Barua ya Kitume ya Papa Leo XIV: 'In unitate Fidei.'Wakristo waungane kwa ishara ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika umoja wa imani, uliotangazwa tangu asili ya Kanisa, Wakristo wanaitwa kutembea kwa amani, wakilinda na kusambaza zawadi waliyopokea kwa upendo na furaha. Hili linaoneshwa katika maneno ya Imani: "Tunasadiki kwa Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, aliyeshuka kutoka mbinguni kwa ajili ya wokovu wetu, iliyoandaliwa na Mtaguso wa Nicaea, mnamo 325 katika tukio la kwanza la kiekumene katika historia ya Ukristo, miaka 1700 iliyopita. Ni katika Barua ya Kitume ya Baba Mtakatifu Leo XIV iliyopewa jina la In unitate fidei yaani Katika umoja wa imani, katika fursa ya kumbukumbu miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicaea," ambayo aliwasilisha kwa Kanisa tarehe 23 Novemba 2025,katika Sherehe ya Yesu Kristo, Mfalme wa Ulimwengu, siku chache kabla ya kuanza ziara yake ya kwanza ya kitume nchini Urutuki iyakayomuona pia nchini Lebanon ili kuhimiza msukumo mpya katika ungamo moja la imani, ambalo ukweli wake, ambao kwa karne nyingi umekuwa urithi wa pamoja kati ya Wakristo, unastahili kusadiki na kuchunguzwa kwa njia mpya na ya wakati unaofaa.
Uchunguzi wa dhamiri
Baba Mtakatifu Leo, anarejea Hati ya Tume ya Kitaalimungu ya Kimataifa: yenye kichwa: "Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Mwokozi. Maadhimisho ya Miaka 1700 ya Baraza la Kiekumeni la Nicea,"(https://www.vatican.va/roman_curia/congregations/cfaith/cti_documents/rc_cti_doc_20250403_1700-nicea_en.html kwa uelewa wa kina na muhimu, si tu wa kitaalimgunu na kikanisa, bali pia wa kiutamaduni na kijamii, wa Mtaguso wa Nicea"na inahimiza uchunguzi wa dhamiri, ikipata msukumo kutoka katika kanuni ya Imani ya Nicea, ambayo "inaanza kwa kukiri imani katika Mungu, Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia: 'Mungu anamaanisha nini kwangu, na ninawezaje kushuhudia imani yangu kwake?' Je, Yeye ndiye "Mungu mmoja na wa pekee," au kuna "sanamu muhimu zaidi" kuliko Yeye "na amri zake?" "Je, Yeye ndiye Muumba ambaye nina deni lake lote nililo na nililonalo, ambaye ninaweza kumpata katika kila kiumbe? Je, niko tayari kushiriki mali za dunia, ambazo ni za wote, kwa njia ya haki na usawa?" "Je, ninanyonya" uumbaji, "je, ninauharibu, badala ya kuulinda na kuukuza kama makao ya kawaida ya wanadamu?"
Imani katika Kristo inatoa matumaini
Moyo wa imani ya Kikristo ni ungamo la imani katika Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Baba Mtakatifu Leo anarudia, akitangaza kuhusu tamko la Nicea, kwamba bado linatamkwa hata leo wakati wa Misa katika kanuni ya Imani ya Nicea ambayo inawaunganisha Wakristo wote" na "inatupatia tumaini katika nyakati ngumu tunazoishi, katikati ya wasiwasi na hofu nyingi, vitisho vya vita na vurugu, majanga ya asili, dhuluma kubwa na ukosefu wa usawa, njaa na umaskini unaowatesa mamilioni ya watu."
