Zahanati ya Mt.Martino inazinduliwa katika nguzo za Mtakatifu Petro
Vatican News
Chini ya Nguzo, muundo mpya wa Upendo wa Kitume unafunguliwa ili kuongeza huduma za afya zinazotolewa kwa maskini na kwa huduma ya Picha ili kugundua mara moja magonjwa ya mara kwa mara kwa wale wanaoishi mitaani.
Uso wa Yesu kwa Maskini
Kituo kilichoanzishwa kwa ushirikiano na Kurugenzi ya Afya na Usafi ya Gavana wa Jiji la Vatican ambacho hutoa huduma kamili kwa wale wanaotafuta msaada. Mahali ambapo watu wanakaribishwa na kutunzwa, hivyo kurejesha heshima kwa maskini wanaobisha mlango wa Ofisi ya Misaada, wale wanaohitaji "ambao ndani yao hatuoni mtu asiye na makazi, mtu maskini, bali uso wa Yesu," alisisitiza Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo.
Huduma ya Afya Bila Malipo
Kwa hivyo, Zahatani ya Mtakatifu Martino inakamilisha Zahanati ya ya 'Madre di Misericordia,'- 'Mama wa Huruma' ambayo hutoa huduma ya afya bila malipo kila siku kwa wale wanaoishi katika umaskini, kutengwa, au shida, ikitegemea moja kwa moja kanuni za Injili na Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa.
Katika Zahanati ya Baraza la Kipapa la Upendo, zaidi ya huduma 2,000 za afya hutolewa bure kabisa kila mwezi kutokana na kazi ya madaktari, wauguzi, na wataalamu wa afya 120 wa kujitolea. Takriban watu maskini 10,000 wa mataifa 139 tofauti wanasaidiwa. Hadi sasa, huduma za afya hiyo za watu 102,060 zimetolewa bure kabisa kwa wale wanaohitaji zaidi na vifurushi 141,200 vya dawa vimesambazwa.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
