Papa akutana na Waziri Mkuu wa Latvia
Vatican News.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya Habari, Vatican imebanisha kuwa “Asubuhi ya leo, tarehe 24 Novemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alimpokea kwa Mkutano katika Jumba la Kitume la Vatican, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Latvia, Mheshimiwa Bi Evika Siliņa, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican , akifuatana na Askofu Mkuu Paul R. Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.”
Wakati wa mazungumzo ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, pande zote mbili zilielezea kuridhika na uhusiano mzuri kati ya Vatican na Jamhuri ya Latvia, pamoja na mchango chanya ambao imani ya Kikristo na Kanisa Katoliki hutoa kwa nchi. Mazungumzo hayo pia yaligusia masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa, hasa juhudi za kufikia amani na kukomesha vita nchini Ukraine.
