Papa Leo XIV:Oktoba 11,kusali Rozari kwa ajili ya Amani katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Rozari ya Amani katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Jumamosi, tarehe 11 Oktoba 2025 siku ambayo Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Yohane XXIII, Papa wa Waraka wa Pacem huko Terris na ujumbe wa radio unaowasihi viongozi wa Marekani na USSR "kuleta amani" katika kilele cha Mgogoro wa Kombora la Cuba. Na siku ile ile ya ilikuwa ya ufunguzi wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican tarehe 11 Oktoba 1962, na siku maarufu ya "hotuba kwa mwezi," inayojulikana ya Papa Roncalli, mwishoni mwa siku kuu ya amani.
Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 24 Septemba akiwageukia waamni na mahujai waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro alitangaza mpango wa maombi, uliopangwa kufanyika saa 12 kamili, masaa ya Ulaya na saa 1.00 kamili masa ya Afrika Mashariki, jioni, katika muktadha wa Jubilei ya Tasaufi ya Maria Papa alisema: “Wapendwa kaka na dada, mwezi wa Oktoba, unaokaribia sasa, umejitolea hasa kwa Rozari Takatifu katika Kanisa. Kwa hiyo, ninamwalika kila mtu, kila siku ya mwezi ujao, kusali Rozari kwa ajili ya amani, kibinafsi, katika familia zao, na katika jumuiya zao.” Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa “pia ninawaalika wale wanaohudumu mjini Vatican kusali sala hii katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kila siku saa 1:00 jioni.”
Kwa namna ya pekee, jioni ya Jumamosi, tarehe 11 Oktoba, saa 12:00 jioni, tutafanya hivyo kwa pamoja katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, wakati wa Mkesha wa Jubilei ya Tasaufi ya Maria, pia kukumbuka kumbukumbu ya kufunguliwa kwa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican.
Katika salamu zake kwa Lugha ya Kiingereza
“Nina furaha kuwakaribisha asubuhi ya leo mahujaji na wageni wanaozungumza Kiingereza, hasa wale kutoka Uingereza, Scotland, Ireland, Kaskazini, Denmark, Afrika Kusini, Uganda, Australia, New Zealand, Bangladesh, India, Indonesia, Malaysia, Qatar, Ufilipino, Vietnam, Canada, na Marekani. Kwa maombi na kuwatakia mema Jubilei hii ya Matumaini iwe kwenu na familia zenu wakati wa neema na kufanywa upya kiroho, ninawaombea furaha na amani ya Bwana wetu Yesu Kristo.”
