Papa Leo alichaguliwa tarehe 8 Mei 2025. Papa Leo alichaguliwa tarehe 8 Mei 2025. 

Miezi sita na Papa Leo XIV:Kanisa lililoungana na wazi,ishara ya amani kwa dunia iliyojeruhiwa na chuki

Kuna mwongozo stahiki unaopita katika Majisterio ya Papa mpya anayependekeza mtindo wa Jumuiya ya Kikristo,ya kimisionari katika asili ambapo wanaishi kwa ushirika,umisionaria,hivyo uwezo wa kuwahudumia wote,kuanzia wa mwisho;kujitolea kukuza mazungumzo na amani.Kanisa "lisiloegemea”wenye nguvu wala halichanganyi utume na biashara ya kidini,bali linajua jinsi ya kuwa chachu kwa sababu linaakisi mwanga wa Mwingine.

Andrea Tornielli.

Imepita miezi sita tangu wakati ule wa mchana wa tarehe 8 Mei wakati Askofu wa Roma, Papa wa kwanza wa Marekani na Muagostino, alipochunguliwa kupitia dirisha kubwa la Basilika ya Mtakatifu Petro. Kuna mwongozi stahiki wa kawaida unaopitia mafundisho yake: Kanisa ambalo ni ishara ya umoja na ushirika, chachu ya ulimwengu uliopatanishwa katika uso wa vita, chuki, na vurugu. Inafaa kufuatilia baadhi ya hatua za mafundisho haya, ambazo zinaakisi jinsi utangazaji wa kiini cha imani usivyotenganishwa na ushuhuda wa upendo, kutoka katika kujitolea kwa dhati kwa maskini na kujenga jamii yenye haki zaidi. Hii inaanza na maneno yake ya kwanza, yaliyosemwa katika hotuba yake mara tu baada ya kuchagulia kwake kwenue dirisha kuu la katikati ya Basilika ya Vatican:(first words): "Amani iwe nanyi nyote! (...) Hii ni amani ya Kristo Mfufuka, amani inayoondoa silaha, amani inayoondoa silaha, ya unyenyekevu, na inayodumu. Inatoka kwa Mungu, Mungu anayetupenda sote bila masharti. (...) Lazima tutafute pamoja jinsi ya kuwa Kanisa la kimisionari, Kanisa linalojenga madaraja, mazungumzo, ambayo huwa wazi kila wakati kwa kukaribisha."

Kanisa, alisema katika mahubiri (homily) yake kwenye Misa ya kuanza kwa Upapa wake mnamo tarehe 8 Mei 2025, "tumeungana, ishara ya umoja na ushirika, ambayo inakuwa chachu ya ulimwengu uliopatanishwa. Katika wakati wetu, ambao bado tunaona ugomvi mwingi, majeraha mengi yanayosababishwa na chuki, vurugu, ubaguzi, hofu ya wale walio tofauti, na dhana ya kiuchumi inayotumia rasilimali za Dunia na kuwatenga maskini zaidi. Na tunataka kuwa, ndani ya unga huu, chachu ndogo ya umoja, ushirika, na udugu."

Katika moyo wa utume: ni kutoweka ili Kristo abaki

Siku moja baada ya kuchaguliwa kwake, katika maadhimisho yake ya kwanza na Makardinali katika Kikanisa cha Sistine, (celebration with the cardinals)Papa Leo XIV alikumbuka "ahadi muhimu kwa yeyote katika Kanisa anayetekeleza huduma ya mamlaka ya: kutoweka ili Kristo abaki, kujifanya mdogo ili aweze kujulikana na kutukuzwa, kujitoa kikamilifu ili hakuna mtu anayekosa fursa ya kumjua na kumpenda." Katika mahubiri yake mnamo Mei 18, Papa alizungumzia "upendo na umoja" kama vipimo viwili vilivyokabidhiwa na Yesu kwa Petro na akaelezea kwamba kazi hii inawezekana tu kwa sababu Petro "alifanya uzoefu katika maisha yake mwenyewe upendo usio na kikomo na usio na masharti wa Mungu, hata katika saa ya kushindwa na kukana." Kwa sababu, kama alivyowaambia vijana waliokusanyika huko Tor Vergata jioni ya Agosti 2, ( 2 August,)"asili yetu wenyewe hakukuwa na uamuzi wetu, bali upendo uliotutaka."

