Papa amteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu
Vatican News
Jumatatu tarehe 24 Novemba 2025, Baba Mtakatifu amemteua Katibu Msaizidi wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamanai ya Binadamu, Monsi Jozef Barlaš, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican.
Wasifu wake
Mons. Barlaš alizaliwa tarehe 7 Mei 1985 huko Snina (Slovakia). Alipewa daraja la upadre kwa ajili ya Jimbo Kuu la Košice mnamo tarehe 19 Juni 2010. Alipata Shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran mnamo 2022.
Tangu tarehe 1 Oktoba 2020, amekuwa Afisa katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican. Aliteuliwa kuwa Padre wa Kikanisa cha Baba Mtakatifu mnamo mwaka huu 2025. Mbali na Kislovakia, anazungumza Kiitaliano, Kiingereza, na Kihispania.
