Papa atembelea Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani:kukuta hadhi ya binadamu
Na Salvatore Cernuzio - Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alitembelea Baraza la Kipapa la Kipapa la kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Kibinadamu, alasiri, alhamisi tarehe 9 Okotba 2025. Alifika katika Jumbla la Mtakatifu Callist, katikati mwa kitongoji cha Trastevere, karibu 9:30 alasiri akihitimisha siku kali iliyoanza na mikutano mitatu. Wakati wa kufika alipewa kitabu cha heshima cha kusaini ambapo aliandika maneno haya: "Katika tukio la ziara yangu katika Baraza hili, siku ile ile ya kuchapishwa kwa Dilexi Te, ninawashukuru ninyi nyote mnaofanya kazi yenu kuwa kielelezo cha kweli cha utume wa Kanisa." Kwa njia hiyo Papa aliishukuru "familia" nzima ya Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Kibinadamu, na Kardinali Michael Czerny, alikuwa miongoni mwa wazungumzaji waliokuwa wakiwasilisha hati hiyo asubuhi ya katika Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican.
Maswali na Salamu
Papa alikumbuka Wosia wake wa kwanza katika kujitolea kwake na kwa wakati alioshiriki na wanachama na wafanyakazi wote wa Baraza la Curia Romana (wengine pia waliunganishwa mtandaoni) katika Ukumbi wa Van Thuan. Wakati "rahisi na wa kina", kama wale waliohudhuria walivyoelezea, wakati ambapo Papa Leo XIV alijibu maswali ya hiari kutoka kwa wafanyakazi, baadhi hasa yakihusiana na wito na mialiko ya utume wa Kanisa na huduma kwa maskini iliyomo katika Dilexi te. "Asante kwa kazi yenu, asante kwa kujitolea kwenu," Papa aliwaambia wafanyakazi wa Baraza hilo, ambalo linafanya kazi kwa ajili ya Vatican ulimwenguni katika maeneo mengi: uhamiaji, uchumi, ikolojia, afya, elimu na usalama.
Wakati wa takriban saa mbili zilizotumika huko Mtakatifu Calist, Papa Leo pia alikuwa na mkutano wa faragha na Mwenyekiti wa Baraza hilo Kardinali Czerny, Katibu Mkuu Sr Alessandra Smerilli, na makatibu i wawili wasaidizi , Kadinali Fabio Baggio na Monsinyo Anthony Ekpo. Zawadi kadhaa ziliwasilishwa kwa Papa, ambaye pia aliwasalimia waliohudhuria mmoja mmoja, akisimama na baadhi kwa mazungumzo. Hasa, Papa alibariki picha iliyowasilishwa kwake na Mercedes de la Torre, mwandishi wa habari wa Mexico na mfanyakazi wa mawasiliano katika Baraza hilo la Kipapa(DSSUI:Ilikuwa ni picha ya mama na baba yake, ambao walifariki mwaka mmoja uliopita. Papa Leo, alimbariki mwanamke huyo na familia yake.
Baraka ya kazi ya sanaa "Mti wa Hadhi ya Binadamu"
Miongoni mwa mambo makuu ya ziara hiyo, hatimaye, ilikuwa ni baraka ya Sanaa ya "Mti wa Hadhi ya Binadamu," ufungaji uliozinduliwa hivi karibuni mwezi Julai iliyopita mwaka huu ambao unawakilisha mwendelezo kati ya siku zilizopita na za sasa. Hivyo basi, mizizi ya Baraza hili lililoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo Januari 2017, baada ya kuunganishwa kwa Mabaraza manne ya Kipapa yaliyopita: Kor Unum, Haki na Amani, Wahamiaji na Wasafiri, na Wahudumu wa Afya. Kutoka katikaa haya, Baraza hili la sasa (DSSUI) ilirithi mada mbalimbali inayozungumzia na dhamira ya kukuza utu wa binadamu wa watu wote, bila ubaguzi, kwa kuzingatia hasa wanyonge, wasiobahatika na waliotengwa.
