Nia za Maombi ya Papa Desemba 2025:Wakristo katika maeneo ya migogoro

Katika Nia ya maombi ya Papa iliyotayarishwa na Mtandao wa Kimataifa kwa ajili ya mwezi Desemba 2025 anasali kwa ajili ya watu wanaoteseka katika maeneo ya vita,hasa Mashariki ya Kati ili wahisi wema mpole wa Mungu na ukaribu wa Kanisa la ulimwengu wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa anajiandaa kwenda ziara yake ya Kwanza ya Kitume kwenda Türkiye -Uturuki) na Lebanon,  alitoa maombi yaka kwa njia ya Video Jumatano  tarehe 26 Novemba 2025 ili kuambatanisha nia yake ya maombi ya Mwezi  Desemba, ambayo ni kwa ajili ya "Wakristo wanaoishi katika maeneo ya migogoro." Tuombe kwamba Wakristo wanaoishi katika maeneo ya vita au migogoro, hasa Mashariki ya Kati, waweze kuwa mbegu za amani, upatanisho, na matumaini," alisema katika video hiyo. Vile vile Baba Mtakatifu  alitoa sala kwa Mungu wa Amani kwamba Wakristo waliozungukwa na maumivu waweze kuhisi “wema mpole wa uwepo wako na maombi ya kaka na dada zao katika imani." Aliomba pia kwamba Mungu awasaidie kuimarisha vifungo vya kidugu na kuwa mbegu za upatanisho zinazojenga matumaini na madaraja ya haki na huruma. Papa aliwaalika Wakristo wote kuomba ili tusije tukawa wasiojali mateso ya Wakristo wengine, bali tuweze kuwa wajenzi wa umoja.”

‘Imani isiyotikisika hata katikati ya magofu’

Mtandao wa Maombi wa Papa  Kimataifa , ambao hutoa Video ya Papa ya kila mwezi na Vatican Media, ulitoa taarifa inayounganisha nia ya maombi na ziara yake Türkiye na Lebanon. Hata Mashariki ya Kati ikikabiliwa na ukosefu wa utulivu, jumuiya za Kikristo zinaendelea kulinda imani, kuwahudumia maskini, na kufanya kazi pamoja na watu wa Makanisa na imani zingine kujenga madaraja ya kuishi pamoja.

Kulingana na Ripoti Huru wa Kidini ya  Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji 2025,” lilibainisha taarifa hiyo, kuwa “idadi ya migogoro katika Mashariki ya Kati na hali ya kijamii na kiuchumi huko inaweka wazi watu wachache wa kitawa, na hasa Wakristo, katika hali ya udhaifu mkubwa.” Katika imani yao isiyotikisika hata katikati ya magofu, jumuiya za Kikristo zinafufuka baada ya vita vya hivi karibuni na kutoa msaada waupendo  na msaada wa kiroho kwa wengine. Kwa njia hiyo haya yote ni ishara za uwepo wa Roho Mtakatifu ambaye, kama sala inavyosomeka, ambapo Papa anasema, ndiye chanzo cha tumaini katika nyakati za giza zaidi.

Sala kamili ya Papa Leo

Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Mwanaoumeupatanisha ulimwengu na Wewe, leo hii tunawaombea Wakristowanaoishi katikati ya vita na vurugu. Hata wakiwa wamezungukwa na maumivu, wasiache kamwe kuhisi wema mpole wa uwepo wako na maombi ya ndugu na dada zao katika imani. Kwani ni kupitia Wewe tu, na kuimarishwa na vifungo vya kidugu, wanaweza kuwa mbegu za upatanisho, wajenzi wa matumaini kwa njia ndogo na kubwa, wenye uwezo wa kusamehe na kusonga mbele, wa kuziba migawanyiko, na wa kutafuta haki kwa huruma.

Bwana Yesu, aliyewaita wenyeheri wale wanaofanya kazi kwa ajili ya amani, utufanye vyombo vyako vya amani hata pale ambapo maelewano yanaonekana kuwa hayawezekani. Roho Mtakatifu, chanzo cha tumaini katika nyakati za giza, udumishe imani ya wale wanaoteseka na uimarishe tumaini lao. Usituache tuanguke katika kutojali, na utufanye wajenzi wa umoja, kama Yesu. Amina.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku:Just click here

26 Novemba 2025, 16:30