Vita nchini Ukraine vinaendelea kuwacha magofu na uharibifu wa miundo mbinu Vita nchini Ukraine vinaendelea kuwacha magofu na uharibifu wa miundo mbinu  (ANSA)

Papa Leo XIV:Ukraine idumu katika imani licha ya janga la vita

Kabla ya salamu kwa lugha ya Kiitaliano,Papa Leo XIV alitoa wazo kwa nchi ya Ulaya Mashariki,akiomba maombezi ya Padre Petro Paolo Oros,aliyeuawa kwa chuki kwa imani,ambaye alitangazwa kuwa mwenyeheri Jumamosi Septemba 27.

Vatican news

Tuombe kwa maombezi ya Mwenyeheri mpya ili watu wapendwa wa Ukraine waweze kudumu kwa ujasiri katika imani na matumaini licha ya janga la vita. Ni maombi ya Baba Mtakatifu Leo XIV akirejea nchi ya Ukraine, ambayo sasa imeharibiwa na vita kwa miaka mitatu. “Kwa masikitiko ya kupoteza maisha ya binadamu, wapendwa wetu, na maeneo ya wapendwa, Baba Mtakatifu aliwataka watazame mfano wa Padre Petro Paulo Oros wa Upatriaki wa Mukachevo, aliyeuawa mnamo mwaka 1953 kwa chuki ya imani yake ambaye Jumamosi tarehe 27 Septemba, Mama Kanisa amemtangaza kuwa mwenyeheri huko Bilky.

Petro Paulo Oros
Petro Paulo Oros

Mwaminifu kwa Mungu

Kabla ya salamu za Kiitaliano, Papa Leo XIV alikumbuka muktadha ambamo Padre huyo alifanya kazi kwa ajili ya upendo wa Mungu. Kanisa Katoliki la Ugiriki lilipopigwa marufuku, alibaki mwaminifu kwa Mrithi wa Petro na kwa ujasiri aliendelea kufanya huduma yake kisirisiri, akijua hatari zake. Ibada ya kumtangaza mwenyeheri inaongozwa na Kardinali Grzegorz Ryś, Askofu Mkuu wa Łódź, nchini Poland, na mwakilishi wa Papa. Peter Oros alizaliwa tarehe 14 Julai 1917, katika kijiji cha Bir, nchini Hungaria, (Ukraine), eneo ambalo Padre, Ivan, Padre wa Kikatoliki wa Ugiriki, alikuwa ametumwa kutekeleza huduma yake.

Misa ya kutangwaza mwenyeheri mpya huko Bilky
Misa ya kutangwaza mwenyeheri mpya huko Bilky

Akiwa na umri wa miaka tisa, mama yake alikufa na akachukuliwa na familia ya Padre mwingine wa Kikatoliki wa Ugiriki huko Ukraine. Mnamo 1942, alipewa upadre wa Jimbo la Mukachevo. Alitekeleza huduma yake katika kipindi ambacho serikali ya Kisovieti ilikuwa ikijaribu kukandamiza Kanisa Katoliki la Ugiriki. Baada ya 1949, shughuli za uchungaji zilipopigwa marufuku na maeneo yote ya ibada ya Wakatoliki wa Ugiriki kufungwa, alifanya kazi mafichoni. Mnamo tarehe 27 Agosti 1953, aliuawa na wakala wa huduma ya siri katika kijiji cha Zarichchia, mbele ya waamini wake. Tarehe 5 Agosti 2022, Papa Francisko alitia saini amri ya kutambua mauaji ya Padre huyo.

Wito wa Papa kwa Ukraine
27 Septemba 2025, 13:48