwenyeheri  Profittlich Tallin -Estonia
Misa ya kutangazwa mwenyeheri Profittlich Tallin -Estonia

Katika hali hii hii, Papa aliongeza kusema, “inapendeza kukumbuka kwamba jana(Septemba 6, 2025)  Kanisa pia lilitajirishwa na baraka mbili mpya. Huko Tallinn, mji mkuu wa Estonia, Askofu Mkuu Mjesuit Eduard Profittlich, aliyeuawa mwaka 1942 wakati wa mnyanyaso ya serikali ya Kisovieti dhidi ya Kanisa, alitangazwa mwenyeheri. Na huko Veszprém, Hungaria, Mária Magdolna Bódi, mwanamke kijana aliyeuawa mwaka 1945 kwa kuwapinga wanajeshi waliotaka kumbaka, alitangazwa kuwa mwenyeheri. Kwa njia hiyo tumsifu Bwana kwa ajili ya mashahidi hawa wawili, mashahidi jasiri wa uzuri wa Injili.”

Kutangazwa Mwenyeheri Magdalena Bod huko Hungaria
Kutangazwa Mwenyeheri Magdalena Bod huko Hungaria

Maombi ya Papa Leo XIV kwa ajili ya Ukraine,Nchi Takatifu na duniani kwa ujumla

Papa Leo kadhalika alisema “Kwa maombezi ya Watakatifu na Bikira Maria, tunakabidhi sala yetu isiyo na kikomo ya amani, hasa katika Nchi Takatifu na Ukraine, na katika kila nchi nyingine iliyomwagika damu na vita. Kwa wale walio na mamlaka, ninarudia: sikilizeni sauti ya dhamiri!”

Watu hawana mahali pa kuishi Gaza
Watu hawana mahali pa kuishi Gaza

“Ushindi unaoonekana kupatikana kwa nguvu ya silaha,” kupanda kifo na uharibifu, Papa alikazia kiukweli ni kushindwa na kamwe hauleti amani na usalama. Mungu hataki vita. Mungu anataka amani! Na Mungu anawaunga mkono wale waliojitolea kujinasua kutoka katika mduara wa chuki na kutembea njia ya mazungumzo.

Yafuatayo ni mahojiano na walioshiriki Misa Takatifu ya Kutangazwa kuwa Watakatifu Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis:

Ndugu msikilizaji, tukiwa katika furaha hii ya kuwa na vijana watakatifu wa kizazi chetu,  ndani ya studio hizi, tunaye mgeni ambaye, mara baada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Leo XIV, na ameudhuria Misa Takatifu, basi tumsikilize ushuhuda wake kuhusiana na si kukuu ya leo.  Tunakukaribisha na karibu sana katika vyombo hivi vya Radio Vatican kwa mara nyingine tena, kama mtangazaji mwenzetu na mwandishi mwenzetu.

“Mimi naitwa Grace Kabogo, nimekuwa mara kadhaa nikichangia hapa Radio Vatican. Nashukuru tena kwa kunialika Sista, nifuraha sana kuwa hapa. Kwa ufupi tu kiukweli Misa ya leo, imekuwa ya baraka sana kwangu, kwa sababu ninaweza nikasema ni mara ya kwanza kuhudhuria ibada ya Misa ya kutangazwa watakatifu. Sijawahi kuhudhuria Misa yoyote ile ya Papa akimtangaza Mwenyeheri wala kumtangaza Mtakatifu yeyote. Kwa hiyo, hii ni mara yangu ya kwanza. Papa, ametoa mahubiri ambayo ya metuonesha tafakari ya maisha ya hawa Watakatifu wapya Carlo Acutis na Pier Giorgio Frassati. Amezungumzia maisha yao na ilikuwa ni Misa ya furaha sana kwa sababu nilikuwa naomba sana mwenyezi Mungu anijaliye afya njema,  niweze kushuhudia, kwahiyo kulikuwa na ile hali ya kuwa na furaha, hali ya kuwa na machozi ya furaha. Kwa sababu mimi Carlo Acutis katika hawa Watakatifu wawili ni Mtakatifu ambaye nilikuwa ni kimuomba sana. Amekuwa Mtakatifu ambaye ni miongoni mwa Watakatifu na wenyeheri wa familia yangu, amekuwa Mtakatifu ambaye nimemchukua kama mwanangu. Kwa hiyo, ni uelewa pia kuandaa makala kwa ajili yake, kwa hiyo nimefurahi sana, kuudhuria  Misa hii ya kutangazwa hawa Watakatifu wawili wapya.”