Jumuiya ya Kikristo ya Ulimwenguni: Ishara ya Amani
Katika maandishi, Papa Leo anarudia historia ya Mtaguso wa Kwanza wa Nicea na anazingatia kanuni ya Imani iliyoandaliwa na Mtaguso huo. Kisha Papa anatoa mwaliko wa kutafakari imani katika Mungu katika wakati huu, juu ya Sadaka ya Kristo, aliyekufa msalabani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, "akitufungulia njia ya maisha mapya kwa ufufuko wake na kupaa kwake, juu ya upendo wa jirani uliohubiriwa na Yesu, na juu ya "thamani ya juu zaidi ya kiekumene" ya Mtaguso wa Nicea. Harakati ya kiekumeni inategemea mwisho, na imepata matokeo mengi katika kipindi cha miaka sitini iliyopita.
Na ikiwa umoja kamili unaoonekana na Makanisa ya Kororthodox na yale ya Kiorthodox ya Mashariki na jumuiya za kikanisa zilizozaliwa kutokana na Mageuzi ya Kanisa bado hayajapewa kwetu hasa mazungumzo ya kiekumene yametuongoza kutambua kama kaka na dada zetu katika Yesu Kristo wale ambao ni wa Makanisa mengine na jumuiya za kikanisa na kugundua upya jumuiya moja na ya ulimwengu mzima ya wanafunzi wa Kristo ulimwenguni kote. Katika ulimwengu wa leo, uliogawanyika na kuharibiwa na migogoro mingi, hii inaweza kuwa ishara ya amani na chombo cha upatanisho, ikichangia kwa dhati kujitolea kwa amani duniani kote," Papa anasema.
Kutembea pamoja ili kufikia umoja
Kwa maana hiyo , kumbukumbu ya mashahidi wengi Wakristo kutoka Makanisa yote na jumuiya za kikanisa ambao ushuhuda wao ulikumbukwa na Yohane Paulo II, unatuunganisha na unatutia moyo kuwa mashahidi na wafanyakazi wa amani duniani, ambaye anahimiza: "Ili kutekeleza huduma hii kwa uaminifu, lazima tutembee pamoja ili kufikia umoja na upatanisho miongoni mwa Wakristo wote. Kanuni ya Imani ya Nicea inaweza kuwa msingi na kigezo cha marejeo kwa safari hii. Kiukweli, inatupatia mfano wa umoja wa kweli katika utofauti halali. Umoja katika Utatu, Utatu katika Umoja, kwa sababu umoja bila wingi ni udhalimu, wingi bila umoja ni kutengana." Zaidi ya hayo, Papa Leo anatoa wito wa kuacha mabishano ya kitaalimungu ambayo yamepoteza sababu yao ya kuwa ili kupata uelewa wa pamoja na, zaidi ya hayo, sala ya pamoja kwa Roho Mtakatifu, ili atukusanye sote katika imani moja na upendo mmoja.
Kusikilizana ili kurejesha umoja miongoni mwa Wakristo
Kile ambacho Papa anarejea si uekumene wa kurudi nyuma katika mgawanyiko wa mwanzoni wala utambuzi wa pamoja wa hali ya sasa ya utofauti wa Makanisa na jumuiya za kikanisa. Badala yake, ni uekumene unaolenga mustakabali, wa upatanisho kupitia mazungumzo, wa kubadilishana "zawadi za kiroho na urithi. Kurejesha umoja miongoni mwa Wakristo hakutufanyi kuwa maskini; kinyume chake, kunatutajirisha. Kama ilivyo katika Mtaguso wa Nicea, hii itawezekana tu kupitia safari ya uvumilivu, ndefu, na wakati mwingine ngumu ya kusikilizana na kukubaliana. Hii ni changamoto ya kitaalimungu na, zaidi ya hayo, changamoto ya kiroho, inayohitaji toba na uongofu kutoka kwa wote. Kwa sababu hiyo, tunahitaji umoja wa kiroho wa maombi, sifa, na ibada, kama ilivyo katika Imani ya Nicea na Constantine
Yaliyomo katika Kanuni ya Imani ya Nicea
Tukirudi nyuma katika wakati, Papa Leo anakumbusha kwamba Mtaguso wa Nicea ulianza wakati wa mmojawapo wa migogoro mikubwa zaidi katika historia ya Kanisa la milenia ya kwanza, wakati mzozo wa Arian ulipokuwa ukipamba moto, na kwamba mwishoni mwa mkutano, maaskofu, walioitwa na Mfalme Constantine ili kurejesha umoja katika Kanisa, walionesha imani yao katika Mungu mmoja na wa pekee na kukiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwa sababu yeye ni 'kiini(ousia) cha Baba [...] aliyezaliwa, bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja (homooúsios) sawa na Baba kwa hivyo kukataa "tasnifu ya Arian."
