Papa Leo XIV:Hakuna nafasi ya kutojali mbele ya uongofu wa kiikolojia

Katika hotuba ya Papa kwenye Kituo cha Mariapoli cha Wafocolari huko Castel Gandolfo,kama sehemu ya mkutano wa "Kuinua Matumaini juu ya Mabadiliko ya Tabianchi,"alikumbuka Matokeo ya Waraka wa Laudato si',unaoadhimisha miaka10.Alihimiza makampuni na watu binafsi kuweka shinikizo kwa serikali kuunda kanuni za kukabiliana na uharibifu wa mazingira.Kilio cha dunia lazima kisiwe mtindo wa kupita,bali uongofu wa kiikolojia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu ameshiriki ufunguzi wa tukio la Kimatafa, jioni tarehe 1 Oktoba 2025  kwenye Kituo cha Mariapoli cha Wafocolari huko Castel Gandolfo, kama sehemu ya mkutano wa "Kuinua Matumaini juu ya Mabadiliko ya Tabianchi,” ulioandaliwa na Jumuiya ya Laudato si' kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Caritas Internationalis, CIDSE, UISG, Harakati ya Wafocolari,na Mtandao wa Mshikamano wa Kikanisa. Hafla hiyo ya siku mbili, iliyopangwa kufanyika tarehe 2 na 3 Oktoba, itahudhuriwa na zaidi ya watu elfu moja, wakiwemo viongozi kutoka Ulimwengu wa imani tofauti, harakati, sayansi na siasa.

Hotuba ya Papa
Hotuba ya Papa   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu akianza kuwahutubia alitoa salamu ya “amani iwe nanyi.” Akirejea  juu ya taarifa  iliyotolewa hapo awali na Arnold Schwarzenegger, gavana wa zamani wa California na rais wa sasa wa Taasisi ya USC Schwarzenegger, mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo, na ambaye kwanza katika hotuba yake alisema alivyojisikia "kuheshimiwa" kuwa karibu na "shujaa wa hatua. "Kwa njia hiyo,  Papa Leo  XIV alisema: “Kabla ya kuendelea na maelezo machache yaliyotayarishwa, alipenda kuwashukuru wazungumzaji wawili waliomtangulia. Na alipenda kuongeza kwamba “kweli kuna shujaa wa hatua pamoja katika siku hiyo yaani wao wote wanaojikita na shughuli ya pamoja kuleta mabadiliko.”

Gavana wa California na rais wa sasa wa Taasisi ya USC Schwarzenegger akizungumza
Gavana wa California na rais wa sasa wa Taasisi ya USC Schwarzenegger akizungumza   (@Vatican Media)

Tunapoadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya Waraka wa Laudato Si’ kuhusu utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, aliwasalimu kwa moyo mkunjufu waandaaji, wasemaji, washiriki na wale wote waliofanikisha Kongamano la “Kuinua Tumaini." Na aliwashukuru sana Harakati ya Laudato Si’ kwa kuunga mkono usambazaji na utekelezaji wa ujumbe wa Papa Francisko tangu mwanzo. Waraka huu umetia moyo sana Kanisa Katoliki na watu wengi wenye mapenzi mema. Umethibitika kuwa chanzo cha mazungumzo. Umeibua vikundi vya kutafakari, programu za kitaaluma katika shule na Vyuo Vikuu, na ushirikiano na miradi ya aina mbalimbali katika kila bara. Majimbo mengi  na taasisi za kidini zimesukumwa kuchukua hatua ya kutunza nyumba yetu ya pamoja, na kusaidia kwa mara nyingine tena kutoa kipaumbele kwa maskini na waliotengwa katika mchakato huo.