Hawa ni Watakatifu wa siku zetu na zaidi,  Carlo Acutis anajulikana sana, lakini tusema hivi, sura nyingine ya  Mtakatifu mpya ni kijana ambaye kama ingekuwa ni vizuri zaidi wanachuo wa vyuo vikuu, wakajifunza kutokana na yeye, kiasi kwamba hata Baba Mtakatifu Leo, amesisitiza, na ametoa ushuhuda wake kwamba wakati anakwenda kuwasaidia maskini, alikuwa anachukua mkokoteni, mpaka ukaitwa kwamba ni usafiri wa Frassati kwa ajili ya kwenda kuwapelekea mizigo maskini. Je, kama wanafunzi wa Vyuo Vikuu,  unawashauri kitu gani?

Kwa sababu Frassati, kwanza kabisa alipenda sana masomo, kwa hiyo, ningewashauri wanafunzi wa Vyuo Vikuu wafuate nyayo zake kwa kupenda sana masomo, wazingatie masomo. Lakini vile vile, mbali tu nakuzingatia masomo, wakumbuke pia kuwajali na kuwasaidia maskini kama alivyofanya Frassati, maana yake kumbuka pia alikuwa anachukua nauli anayopewa badala kutumia kusafiri, kurudi nyumbani ama kwenda chuo, yeye alikuwa anagawa kwa maskini.  Kipindi cha baridi kali, majaketi yale, yale makoti alikuwa pia na masweta mazito kwa ajili ya kuvaa kujizuia baridi,  lakini alikuwa anayatoa kwa watu maskini, wasio na uwezo, ambao walikuwa hawana uwezo wa kunua makoti wala kununua masweta yale mazito kujifunika kujizuia baridi. Kwayo ningewaasa tu wajaribu kufata nyayo zake Mtakatifu Frassati.

Kwa hayo machache, unayo mengine zaidi ambayo ungeza kuwaelezea mbali na haya ambayo tumezungunza pamoja?

“Naweza nikasema hawa ni watakatifu wa kizazi cha sasa, japokuwa Carlo Acutis, ndiye Mtakatifu wa milenia kama tunavyo fahamu na ndiye Mtakatifu wa kwanza wa milennia, ameishi katika maishi ambayo tunaishi sisi halisia, amaisha ya Mitandao. Yeye alikuwa ni mtu wa mitandao, kwamba alitumia mitandao ya internet, mtu ambaye alitumia simu ya mkononi na ndiye anakuwa Mtakatifu wa kwanza kwa hayo mambo. Kwa hiyo ningewaasa, vijana,  hata sisi watu wazima ambao hivi sasa tunatumia sana Mitandao, japokua tumengia zaidi kwa Mitandao ya Kijami, tunatumia simu za mkononi na hasa hizi za kisasa, tuzitumie vizuri katika kueneza Injili na kumtangaza Yesu Kristu na hasa Ekaristi Takatifu kama alivyofanya Mtakatifu Carlo Acutis, ninakushukuru sana.

Basi, ndugu msikilizaji, ndani ya studio hizi tunaye mwingine ambaye naye ajitambulishe na atueleze yale ambayo yamemgusa kwa siku ya leo katika sikukuu hii ya kuwatangaza Watakatifu wapya Pier Giorgio Frassati pamoja na Carlo Acutis.

Mimi naitwa Florian Anthony Lengama, niko hapa Roma kwa ajili ya sherehe hii ya kuwatangaza watakatifu. Nimemshukuru Mungu kwa fursa hii tuliyoipata na nimejifunza mengi na siku zote tukumbuke kusali. Kusali ni muhimu ili baadaye tuweze kuwa watakatifu…..

Na zaidi hasa kwa vijana, kuwa watakatifu wa leo vijana, huyu wa miaka 15 na mwingine miaka 24 unawashauri kitu gani hasa vijana wetu wa kizazi hiki kipya

 Kwa vijana wa kizazi kipya muhimu ni kusali na kumuomba Mungu awaongoze katika kila jambo wanalofanya na kumtegemea Mungu kwa mambo yote, ili hapo badae waweze kuwa na maisha mema na mwisho wa siku warudi kwa Mungu Baba.

Nawashukuru sana na Mungu awabariki katika safari yenu na katika shughuli zenu za kila siku.

Nashukuru sana asante kwa fursa Mungu akubariki sana.

Ninashukuru ninyi nyote kwa ushuhuda mliy tutolea,na Mungu awabariki sana.         

Mara baada ya Misa Papa ametoa wito

 

07 Septemba 2025, 16:06