Leo XIV kwa Wajesuit:Jumuiya isoma ishara za nyakati&utambuzi katika utume
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa Hotuba yake alasiri, tarehe 24 Oktoba 2025 kwa wakuu wa Shirika la Kijesuit, zaidi ya mia moja aliokutana nao katika Ukumbi wa Sinodi, wakiongozwa na Mkuu wa Shirika hilo, Padre Arturo Sosa. Hotuba hiyo ndefu ilikuwa mada mbali mbali ambapo Papa alianza kumshukuru Mkuu wa Shirika hilo na kuhimiza Jumuiya kutambua njia mpya za kuishi kulingana na utume wako katika ulimwengu wa leo. Mkutano wa Wakuu wa Shirika hilo ulianza tangu 2005 ambao unawaleta pamoja takriban Wajesuiti 100 kutoka ulimwenguni, wakiwemo Wakuu kanda , na marais wa Baraza . Mkutano huo wa siku kumi, ulioanza tarehe 17 Oktoba 2025, unajumuisha nyakati za kutafakari, utambuzi wa pamoja, na hija ya Jubilei kupitia Mlango Mtakatifu.
Katika hotuba yake pana, Papa Leo XIV alielezea wakati uliopo kama mabadiliko ya enzi yaliyooneshwa na mabadiliko ya haraka katika utamaduni, teknolojia, na siasa. “Akili Unde(AI) na uvumbuzi mwingine unabadilisha uelewa wetu wa kazi na mahusiano, na hata kuibua maswali kuhusu utambulisho wa binadamu," alisema, akibainisha pia vitisho vya uharibifu wa ikolojia, ukosefu wa usawa, na mgawanyiko. “Lakini katika ulimwengu huu, Kristo bado anawatuma wanafunzi wake," alifafanua huku, akikumbuka jinsi Mtakatifu Ignatius wa Loyola na wenzake ambao hawakuogopa kutokuwa na uhakika au ugumu; walikwenda pembezoni, ambapo imani na sababu ziliingiliana na tamaduni mpya na changamoto kubwa.
Akinukuu hotuba ya Mtakatifu Paulo VI ya mnamo 1974 kwa Wajesuit, Papa alirudia: kusema kuwa "Popote Kanisani, hata katika nyanja ngumu na kali zaidi ... Kumekuwa na... na kuna, Wajesuiti." Na kwa hiyo Papa aliendelea kusema kuwa “Narudia: Kanisa linawahitaji kwenye mipaka, iwe ni ya kijiografia, kiutamaduni, kiakili au kiroho. Hizi ni sehemu za hatari, ambapo ramani zinazojulikana na hazitoshi tena." Papa aliwaalika Wajesuit kutambua kwa ujasiri na kutekeleza kanuni ya Mtakatifu Ignatius ya kujali utakatifu kama utayari wa kuachana na miundo au majukumu yanayothaminiwa nje, wakati Roho inapoongoza mwili wa kitume mahali pengine kwa manufaa zaidi."
Miongoni mwa mipaka mikubwa inayolikabili Kanisa leo hii, Papa Leo XIV aliakisi njia ya sinodi, akiiita safari inayohitaji kumsikiliza Roho Mtakatifu kwa undani zaidi na kwa kila mmoja. Aliishukuru Jumuiya kwa michango yake katika mchakato wa sinodi na kwa kusaidia jumuiya za Kanisa kutembea pamoja kwa matumaini. Akigeukia mada ya upatanisho, alisema dunia inaendelea kuteseka kutokana na migogoro, ukosefu wa usawa na unyanyasaji, na kwamba majeraha mengi yanaendelea kutopona katika vizazi na watu. Lazima tupinge utandawazi wa ukosefu wa nguvu kwa utamaduni wa upatanisho, na kukutana katika ukweli, msamaha na uponyaji Papa alisisitiza akiwahimiza Wajesuit kuwa wataalamu wa upatanisho, wakiwa na uhakika kwamba mema yana nguvu kuliko uovu.
Papa Leo XIV alijikita na sehemu ya hotuba yake katika changamoto za kimaadili zinazotokana na teknolojia mpya, hasa akili Unde (AI). Aliita hii ni vizingiti muhimu, akibainisha kwamba kuwa ingawa ina uwezo mkubwa, pia ina hatari za kutengwa, kupoteza kazi na aina mpya za udanganyifu. Kwa hiyo "Kanisa lazima lisaidie kuongoza maendeleo haya kimaadili, kutetea hadhi ya binadamu na kukuza manufaa ya wote. Tunahitaji kutambua jinsi ya kutumia majukwaa ya kidijitali kuinjilisha, kuunda jumuiya na kutoa changamoto kwa miungu ya uongo, nguvu na kujitosheleza."
