Papa aonya kuhusu sintofahamu kwa anayeteseka,majibu yahitajika kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu leo XIV Alhamisi tarehe 2 Oktoba 2025 alizungumza na washiriki katika Kongamano la Kimataifa kuhusu mada ya "Wakimbizi na Wahamiaji katika Nyumba Yetu ya Pamoja," ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Villanova(Chuo Kikuu alichosomea Robert Francis Prevost mwenyewe), ambapo Kongamano hilo, lililofanyika katika Chuo cha Baba wa Kanisa(Augustinianum)katika siku chache kabla ya Jubilei ya Wamisionari na ya Ulimwengu wa Wahamiaji,kwa kuwaleta pamoja wawakilishi wa vyuo vikuu, mashirika yasiyo ya kiserikali, na washirika wa jamii ili kuandaa mipango ya utekelezaji kushughulikia sababu za kimuundo za uhamaji. Tuanze kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Papa alianza: "Amani iwe nanyi! Habari za asubuhi ninyi nyote na karibuni! Ni furaha yangu kuwakaribisha Vatican kama sehemu ya mkutano wenu ambao mada yake ni, “Wakimbizi na Wahamiaji katika Makao Yetu ya Pamoja.” Ninawashukuru wale ambao wameandaa siku hizi za majadiliano, tafakari, na ushirikiano, pamoja na kila mmoja wenu kwa uwepo wenu na kwa michango yenu katika mpango huu. Muda wenu pamoja huanza mpango wa miaka mitatu kwa lengo la kuunda "mipango ya utekelezaji" inayozingatia nguzo kuu nne: ufundishaji, utafiti, huduma, na utetezi.
Baba Mtakatifu Leo aliendelea kusema kuwa: “Kwa njia hii, wanatii wito wa Baba Mtakatifu Francisko kwa jumuiya za wasomi kusaidia katika kukidhi mahitaji ya kaka na dada zetu waliohamishwa kwa kuzingatia maeneo ambayo ni uwezo wenu (taz. Hotuba kwa Washiriki katika Mkutano wa Wakimbizi Uliohamasishwa na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, 29 Septemba 2022).” Papa alisema kwamba “Nguzo hizi ni sehemu ya dhamira moja: kuleta pamoja sauti zinazoongoza katika taaluma mbalimbali ili kukabiliana na changamoto za dharura za sasa zinazoletwa na kuongezeka kwa idadi ya watu, ambayo sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 100, ambao wameathiriwa na uhamiaji na uhamisho.” Papa aliomba kwamba jitihada zao ziweze kuleta mawazo na mbinu mpya katika suala hilo, kutafuta daima kuweka utu wa kila binadamu katikati ya ufumbuzi wowote. Wanapoendelea na mkusanyiko wao, Papa alipenda kupendekeza mada mbili ambazo wanaweza kufikiria kujumuisha katika mipango yao ya utekelezaji: upatanisho na matumaini.
Moja ya vikwazo ambavyo mara nyingi hutokea wakati wa kukabiliana na matatizo ya ukubwa huo ni mtazamo wa kutojali kwa upande wa taasisi na watu binafsi. Papa amekumbusha urithi wa Mtangulizi wake Baba Mtakatifu Francisko kwamba “alizungumza juu ya "utandawazi wa kutojali," ambapo tunazoea mateso ya wengine na hatujaribu tena kuwapunguzia.” Hii inaweza kusababisha – Papa aliongeza “kile nilichotaja hapo awali kuwa "utandawazi wa kutokuwa na uwezo" ambapo tunahatarisha kutokuwa na uwezo wa kusonga mbele, kimya, labda huzuni, tukifikiri kwamba hakuna kitu kinachoweza kufanywa wakati tunakabiliwa na mateso yasiyo na hatia (Ujumbe wa Video kuhusu Tukio la Uwasilishaji wa Mgombea wa Mpango wa "Ishara za Kukaribisha" katika Orodha ya UNESCO ya Utamaduni wa Mali zisizogusika2022 Septemba 2022). Kama vile Papa Francisko alivyozungumzia utamaduni wa kukutana kama dawa ya utandawazi wa kutojali, ni lazima tufanye kazi ili kukabiliana na utandawazi wa kutokuwa na uwezo kwa kukuza utamaduni wa upatanisho.
Kwa njia hii mahususi ya kukutana na wengine, “tunakutana sisi kwa sisi kwa kuponya majeraha yetu, kusameheana maovu tuliyofanya na pia ambayo hatujafanya, lakini ambayo matokeo yake tunayabeba.” Hili Papa alikazia tena “linahitaji subira, nia ya kusikiliza, uwezo wa kutambua maumivu ya wengine na kutambua kwamba tuna ndoto sawa na matumaini sawa. Kwa njia hiyo Papa alihimiza “kupendekeza njia madhubuti za kukuza ishara na sera za upatanisho, hasa katika nchi ambazo kuna majeraha ya kina kutokana na migogoro ya muda mrefu. Hili si jambo rahisi, lakini ikiwa jitihada za kufanyia kazi mabadiliko ya kudumu zitafanikiwa, lazima zijumuishe njia za kugusa mioyo na akili.” Katika kuandaa mipango yao ya utekelezaji, ni muhimu pia kukumbuka kwamba wahamiaji na wakimbizi wanaweza kuwa mashuhuda wa pekee wa matumaini kupitia uthabiti wao na kupitia imani yao kwa Mungu (taz. Ujumbe kwa Siku ya 111 ya Wahamiaji na Wakimbizi).
Papa Leo XIV amebanisha kwamba “Mara nyingi wao hudumisha nguvu zao huku wakitafuta maisha bora ya baadaye, licha ya vizuizi wanavyokumbana navyo. Tunapojiandaa kusherehekea Jubilei za Wahamiaji na Siku ya Umisionari katika mwaka huu mtakatifu wa Jubile, amewahimiza kukukuza mifano kama hii ya matumaini katika jumuiya za wale unaowahudumia. Kwa njia hii, wanaweza kuwa msukumo kwa wengine na kusaidia katika kutengeneza njia za kushughulikia changamoto ambazo wamekumbana nazo katika maisha yao wenyewe.” Kwa hisia hizi, Papa aliwatakia mema ya mkutano wenye matunda na aliomba kwamba, kwa kuangazwa na Roho Mtakatifu, waendelee kufanya kazi katika kutafuta masuluhisho ya kina ili kukuza utamaduni wa kukutana, upatanisho, na mshikamano wa kidugu kwa manufaa ya wote. Alitoa barala zake kwa wote na kwa wale wote ambao ni sehemu ya utume wao.Aliwashukuru sana na akawaomba kusali Pamoja kama Yesu alivyotufundisha: ile sala ya Baba yetu…