Tukio la Mkutano kuhusu Ikolojia fungamani
Tukio la Mkutano kuhusu Ikolojia fungamani   (@Vatican Media)

Papa alizidi kukazia kuhusu Waraka huo kwamba: "Matokeo yake yameenea hata kwenye mikutano ya kilele ya kimataifa, mazungumzo ya kiekumene na ya kidini, mijadala ya  uchumi na biashara, pamoja na masomo ya kitaalimungu  na kibiolojia. Maneno "kutunza nyumba yetu ya kawaida" pia yamejumuishwa katika hotuba na hotuba za kitaaluma, kisayansi na kisiasa. Wasiwasi na mapendekezo ya Papa Francisko yamethaminiwa na kukubaliwa sio tu na Wakatoliki, lakini pia watu wengi nje ya Kanisa ambao wanahisi kueleweka, kuwakilishwa na kuungwa mkono wakati huu maalum katika historia yetu. Uchambuzi wake wa hali (rej. sura ya 1), pendekezo la dhana ya ikolojia fungamani (rej. Sura ya 4), wito unaosisitiza wa mazungumzo (rej. sura ya 5), ​​na miito ya kushughulikia sababu kuu za matatizo na "kuleta familia nzima ya kibinadamu pamoja kutafuta maendeleo endelevu na fungamani" (na. 13) imeamsha shauku kubwa.

Maadhimisho ya miaka 10 ya Laudato si
Maadhimisho ya miaka 10 ya Laudato si   (@Vatican Media)

Papa alisisitiza kuwa: “Tumshukuru Baba yetu aliye mbinguni kwa zawadi hii tuliyorithi kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko! Changamoto zilizobainishwa katika Laudato Si’ kiukweli zinafaa zaidi leo kuliko ilivyokuwa miaka kumi iliyopita. Changamoto hizi ni za kijamii na kisiasa, lakini kwanza kabisa ni za kiroho: zinataka uongofu. Kama ilivyo kwa kila maadhimisho ya aina hii, tunakumbuka yaliyopita kwa shukrani, lakini pia tunajiuliza ni nini kinachobaki kufanywa. Kwa miaka mingi, tumebadilika kutoka kuelewa na kusoma Waraka  hadi kuuweka katika vitendo.

Papa wakati wa hotuba yake
Papa wakati wa hotuba yake   (@Vatican Media)

Ni nini lazima kifanyike sasa ili kuhakikisha kwamba kutunza makao yetu ya pamoja na kusikiliza kilio cha dunia na maskini hakionekani kuwa mielekeo ya kupita kawaida tu au, baya zaidi, kwamba kunaonekana na kuhisiwa kuwa masuala yenye mgawanyiko? Aliuliza Papa leo XIV.  Kwa mujibu wa Waraka wa Kitume wa Laudato Si’, na  Laudate Deum, iliyochapishwa miaka miwili iliyopita, ilibainisha kwamba “wengine wamechagua kudhihaki” (sura ya 6) ishara zinazozidi kuonekana za mabadiliko ya Tabianchi, “kuwadhihaki wale wanaozungumza juu ya ongezeko la joto duniani” (sura ya 7) na hata kuwalaumu maskini kwa jambo lenyewe linalowaathiri zaidi. Kando na kueneza ujumbe wa Waraka wa Kitume, sasa ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kurudi moyoni.

Mkutano kuhusu "Kuinua matumaini"
Mkutano kuhusu "Kuinua matumaini"   (@Vatican Media)

Katika Maandiko, moyo sio kitovu cha hisia tu na  muhemko, lakini mahali pa uhuru. Ijapokuwa moyo hujumuisha akili, huipita na kuibadilisha, kuathiri na kuunganisha vipengele vyote vya mtu na mahusiano yake ya msingi.  Moyo ni mahali ambapo ukweli wa nje una athari kubwa zaidi, ambapo utafutaji wa kina zaidi unafanyika, ambapo shauku za kweli zaidi zinagunduliwa, ambapo utambulisho wa mwisho wa mtu unapatikana, na ambapo maamuzi yanaundwa. Ni kwa kurudi moyoni tu ndipo uongofu wa kweli wa ikolojia unaweza kutokea. Ni lazima kuhama kutoka kukusanya data na kujali; na kutoka katika mazungumzo ya kimazingira hadi ubadilishaji wa ikolojia ambao hubadilisha mitindo ya maisha ya kibinafsi na ya jumuiya.