Upendo huu unatutangulia, kama Papa alivyoelezea katika Katekesi yake mbele ya hadhira siku ya Jumatano, Agosti 20, (General Audience of 20 August,)akizungumzia Yuda akipokea kipande cha mkate kutoka kwa Yesu kwenye Karamu kuu ya Mwisho: "Yesu hupeleka mbele  upendo wake na kwa ukamilifu (...) Kwa sababu anajua kwamba msamaha wa kweli haungoji toba, bali hujitoa kwanza, kama zawadi ya bure, hata kabla ya kupokelewa." Utume waa Kanisa ni kushuhudia upendo huu. Ili kufanya hivyo, Papa Leo alielezea mnamo tare 7 Juni 2025, (Pentecost Vigil,)wakati wa Mkesha wa Pentekoste, "hatuhitaji wafuasi wenye nguvu, maelewano ya kidunia, au mikakati ya kihisia. Uinjilishaji ni kazi ya Mungu, na ikiwa wakati mwingine hupitia watu wetu, ni kwa sababu ya vifungo vinavyowezesha." Kanisa halihitaji mikakati ya biashara; uinjilishaji, kiukweli, ni Mungu anayefanya kazi. Msingi wa utume ni umoja katika utofauti, yaani, ushirika ulio hai.

Ni imani, kama alivyosisitiza Dominika tarehe 5 Oktoba 2025, (Jubilee of the Missionary World,) akisherehekea Jubilei ya Ulimwengu wa Wamisionari, ambayo "hailazimishwi kwa nguvu na kwa njia za ajabu (...) Ni wokovu unaokuja tunapojitolea kibinafsi na kujali, kwa huruma ya Injili, kwa mateso ya jirani yetu." Ni imani ambayo haiwahukumu wengine, ambayo haitufanyi tujisikie "wakamilifu," pia kwa sababu, kama alivyoelezea katika Sala ya Malaika wa Bwana Dominika Agosti 24, ( Angelus)Yesu anadhoofisha "usalama wa waamini": "Kiukweli, anatuambia kwamba haitoshi kukiri imani yetu kwa maneno, kula na kunywa pamoja naye tukisherehekea Ekaristi, au kuwa na ujuzi mzuri wa mafundisho ya Kikristo. Imani yetu ni halisi inapokumbatia maisha yetu yote, inapogeuka kuwa kigezo cha chaguzi zetu, inapotufanya wanawake na wanaume wanaojitolea kwa mema na kuchukua hatari katika upendo, kama vile Yesu alivyofanya."

Kushuhudia Amani

Baada ya kufanya hivyo katika salamu hiyo ya kwanza siku ya kuchaguliwa kwake, Papa Leo XIV alizungumza mara nyingi kuhusu amani, akiwaalika Wakristo kuishuhudia kwa uhalisia: "Kutotumia nguvu kama njia na mtindo lazima kutofautisha maamuzi yetu, mahusiano yetu, matendo yetu," alisema hayo kunako Mei 30 ( Arena of Peace.)kwa harakati na vyama vya “Arena della Pace.” Wakati huo huo, Mrithi wa Petro amezungumza mara kwa mara dhidi ya silaha, kama alivyofanya mwishoni mwa Katekesi ya  Juni 18 ( General Audience): "Hatupaswi kuzoea vita! Hakika, lazima tukatae mvuto wa silaha zenye nguvu na za kisasa kama kishawishi."

Papa Leo XIV  kunako tarehe 26 Juni akikutana na washiriki wa Mkutano wa Matendo kwa ajili ya Makanisa Hitaji ya Mashariki ya Kati (ROACO)( ROACO,)alisema: “Mtu anawezaje kuamini, baada ya karne nyingi za historia, kwamba vita huleta amani na haviwarudishi wale waliovipiga? (…) Tunawezaje kuendelea kusaliti matamanio ya watu ya amani kwa propaganda za uwongo za silaha, katika udanganyifu mtupu kwamba ukuu hutatua matatizo badala ya kuchochea chuki na kisasi? Watu wanazidi kutojua kiasi cha pesa kinachoingia mifukoni mwa wafanyabiashara wa kifo, ambacho wangeweza kujenga hospitali na shule; na badala yake, zile ambazo tayari zimejengwa zinaharibiwa!

Upokonyaji silaha unaotakiwa na Askofu wa Roma unawahusu viongozi wa mataifa, ili wasigeuze utajiri "dhidi ya mwanadamu, wakiubadilisha kuwa silaha zinazoharibu watu na ukiritimba unaowadhalilisha wafanyakazi" (Mahubiri, Septemba 21, katika Parokia ya Mtakatifu Anna mjini Vatican), na kila mmoja wetu, kwa sababu mwaliko wa Yesu ni kupokonya mkono, lakini kwanza kabisa moyo. Kama Papa Leo alivyosema mwishoni mwa Mkesha wa Amani wa  Sala kwa Bikira Maria siku ya Jumamosi, tarehe 11 Oktoba  2025(  Marian Vigil for Peace): "Weka upanga wako pembeni" ni neno linaloelekezwa kwa wenye nguvu duniani, kwa wale wanaoongoza hatima ya watu: kuwa na ujasiri wa kupokonya silaha! Na pia linaelekezwa kwa kila mmoja wetu, ili kutufanya tuelewe zaidi kwamba hatuwezi kuua kwa ajili ya wazo lolote, au imani, au siasa. Moyo lazima upokonywe silaha kwanza, kwa sababu ikiwa hakuna amani ndani yetu, hatutatoa amani."

