Papa Montini. Papa Montini.  Tahariri

"Kamwe kusiwe na vita tena!"kilio kisichosikika na cha wakati mwafaka cha Paulo VI

Miaka 60 iliyopita,Papa Montini alihutubia Umoja wa Mataifa,miaka ishirini baada ya kumalizika kwa maafa makubwa ya Vita vya Pili vya Dunia.Ulimwengu uligawanywa katika kambi mbili na wakati wa mazungumzo yalikuwa yameanza na kutoa ubridi.

Andrea Tornielli

“Jamais plus la guerre, jamais plus la guerre!”- yaani “kamwe vita visiwepo, kamwe pasiwepo na vita.” Miaka 60 imepita tangu Papa Paulo VI, Askofu wa Roma, alipohutubia kilio chake cha amani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ilikuwa Jumatatu,tarehe 4  Oktoba 1965. Ulimwengu, ulioibuka miaka ishirini mapema kutoka katika janga kubwa la Vita vya Pili vya Dunia uligawanywa katika kambi mbili na na mapwma  ulikuwa umeanza kipindi cha mazungumzo na na kuondoa ubaridi,  majaribio ya kwanza ya kufikia makubaliano juu ya udhibiti wa silaha za nyuklia.

(LEGGI QUI IL TESTO COMPLETO DEL DISCORSO DI SAN PAOLO VI)-yaani somoa Hotuba mzima ya Papa Paulo VI.

"Mnatarajia kutoka Kwetu neno hili," Papa Montini alisema, "ambalo haliwezi kuondolewa mvuto na heshima: si dhidi ya kila mmoja, siyo tena, siyo milele! Kwa kusudi hili kuu Shirika la Umoja wa Mataifa lilianzishwa: dhidi ya vita na kwa ajili ya amani!” Naye akaongeza hivi: “Sikiliza maneno yaliyo wazi ya mtu mashuhuri ambaye sasa amefariki, John Kennedy,” aliyetangaza hivi: “Ubinadamu lazima ukomeshe vita, au vita vitakomesha ubinadamu.” Uamuzi wa Kennedy unaonesha uhalisia wake wote wa kutisha kwa usahihi katika saa ya giza ambayo ulimwengu unapitia kwa sasa. Mgogoro wa vyama vingi na taasisi kama UN upo kwa wote kutazama.

Vita hivyo vya Tatu vya Ulimwengu, vilivyoanza kwa sehemu ndogo, ambavyo Papa Francisko alianza kushutumu zaidi ya miaka kumi iliyopita, inaonekana kukaribia kwa kutisha. Ubinadamu unaonekana kupoteza kumbukumbu yake ya siku za nyuma. Tumejawa na mamilioni ya kile kinachoitwa maelezo ya enzi ya kidijitali ambayo hutufanya tujisikie kama kizazi chenye maarifa zaidi, ilhali tumezingirwa na habari za uwongo, propaganda za vita, na masilahi yasiyoelezeka ya watengenezaji silaha na wafanyabiashara wa kifo.

Sauti za Mapapa katika Umoja wa Mataifa(UN)

Vita vya kidugu ndani ya moyo wa Wakristo wa Ulaya, vilivyochochewa na uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na vita vya kidugu katika moyo wa Nchi Takatifu, vilivyochochewa na shambulio la kigaidi lisilo la kibinadamu la Hamas na ambalo sasa linafanywa kwa ghasia zisizo na msingi na jeshi la Israeli: hii ni mizozo miwili tu kati ya mingi inayopambana  ulimwenguni kote ambayo imesahaulika, chini ya rada. Mkasa wa Gaza, kuwekwa kizuizini na kuuawa kwa mateka, mauaji ya raia—makumi ya maelfu ya watoto, wanawake, na wazee—pamoja na waathirika wengi wa raia wa vita katika Ukraine yawakilisha fedheha, shimo jeusi kwa dhamiri ya maadili ya ulimwengu.

Sheria za kimataifa na sheria za kibinadamu zinavutwa kwenye mzozo huo na kupingwa ili kukidhi maslahi ya wenye nguvu zaidi. Wakikabiliwa na serikali zinazozungumza kuhusu vita, kujiandaa kwa ajili yake, na kuwekeza kiasi kikubwa sana katika silaha, kilio cha Papa asiye na ulinzi kutoka Brescia bado kinasikika leo hii, ambacho ni muhimu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka sitini iliyopita. Maneno haya yanahusiana sana na hisia za watu, ambao bado wanahisi kukerwa na mauaji ya kila siku tunayoshuhudia na kutumaini kwamba diplomasia, mazungumzo, ubunifu katika mazungumzo, uwezo wa kushiriki katika mazungumzo na kuchunguza njia mpya za amani hatimaye utapata wale ambao watafuatilia, badala ya kujisalimisha kwa propaganda za vita chafu zaidi.

Ili kutangaza kusudi la Umoja wa Mataifa, Papa Paulo VI alitamani “kukumbuka kwamba damu ya mamilioni ya watu na mateso yasiyohesabika na yasiyosikika, mauaji yasiyo ya lazima, na uharibifu wa kutisha yatia muhuri mapatano ambayo yanakuunganisha, kwa kiapo ambacho lazima kibadilishe historia ya siku zijazo ya ulimwengu. Vita visiwepo kamwe  tena, vita tena visiwepo Amani, amani lazima iongoze hatima ya watu na wanadamu wote!” Tusisahau hili, hasa leo hii.

Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here

05 Oktoba 2025, 10:49