Shirikisho la Waagostiani kutoka Mexico "Agostiniane Recollette della Federazione del Messico" Jumatano tarehe 15 Oktoba 2025 wamekutana na Papa Leo XIV mjini Vatican. Shirikisho la Waagostiani kutoka Mexico "Agostiniane Recollette della Federazione del Messico" Jumatano tarehe 15 Oktoba 2025 wamekutana na Papa Leo XIV mjini Vatican.  (@Vatican Media)

Shirikisho la Watawa wa Augustiani: Rehema na Ukweli: Njia ya Upendo!

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 15 Oktoba 2025 amekutana na Wamonaki wa Shirika la Waagustiniani la Recollete: “Ordo Augustinianorum Recollectorum.” Amewaambia kwamba, hija hii ni wakati muafaka wa kukutana na Kristo Yesu, anayewajaza furaha isiyokuwa na kifani kama anavyosema Mtakatifu Thomas wa Villanova kwamba, Kristo Yesu ni thawabu isiyopimika na kwamba, ili kuweza kukutana na Kristo Yesu wanapaswa kujikita katika njia ya rehema na ukweli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirikisho la Shirika la Waagustiniani la Recollete kutoka Mexico: “Ordo Augustinianorum Recollectorum” ni la Watawa lenye hadhi ya Mashirika ya Kipapa lililoanzishwa kunako mwaka 1589, huko nchini Mexico na kuenea sana nchini: Hispania, Marekani na Ufilippin. Wamonaki hawa, Jumatano tarehe 15 Oktoba 2025 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Leo XIV, kama sehemu ya hija ya maisha ya kiroho katika maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo yanayonogeshwa na Tamko la “Spes non confundit" yaani “Tumaini halitahayarishi.” Rum 5:5 na kwamba, kiini cha maadhimisho haya ni matumaini yatakayowawezesha watu waaminifu wa Mungu kutoka sehemu mbalimbali za dunia kufanya hija ya maisha ya kiroho mjini Roma sanjari na maadhimisho haya kufanyika kwenye Makanisa mahalia, ili kukutana na Kristo Yesu aliye hai na ambaye pia ni Mlango wa uzima. Rej, Yn 10:7.9.

Shirikisho la Waagustiani kutoka Mexico
Shirikisho la Waagustiani kutoka Mexico   (@Vatican Media)

Mama Kanisa anaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini dhidi ya hofu na mashaka; ukosefu wa imani na furaha ya kweli. Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo yanayonogeshwa na kauli mbiu “Peregrinantes in spem” yaani: “Mahujaji wa Matumaini.” Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo, Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana na kuzungumza na Wamonaki wa Shirika la Waagustiniani la Recollete: “Ordo Augustinianorum Recollectorum.” Amewaambia kwamba, hija hii ni wakati muafaka wa kukutana na Kristo Yesu, anayewajaza furaha isiyokuwa na kifani kama anavyosema Mtakatifu Thomas wa Villanova kwamba, Kristo Yesu ni thawabu isiyopimika na kwamba, ili kuweza kukutana na Kristo Yesu wanapaswa kujikita katika njia ya rehema na ukweli. Rej. Zab 24:10.

Hii ni hija ya kukutana na Kristo Yesu katika maisha yao
Hii ni hija ya kukutana na Kristo Yesu katika maisha yao   (@Vatican Media)

Katika njia hizi mbili kama mahujaji wa matumaini wanaelekea kwa Kristo Yesu, huku wakitumikia kama ilivyokuwa kwa Martha katika kazi za rehema au kupumzika miguuni mwa Kristo Yesu na kumsikiliza kwa makini kama ilivyokuwa kwa Maria, Dada yake Lazaro, ili kutafakari ukweli. Rej. Lk 10:38-41. Hii ndiyo njia ambayo Mtakatifu Thomas wa Villanova anavyowafundisha, yaani Njia ya Upendo na kwamba, inapendeza zaidi ikiwa kama watajikita katika upendo kwa Mungu na jirani zao na kwamba, kwa njia hii wataweza kufikia lengo kuu katika maisha yao.

Muhimu: Kujikita katika njia ya rehema na ukweli
Muhimu: Kujikita katika njia ya rehema na ukweli   (@Vatican Media)

Upendo huu sio kitu kinachopatikana kwa juhudi binafsi au kwa nguvu bali unapaswa kupokelewa kama zawadi, safari inayoanzia kutoka katika sakafu ya nyoyo zao, ili kuweza kukutana na Mwenyezi Mungu na hivyo kupokea upendo wake. “Mungu, kwa kweli, haangalii ni nini au kiasi gani unafanya, bali ni kiasi gani unakua katika hamu na upendo Kwake, kwa sababu, hata ikiwa ni kweli kwamba kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake, walakini thamani ya matendo iko katika upendo wa moyo. Zaidi ya hayo, ikiwa moto wa upendo haupo, kazi hupoteza maana na kuwa "mzigo kwa roho," lakini "palipo na upendo, hakuna maumivu.” Baba Mtakatifu amewashauri watawa hawa kuomba ulinzi na tunza ya kina kutoka kwa Bikira Maria Mwema na kwa maombezi ya Mtakatifu Thomas wa Villanova, ambaye alipenda sana kutekeleza  utume wake huko Amerika ya Kusini, ili waweze kutembea katika njia hii ya ukamilifu kwa uvumilivu na ujasiri, ili hatimaye kuweza kufikia lengo kuu la maisha yao.

Shirikisho la Watawa
15 Oktoba 2025, 15:47