Upendo kwa Maskini

Katika Wosia wake wa kwanza wa Kitume, Dilexi te( Dilexi te,) yaani nimekupenda uliochapishwa mnamo tarehe 9 Oktoba Papa Leo alielezea kwamba kwa kuwasaidia wale wanaoteseka, "hatuko ndani ya upeo wa upendo, bali wa Ufunuo: kuwasiliana na wale wasio na nguvu na ukuu ni njia ya msingi ya kukutana na Bwana wa historia." Upendo kwa maskini si "njia ya hiari," bali unawakilisha "kigezo cha ibada ya kweli."

Akikutana na Mabalozi wa kitume mnamo tarehe 10 Juni 2025,(Apostolic Nuncios) Papa aliwaambia: "Ninawategemea ili kila mtu katika nchi mnazoishi ajue kwamba Kanisa liko tayari kufanya chochote kwa ajili ya upendo, kwamba daima liko upande wa walio wadogo, maskini." Na mnamo Julai 13 huko Castel Gandolfo (Castel Gandolfo,) alihimiza, akifuata mfano wa Msamaria Mwema, tusipite bali tujiruhusu "kuchomwa mioyoni" na "wale wote wanaozama katika uovu, mateso, na umaskini," na "watu wengi waliovuliwa nguo, kuibiwa, na kuporwa, waathiriwa wa mifumo ya kisiasa dhalimu, uchumi unaowalazimisha kuingia katika umaskini, vita vinavyoua ndoto zao na maisha yao."

Katika Jubilei ya Wafanyakazi wa Haki mnamo Septemba 20, Papa alihimiza wasigeuke kutoka katika "ukweli wa nchi na watu wengi wanaotamani na kiu ya haki kwa sababu hali zao za maisha ni mbaya sana na zisizo za kibinadamu kiasi kwamba hazikubaliki," akikumbuka kwamba "hali ambayo hakuna haki si hali." Akizungumza na Harakati Maarufu mnamo tarehe 23 Oktoba 2025, Mrithi wa Petro alikumbuka kwamba "kutengwa ni sura mpya ya dhuluma ya kijamii. Pengo kati ya walio  'wachache, 1% ya idadi ya watu na walio wengi limeongezeka sana. (...) Nikiwa Askofu wa Peru, ninafurahi kuwa nimepitia Kanisa linalowasindikiza watu katika huzuni zao, furaha zao, mapambano yao, na matumaini yao.”

Wahamiaji ni ndugu zetu  

Papa Leo XIV, katika mahubiri yake kwa ajili ya Jubilei ya Ulimwengu wa Wamisionari na Wahamiaji, Dominika tarehe 5 Oktoba, (Jubilee of the Missionary World and of Migrants)alizungumzia"historia ya ndugu na dada zetu wengi wahamiaji" ambao "hawawezi na hawapaswi kukutana na baridi ya kutojali au unyanyapaa wa ubaguzi!"

Na katika hotuba yake kwa Harakati za Watu wa Rom mnamo Oktoba 23, ( Popular Movements) alizungumzia suala la usalama: "Kwa unyanyasaji wa wahamiaji walio katika mazingira magumu, hatushuhudii utekelezaji halali wa uhuru wa kitaifa, bali uhalifu mkubwa unaofanywa au kuvumiliwa na Serikali. Hatua zisizo za kibinadamu zinazozidi kuongezeka, hata zinazosifiwa kisiasa, zinapitishwa ili kuwatendea hawa 'wasiohitajika' kana kwamba ni takataka na si wanadamu. Ukristo, kwa upande mwingine, unamrejea Mungu wa upendo, ambaye anatufanya sote kuwa kaka na dada na anatuomba tuishi kama kaka na dada."

Uongofu wa Kutunza Uumbaji

Papa amezungumzia mara nyingi kuhusu utunzaji wa Uumbaji, akifuata nyayo za Laudato sí ya mtangulizi wake Papa Francisko, kama alivyofanya tarehe 9 Julai, akitambulisha

"Uongodi wa utunzaji wa Uumbaji"( “Mass for Creation”: "Mwanzoni mwa Misa, tuliombea uongofu, uongofu wetu wenyewe. Ningependa kuongeza kwamba tunapaswa kuombea uongofu wa watu wengi, ndani na nje ya Kanisa, ambao bado hawatambui hitaji la dharura la kutunza nyumba yetu ya pamoja. Maafa mengi ya asili tunayoyaona yakitokea karibu kila siku katika ulimwengu wetu, katika sehemu na nchi nyingi, pia kwa sehemu ni matokeo ya kupita kiasi kwa wanadamu na mitindo yetu ya maisha. Tunahitaji kujiuliza kama sisi wenyewe tunapitia uongofu huo. Tunauhitaji kiasi gani!"

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

08 Novemba 2025, 16:59