Imekuwaje kuhusu mapokezi ya ndani ya Imani leo?
Lakini safari ya Papa si rahisi ya kihistoria. Akitambua uhusiano mkubwa wa leo hii kati ya liturujia na maisha ya Kikristo na Kanuni ya Imani ya Nicea na Constantinopoli, na kwa kutambua kuwa siku ya sasa, anauliza kuwa "imekuwaje kuhusu mapokezi ya ndani ya Imani leo hii," na kubanisha kwamba kwa wengi, Mungu na swali la Mungu havina maana yoyote maishani, na kwamba, kama Waraka wa Mtaguso wa Gaudium et spes, "Wakristo wanawajibika kwa kiasi fulani kwa hali hii, kwa sababu hawashuhudii imani ya kweli na kuficha uso wa kweli wa Mungu kwa mitindo ya maisha na matendo yaliyo mbali na Injili.
Na imetokea kwamba vita vimepiganwa, mauaji, mateso, na ubaguzi vimetokea kwa jina la Mungu badala ya kumtangaza Mungu mwenye huruma na kumekuwa na mazungumzo ya Mungu mwenye kisasi anayechochea hofu na kuadhibu. Na badala yake, kwa kuwa "kitovu cha Imani ya Nicea-Constantinopoli" ni kukiri imani katika Yesu Kristo, Bwana na Mungu wetu, lazima tujitoe kumfuata Yesu kama Mwalimu, mwenzake, ndugu, na rafiki, tukikumbuka kwamba njia yake si njia pana na ya starehe, bali ni njia, ambayo mara nyingi huwa na changamoto au hata chungu," na kwamba "ikiwa Mungu anatupenda sisi sote, basi pia sote lazima tupendane.
Hati kamili unaweza kuipata hapa:https://www.vatican.va/content/leo-xiv/en/apost_letters/documents/20251123-in-unitate-fidei.html
Katika kumfuata Yesu, kupaa kwa Mungu hupitia kushuka na kujitolea kwa kaka na dada zetu, Papa Leo XIV alisisitiza kwamba hasa kwa walio na bahati mbaya zaidi, maskini zaidi, walioachwa, na waliotengwa. Na hivyo, katika kukabiliana na majanga, vita, na umaskini, tunaweza kushuhudia huruma ya Mungu kwa wale wanaomtilia shaka ikiwa wanapata huruma yake kupitia sisi, Papa Leo anahitimisha, Barua yake ya Kitume kwa sala kwa Roho Mtakatifu.
Bila Yeye hatuwezi kufanya chochote
Baba Mtakatifu anasali hivi: Wewe, Roho wa milele wa Mungu, fufua imani ya Kanisa kutoka kizazi hadi kizazi. Tusaidie kuiimarisha na kurudia mambo muhimu kila wakati ili kuitangaza. Ili ushuhuda wetu duniani usiwe mgumu, njoo, Roho Mtakatifu, kwa moto wako wa neema, uifufue imani yetu, utuwashe kwa tumaini, utuwashe kwa upendo. Njoo, Mfariji wa Mungu, wewe uliye na maelewano, kuunganisha mioyo na akili za waumini. Njoo utujalie kufurahia uzuri wa ushirika. Njoo, Upendo wa Baba na Mwana, utukusanye katika kundi moja la Kristo. Tuoneshe njia za kufuata, ili kwa hekima yako tuweze kurudi kuwa kile tulicho katika Kristo: kitu kimoja, ili ulimwengu upate kuamini. Amina.