Ukitaka kusoma hotuba nzima ya Papa bonyeza hapa:READ POPE LEO'S FULL DISCOURSE HERE
Mapandeleo 4 ya Utume wa Kijesuit Ulimwenguni
Baba Mtakatfu Leo XIV akijikita kuzungumzia Mapendeleo manne ya Kitume Ulimwenguni ya Shirika la Yesu(Jesuit), yaliyothibitishwa mnamo mwaka 2019 na Mtangulizi wake, Papa Francisko, aliyaelezea kama “mipaka inayohitaji utambuzi na ujasiri." Akikumbuka Upendeleo wa kwanza, aliwahimiza Wajesuit kuwaongoza watu kwa Mungu kupitia Mafungo ya Kiroho na utambuzi, huku akibainisha kwamba wengi leo hii wanatafuta maana, mara nyingi bila kutambua. Akimtaja Mtakatifu Agostino, asemaye: "Umetuumba kwa ajili yako mwenyewe, Ee Bwana, na mioyo yetu haina utulivu hadi itulie ndani yako”, aliwataka Wajesuiti wakutane na watu katika hali hiyo ya kutotulia ... katika nyumba za mapumziko, vyuo vikuu, mitandao ya kijamii, parokia na maeneo yasiyo rasmi ambapo watafutaji hukusanyika, na kubaki"watafakari katika vitendo, wenye mizizi katika urafiki wa kila siku na Kristo."
Pendekezo la Pili kutembea na maskini na waliotengwa
Papa Leo XIV akizungumzia Upendeleo wa pili wa kutembea na maskini na waliotengwa - alilaani "mfumo wa kiuchumi unaoendeshwa na faida zaidi ya hadhi ya mtu," akinukuu Wosia wake wa hivi Karibuni wa Dilexi Te, ambapo alionya dhidi ya udikteta wa uchumi unaoua. “Ukosefu huu wa usawa wa kimataifa unawasukuma watu wengi kuhama wakitafuta kuishi. Ufuasi wa kweli unahitaji kukemea dhuluma na pendekezo la mifumo mipya inayotokana na mshikamano na manufaa ya wote,” alisema. Kwa njia hiyo Papa Leo XIV alihimiza “taasisi za ya KiJesuit, ikiwa ni pamoja na Vyuo vikuu, vituo vya kijamii, machapisho, na Huduma ya Wakimbizi ya Kijesuit, kuhamasisha na kukuza mabadiliko ya kimfumo na kupinga uchovu wa huruma au imani ya hatima, badala yake wakiamini nguvu ya mabadiliko ya upendo wa Mungu.”
Pendeleo la 3 la kusinidikiza vijana
Akigeukia Upendeleo wa tatu, kuhusu kusindikiza vijana, Papa Leo XIV alisema kwamba “vijana wanashiriki kiu ya uhalisi na mabadiliko na kwamba Kanisa lazima lipate na kuzungumza lugha yao. Ni muhimu kuunda nafasi ambapo wanaweza kukutana na Kristo, kugundua wito wao, na kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme, alisema, akibainisha kuwa Siku ya Vijana Duniani ijayo nchini Korea(WYD2027) itakuwa wakati muhimu kwa utume huo.”
Upendeleo wa 4: Utunzaji wa Nyumba yetu ya pamoja
Kuhusu Upendeleo wa nne wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, Papa Leo XIV alielezea ubadilishaji wa ikolojia kama wa kiroho sana, huku ukitaka kupyaishwa uhusiano wetu na Mungu, sisi kwa sisi na kazi ya uumbaji. Jamii zenu ziwe mifano ya uendelevu wa ikolojia, unyenyekevu na shukrani kwa zawadi za Mungu,” alisisitiza Baba Mtakatifu huku akirudia kutazama Waraka wa Laudato Si' wa Papa Francisko na wito wake wa ikolojia fungamani.
Sala, Sakramenti, na maisha ya kijumuiya
Kwa kuhitimisha hotuba yake, Papa Leo XIV aliwaalika Wajesuit kubaki karibu na Yesu kupitia sala, Sakramenti, na maisha ya kijumuiya. “Kutokana na mizizi hii, mtakuwa na ujasiri wa kutembea popote: kusema ukweli, kupatanisha, kuponya, kufanya kazi kwa ajili ya haki, kuwaweka huru mateka. Hakuna mpaka utakaokuwa nje ya uwezo wenu ikiwa mtatembea na Kristo,"aliwashauri. Papa alielezea matumaini yake kwamba “Jumuiya ya Yesu inaweza kuendelea kusoma ishara za nyakati kwa kina cha kiroho,"kukumbatia kile kinachohamasisha heshima ya mwanadamu na kubaki wenye bidii, wabunifu, wenye utambuzi na daima katika utume. Bwana na awaongoze kwenye mipaka ya leo hii na zaidi, na kupyaisha Kanisa na kujenga Ufalme wa haki, upendo na ukweli.”