Ishara mbali mbali katika tukio la Kuinua matumaini
Ishara mbali mbali katika tukio la Kuinua matumaini   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba: Kwa waamini, uongofu huu kiukweli hauna tofauti na ule unaotuelekeza kwa Mungu aliye hai. Hatuwezi kumpenda Mungu ambaye hatuwezi kumwona, huku tukiwadharau viumbe wake. Wala hatuwezi kujiita wanafunzi wa Yesu Kristo bila kushiriki katika mtazamo wake juu ya uumbaji na utunzaji wake kwa kila kitu ambacho ni dhaifu na kilichojeruhiwa. Papa Leo XIV aliwashauri kuacha imani yao iwatie moyo wa kuwa wabeba tumaini linalotokana na kutambua uwepo wa Mungu tayari wanatenda kazi katika historia. Na amesisitiza kukumbuka  jinsi Papa Francisko alivyomuelezea Mtakatifu Francis wa Assisi: "Aliishi kwa urahisi na kwa maelewano ya ajabu na Mungu, na wengine, na asili na yeye mwenyewe. Anatuonesha jinsi gani kifungo kisichoweza kutenganishwa kati ya kujali kwa asili, haki kwa maskini, kujitolea kwa jamii, na amani ya ndani "(Laudato Si', 10).

Kuinua matumaini
Kuinua matumaini   (@Vatican Media)

 Papa Leo XIV aliongeza kwamba “kila mmoja wetu na akue katika mahusiano haya manne - na Mungu, na wengine, na asili na sisi wenyewe - kupitia mtazamo wa kudumu wa uongofu. Ikolojia fungamani  hustawi kwenye mahusiano haya yote. Kupitia ahadi yao yetu tunaweza kukua katika tumaini kwa kuishi kulingana na mbinu ya Laudato Si’ na wito wa umoja na ushirikiano unaotokana nayo. Sisi ni familia moja, pamoja na Baba mmoja, ambaye huchomoza jua na kuwanyeshea kila mtu mvua (taz. Mt 5:45). Wakati huo huo, Papa Leo XIV aliwahimiza kila mtu, hasa vijana, wazazi na wale wanaofanya kazi katika tawala na taasisi mahalia  na za kitaifa, kutekeleza sehemu yao katika kutafuta ufumbuzi wa "changamoto za kiutamaduni, kiroho na elimu" za leo (Laudato Si', 202), daima kujitahidi kwa bidii kwa manufaa ya wote. Hakuna nafasi ya kutojali au kujiuzulu.

Kituo cha Mariapoli
Kituo cha Mariapoli   (@Vatican Media)
Ukumbi ulijaa
Ukumbi ulijaa   (@Vatican Media)

Papa Leo alipenda kuhitimisha “kwa swali linalomhusu kila mmoja wetu. Mungu atatuuliza ikiwa tumelima na kutunza ulimwengu aliouumba (rej. Mwa 2:15), kwa manufaa ya wote na kwa vizazi vijavyo, na ikiwa tumewatunza kaka  na dada zetu(rej. Mw 4:9; Yh 13:34). Jibu letu litakuwa nini? Papa Leo XIV  akiwageukia wote tena aliwashurku kwa kujitolea kwao na aliwapatia baraka zake za furaha. Asante”

Maadhimisho ya miaka 10 ya Laudato si
Maadhimisho ya miaka 10 ya Laudato si   (@Vatican Media)
Papa katika Kituo cha Mariapoli
Papa katika Kituo cha Mariapoli   (@Vatican Media)
Papa na raising hope
01 Oktoba 2025, 18:53