2025.10.23 Wanachama wa Shirika la Kaburi la Takatifu la Yerusalemu. 2025.10.23 Wanachama wa Shirika la Kaburi la Takatifu la Yerusalemu.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Shirika la Kaburi Takatifu: shuhudia upendo unaoshinda chuki na kisasi

Kuhushudia upendo na msamaha katika ulimwengu uliojaa nguvu na gahsia ni ushauri wa Baba Mtakatifu Leo XIV katika hotuba yake kwa zaidi ya mahujaji elfu tatu wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu aliokutana nao katika Ukumbi wa Paulo VI.Papa aliwashukuru kwa msaada wao kwa jumuiya za Nchi Takatifu wakati wa Uviko na vita na kwa jukumu lao kama walinzi wa imani katika maeneo ambayo Yesu aliishi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu  Leo XIV alikutana na wanashirika wapatao 3,600 Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu, waliopokelewa katika Ukumbi wa Paulo VI mwishoni mwa hija yao ya Jubilei, Alhamisi tarehe 23 Oktoba 2025. Baada ya salamu kutoka kwa Mkuu wa Shirika hilo Kardinali Fernando Filoni, Papa  Leo alikumbusha kwamba, ulinzi wa Kaburi la Kristo, uangalizi wa mahujaji, na msaada kwa Kanisa la Yerusalemu ni chimbuko la historia ya taasisi hiyo. Na kwa njia hiyo Ibada inayoendelea leo kwa Wakristo wote wanaoishi katika Maeneo Matakatifu, alisisitiza, akimnukuu Mtakatifu Yohane Paulo II, kuwa bila kelele na utangazaji, na kuunga mkono seminari, shule, kazi za upendo na usaidizi, mipango ya kibinadamu na elimu, chuo kikuu, na msaada kwa Makanisa, kwa uingiliaji maalum wakati wa shida kubwa. Katika haya yote, wanaonesha kwamba kulinda Kaburi la Kristo haimaanishi  kuhifadhi tu urithi wa kihistoria, kiakiolojia, au kisanii, hata kama ni muhimu, lakini kuunga mkono Kanisa lililoundwa kwa mawe hai, ambalo lilizaliwa karibu nalo na bado linaishi leo, kama ishara halisi ya tumaini la Pasaka.

Papa akutana na Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu
Papa akutana na Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu   (@Vatican Media)

Ni katika muktadha huo ambapo Papa alitoa Asante kwa msaada wa ajabu kwa jumuiya za Nchi Takatifu, kupitia usaidizi kwa shughuli za Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, ambayo ilikuwa muhimu wakati wa uviko na katika siku za kutisha za vita. Mwaliko wa kuendelea kuwa  walinzi wa imani kwa wale wanaosimama kwenye kaburi la Kristo, katika tumaini la kutazamia, katika bidii ya mapendo, na katika msukumo wa furaha ya tumaini.

Na katika Jubilei iliyowekwa kwao, Papa Leo XIV   kwa shirika hili alisisitiza mambo matatu: La kwanza ni "tarajio la kutumaini" la wale wanaosimama kwenye Kaburi la Bwana na kupyaisha  imani yao katika Mungu "ambaye hutimiza ahadi zake. Katika ulimwengu ambapo kiburi na jeuri vinaonekana kutawala juu ya upendo, wameitwa kushuhudia kwamba uzima hushinda kifo, kwamba upendo hushinda chuki, kwamba msamaha hushinda kisasi, na kwamba huruma na neema hushinda dhambi. Ili kuendeleza ulinzi wa imani yao  katika Mahali Patakatifu, Baba Mtakatifu aliwaalika wanashirika hao kulisha mioyo yao kwa maisha marefu ya sakramenti, kwa kusikiliza na kutafakari Neno la Mungu, kwa sala ya kibinafsi na ya kiliturujia, na kwa malezi ya kiroho ambayo yanathaminiwa sana katika shirika hilo.

Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu
Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu   (@Vatican Media)

Mwelekeo wa pili wa matumaini, kwa Papa, ni uso wa huduma, ule wa wanawake waliokwenda kwenye kaburi kupaka mafuta mwili wa Yesu, ambao shirika linaendelea kufuatia mapokeo ya kale ya usaidizi. Papa aliongeza “Ni mara ngapi, shukrani kwa kazi yenu, mwangaza wa nuru hufunguka tena kwa watu binafsi, familia, na jumuiya nzima ambayo iko katika hatari ya kulemewa na misiba mbaya, katika kila ngazi, hasa katika maeneo ambayo Yesu aliishi.” Mwelekeo wa tatu, hatimaye, ni ule unaotuongoza kutazama lengo, kama Petro na Yohane ambao walikimbia kuelekea Kaburi asubuhi ya Pasaka. Lengo hili ni kukutana na Bwana, kama kwa hija, katika kutafuta maana kuu ya maisha.

Papa akutana na Shirika la kaburi Takatifu la Yerusalemu mjini Vatican.
Papa akutana na Shirika la kaburi Takatifu la Yerusalemu mjini Vatican.   (@Vatican Media)

Kwa hiyo Papa Leo alisema kwamba kuwapo hapo katika siku hiyo kuwepo hapo sio hatua ya kuwasili, lakini pia hatua kuelekea lengo la uhakika, la ushirika kamili na wa milele na Mungu Mbinguni. Kwa njia hiyo aliwaomba waifanye pia kuwa ushuhuda kwa kaka na dada unaokutana nao: kuwa mwaliko wa kuona mambo ya Ulimwengu huu kwa uhuru na furaha ya wale wanaojua wanasafiri kuelekea upeo wa milele usio na kikomo. Katika kulikabidhi Shirika la  Kaburi Takatifu, kwa niaba ya Kanisa, jukumu la kuwa walinzi wa Kaburi la Kristo, Baba Mtakatifu  Leo alinukuu mwaliko wa Mtakatifu Agostino kwa Wakristo wa wakati wake: "kusonga mbele, kwenda mbele kwa wema. wasipotee, wasirudi nyuma, na wala wasisimame!"

23 Oktoba 2025, 11:55