Katekesi Papa Leo XIV:Kutumaini ni kuwa na msimamo:Dorothy Day

Katika Katekesi kuhusu Jubilei,iliyotanguliwa na kuzunguka kwa Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Novemba 22,Papa Leo alieleza sura nyingine ya Dorothy Day,mwanaharakati wa Marekani aliyebadilisha maisha yake baada ya kukutana na Ukatoliki,akijitolea kikamilifu kwa waliotengwa mwanzoni mwa karne ya ishirini na kuwa bingwa wa upatanisho.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV katika mwendelezo wa Katekesi za Jubilei, Jumamamisi tarehe 22 Novemba 2025 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, ambapo kabla ya kuanza tafakakari alizungukia uwanja na kuwasalimu huku akiwakumbatia na kuwabariki watoto wadogo. Papa aliongozwa na mada ya “Kutumiani ni kuwa na  msimamo.” Dorothy Day.” Hii ni sura nyingine  ya  mwanaharakati wa Marekani aliyebadilisha maisha yake baada ya kukutana na Ukatoliki, huku akijitolea kikamilifu kwa waliotengwa mwanzoni mwa karne ya ishirini na kuwa bingwa wa upatanisho. "Dorothy Day aliandika kama mwandishi wa habari; alifikiri na kuwafanya wengine wafikiri. Uandishi ni muhimu. Na ndivyo ilivyo kwa leo hii kusoma, zaidi ya hapo awali. Kisha Dorothy Day alihudumia milo, alitoa nguo, akavaa na kula kama wale aliowahudumia: aliunganisha akili, moyo na mikono." Kwa njia hiyo ilisomwa Injili kwa lugha mbali mbali:

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@VATICAN MEDIA)

"Kwa kila mtu aliyepewa vingi, vingi vitahitajika; na kwa yule aliyekabidhiwa vingi, zaidi vitahitajika. Nimekuja kuleta moto duniani, na laiti ungekuwa tayari umewashwa! Nina ubatizo wa kubatizwa nao, na nina huzuni sana hadi ukamilike!(Lc 12,48-50.)

Papa akibariki watoto
Papa akibariki watoto   (@Vatican Media)

Papa Leo  alianza kuwasalimia na kusema kuwa “Kwa wengi wenu, kuwa Roma leo ni utimilifu wa hamu kubwa. Kwa wale walio kwenye hija na kufikia mwisho wao, ni muhimu kukumbuka wakati wa kufanya uamuzi. Kuna kitu, mwanzoni, kilihamia ndani yenu, labda kutokana na neno au mwaliko wa mtu mwingine. Hivyo, Bwana mwenyewe alitushika mkono: shauku na kisha uamuzi. Bila hili, usingekuwa hapa. Ni muhimu kukumbuka hili.

Papa alisema kwamba "Na kile tulichosikia muda mfupi uliopita kutoka kwa Injili pia ni muhimu: "Yeyote aliyepewa mengi, mengi yatahitajika; ambaye amekabidhiwa mengi, mengi zaidi yataombwa." Yesu anasema hivi kwa wanafunzi wake wa karibu, kwa wale waliokuwa karibu naye. Na sisi pia tumepokea mengi kutokana na safari tuliyofanya hadi sasa; tumekuwa pamoja na Yesu na Kanisa, na ingawa Kanisa ni jumuiya yenye mapungufu ya kibinadamu, tumepokea mengi. Kwa hivyo, Yesu anatarajia mengi kutoka kwetu. Ni ishara ya uaminifu, ishara ya urafiki. Anatarajia mengi kwa sababu anatujua na anajua tunaweza kuyafanya!

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@VATICAN MEDIA)

Papa alikazia kusema kuwa "Yesu alikuja kuleta moto: moto wa upendo wa Mungu duniani na moto wa hamu ya mioyoni mwetu. Kwa namna fulani, Yesu anaondoa amani yetu ikiwa tunaiona amani kama utulivu usio na kitu. Hata hivyo, hii si amani ya kweli. Wakati mwingine tunatamani "tungeachwa peke yetu": kwamba hakuna mtu anayetusumbua, kwamba wengine hawapo tena. Sio  amani ya Mungu. Amani ambayo Yesu analeta ni kama moto na inatutaka mengi. Zaidi ya yote, inatuomba tuwe na msimamo. Katika hali ya ukosefu wa haki, ukosefu wa usawa, ambapo heshima ya binadamu inakanyagwa, ambapo walio dhaifu wananyimwa uwezo wa kusema: kuwa na  msimamo. Kutumaini ni kuwa msimamo. Kutumaini ni kuelewa moyoni na kuonesha kwa vitendo kwamba mambo hayapaswi kuendelea kama hapo awali. Huu pia ni moto mzuri wa Injili."

Wanahija wa matumaini
Wanahija wa matumaini   (@Vatican Media)

Sura ya Dorothy Day

Papa Leo kwa njia hiyo alisema kwamba alitaka  kumkumbuka mwanamke mdogo, mkubwa wa Marekani, Dorothy Day, aliyeishi katika karne iliyopita. Alikuwa na moto ndani. Dorothy Day alichukua msimamo. Aliona kwamba mfumo wa maendeleo wa nchi yake haukuunda fursa sawa kwa kila mtu. Alielewa kwamba kwa wengi sana, ndoto hiyo ilikuwa ndoto mbaya. Kama Mkristo, ilibidi ashirikiane na wafanyakazi, wahamiaji, na wale waliokataliwa na uchumi unaoua. Aliandika na kutumikia: ni muhimu kuunganisha akili, moyo, na mikono.

Dorothy Day, mwanamke mashuhuri  wa Marekani
Dorothy Day, mwanamke mashuhuri wa Marekani

Hii ni kuwa na  msimamo. Aliandika kama mwandishi wa habari; yaani, alifikiri na kuwafanya wengine wafikiri. Uandishi ni muhimu. Na ndivyo ilivyo kwa leo hii kusoma, zaidi ya hapo awali. Na kisha Dorothy alihudumia milo, alitoa nguo, akavaa na kula kama wale aliowahudumia: aliunganisha akili, moyo, na mikono. Kwa njia hiyo, kutumaini ni kuwa na msimamo. Dorothy Day alihusisha maelfu ya watu.

Bendi ikitumbuiza Papa
Bendi ikitumbuiza Papa   (@Vatican Media)

Papa alisisitiza juu ya sura hii ya mwanaharakati wa upendo kuwa "Alifungua nyumba katika miji mingi, katika vitongoji vingi: sio vituo vikubwa vya huduma, lakini vituo vya upendo na haki ambapo wangeweza kuitana kwa majina, kufahamiana mmoja baada ya mwingine, na kubadilisha hasira kuwa ushirika na vitendo." Hivi ndivyo wapatanishi walivyo yaani wanakuwa na msimamo na kubeba matokeo, lakini wanaendelea mbele. Kutumaini kunamaanisha kuwa na msimamo, kama Yesu, pamoja na Yesu. Moto wake ni moto wetu. kwa kuhitimisha Papa alisema  "Jubilei na iwashe tena ndani yetu na katika Kanisa lote!"

22 Novemba 2025, 14:40