Papa Leo XIV:Uelewa Zaidi Kuhusu Matatizo Yanayohusiana na Ukosefu wa Ajira
Vatican News
"Uelewa mpya wa taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii kuhusu matatizo yanayohusiana na ukosefu wa ajira." Hili ndilo tumaini lililotolewa na Papa Leo XIV kwa washiriki wa Mkutano Mkuu Mafundi na Biashara ndogo ndogo (Confartigianato), tukio la kila mwaka kwa mafundi wa Italia na biashara ndogo ndogo, ambalo lilifunguliwa tarehe 25 Novemba 2025, katika Ukumbi wa Conciliazione jijini Roma.
Katika ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, uliosomwa wakati wa ufunguzi wa mkutano, Papa "alihimiza uvumilivu katika kukuza utamaduni wa mshikamano na haki kulingana na maadili ya kiinjili." Papa Leo XIV pia aliwahakikishia wote waliohudhuria maombi yake na akatuma baraka zake. Hawa ni pamoja na wajasiriamali na wawakilishi wa Mfumo wa Confartigianato kutoka Italia yote, viongozi wa taasisi, wawakilishi wa Bunge, na wawakilishi wa vikundi vya kiuchumi na kijamii nchini Italia.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