Salamu kwa Watu
Papa aliwasili Trastevere mapema alasiri, Gari lenye vioo vyeusi lililombeba Papa, likisindikizwa na Maaskari wa Vatican na mawakala wa Ukaguzi wa Vatican, mara moja lilivutia hisia za wakazi, wapita njia, na watalii katika eneo hili katikati mwa Roma, hatua chache tu kutoka kwa Basilika ya Mtakatifu Maria huko Trastevere. Miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika uwanja wa Makao makuu ya Baraza hilo walikuwa wanafunzi kutoka shule ya lugha ya Kiitaliano inayotolewa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa wahamiaji na wakimbizi wote wanaokaribishwa nchini Italia. Wanaume na wanawake darasani wakati huo waliacha kila kitu kutoka nje na kujaribu kumsalimu Papa Leo XIV. Wengi wanatoka Peru, nchi ambayo Robert Francis Prevost alitumikia muda wake akiwa mmisionari kwa zaidi ya miaka ishirini.
Yapata saa kumi na mbili jioni, Papa alitoka nje ya lango kuu, akipunga mkono kutoka dirishani hadi kwa umati uliokusanyika kwenye uwanja huo mdogo, akipunga mkono, wakipiga makofi, na kupiga kelele "E’ Viva Papa” yaani “Uishi Papa!" Hii ni mara ya pili kwa Papa Leo XIV kutembelea moja ya Mabaraza ya Kipapa La kwanza lilikuwa mnamo Mei 20, chini ya majuma mawili baada ya kuchaguliwa kwake katika Kiti cha Mtume Petro, ambapo alikwenda katika Baraza la Kipapa la Maaskofu, Kiungo cha Curia Romana ambacho yeye mwenyewe alihudumu kwa miaka 2 kama Mwenyekiti wa Baraza hilo.
Mchoro "Mti wa Hadhi ya Binadamu"
Kusimikwa kwake mnamo Julai 2025, kunaonesha historia ya Mabaraza manne ya Kipapa yaliyounganishwa na kuwa Baraza moja la Huduma ya Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu tarehe 1 Januari 2017. Wageni wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, watakumbana na usakinishaji wenye urefu wa zaidi ya mita tisa na urefu wa karibu mita tatu, unaoitwa "Mti wa Hadhi ya Binadamu." Madhumuni ya kazi ni kuwakilisha mwendelezo kati ya zamani na sasa. Zamani huungana na za sasa.
Kwa njia hiyo DSSUI ilizaliwa tarehe 1 Januari 2017, kutokana na kuunganishwa kwa Mabaraza manne ya Kipapa yaliyopita: Cor Unum, Haki na Amani, Wahamiaji na Wasafiri, na Wahudumu wa Afya. Kutoka kwa haya, ilirithi mada mbalimbali zilizoshughulika na dhamira yake: kukuza utu wa binadamu wa watu wote, bila ubaguzi, kwa uangalifu maalum kwa wanyonge, wasio na bahati, na waliotengwa. Kwa hiyo matokeo ya mwisho ni picha ya mti mkubwa. Kila Baraza la Kipapa linawakilisha mojawapo ya chimbuko ambalo Baraza lilizaliwa na kuendelezwa.
Mizizi ni imara, na matawi na majani yanawakilisha ukuaji kuelekea wakati ujao wenye heshima zaidi. Vigogo vya mti huo vina majina ya Wenyeviti mbalimbali walioongoza na kutoa msukumo wa kazi za Mabaraza manne ya Kipapa, huku majani yakiwakilishwa na majopo yanayoelezea matukio muhimu na mipango ya ofisi mbalimbali. Huko nyuma, njia ya mawe ya uso kutoka asili, mahalia, na enzi tofauti, inayowakilisha ubinadamu ambao Baraza linatafuta kutumikia, linaunda njia ambayo inatukumbusha Baraza mahali linapotoka na linalosonga mbele.
Kazi hiyo imejengwa karibu kabisa na mti, iliotibiwa na vitu vyenye mazingira rafiki ili kuhakikisha uimara wake. Rangi hurejea asili na Ulimwengu wa mimea. Nia ni kuunganisha tena kazi ya ofisi hii na sayari tunayoishi na ambayo tumeitwa kuishi nayo kwa ushirikiano. Dhana na muundo ni wa Kaleidon, wakati uzalishaji ni wa Mela-P.
Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho, tunakualika kujiandikisha hapa ili kupata habari za kila siku: cliccando qui
