2025.11.15 Papa alikutana na Rais, Makamu na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Canada. 2025.11.15 Papa alikutana na Rais, Makamu na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Canada.  (@Vatican Media)

Papa atoa mabaki 62 ya sanaa kutoka Makumbusho ya Vatican kwa maaskofu wa Canada

Papa Leo XIV alikutana na wawakilishi wa Baraza la Maaskofu wa Canada.Zawadi hizo,kulingana na taarifa ya pamoja na Vatican,ni "ishara halisi ya mazungumzo,heshima, na udugu"na zinashuhudia"historia ya kukutana kati ya imani na tamaduni za watu wa kiasili."Maaskofu wamejitolea kulinda,kukuza,na kuhifadhi ipasavyo kazi hizo.

Vatican News

Tarehe 15 Novemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana  katika Jumba la Kitume na Askofu Pierre Goudreault, wa Jimbo la Mtakatifu Anna wa  Pocatière  na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Canada,  akisindikizana na Askofu Mkuu Richard Smith, wa Jimbo Kuu la  Vancouver, Padre  Jean Vézina, Katibu Mkuu wa Baraza La Maaskofu hilo.

Katika taarifa iliyotolewa pamoja na Vatican  na Baraza la Maaskofu Canada, inabainisha kuwa “Wakati wa  Mkutano huo Papa ametoa zawadi ya mabaki 62 ya kisanaa kutoka kwenye makusanyo ya kiutamaduni ya Makumbusho ya Vatican,  kwa Baraza la  Maaskofu wa Canada. Akihitimisha ile safari  iliyoanzishwa na Papa Francisko, kupitia Ziara  yake ya Kitume mnamo 2022 kwenda Canada, mikutano  mbalimbali na Jumuiya za watu wa Asilia na kuchapishwa kwa Azimio la 2023 kuhusu Mafundisho ya Ugunduzi,  ambapo Baba Mtakatifu Leo XIV alitaka zawadi hiyo iwakilishe ishara halisi ya mazungumzo, heshima, na udugu. Hili ni tendo la kushiriki  Kanisa, ambalo Mrithi wa Petro alikabidhi mabaki haya kwa Kanisa nchini Canada, ambayo yanashuhudia historia ya kukutana kati ya imani na tamaduni za watu wa asilia.

Papa na Ujumbe kutoka Kanisa Katoliki la Canada
Papa na Ujumbe kutoka Kanisa Katoliki la Canada   (@Vatican Media)

Mabaki sitini na mbili, yanayotoka katika jumuiya mbalimbali, ambayo  ni sehemu ya urithi uliopokelewa wakati wa Maonesho ya Kimisionari ya Vatican ya 1925, yaliyotangazwa na Papa Pio XI wakati wa Mwaka Mtakatifu, ili kutoa ushuhuda wa imani na utajiri wa kiutamaduni wa watu. yaliyotumwa Roma na wamisionari Wakatoliki kati ya 1923 na 1925, mabaki haya baadaye yalitiririka hadi Jumba la Makumbusho ya Kimisionari ya Lateran, ambalo baadaye likawa Jumba la Makumbusho la Kimisionari la "Anima Mundi" la Makumbusho ya Vatican.

Zawadi ya Baba Mtakatifu ni sehemu ya Jubilei ya 2025, ambayo inaadhimisha “Matumaini”, na “miaka mia moja ya Maonesho ya Kimisionari ya Vatican.” Mabaki haya ya sanaa, yakiambatana na taarifa zilizomo katika Makumbusho ya Vatican, ambayo yanathibitisha asili yake na hali ya kuhamishiwa kwao Roma kwa ajili ya Maonesho ya 1925, yaliwasilishwa katika Mkutano wa Maaskofu wa Canada, ambao, kwa roho ya ushirikiano mwaminifu na mazungumzo na Kurugenzi ya Urithi wa Utamaduni na Jiji la  Vatican, wameazimia kuhakikisha kwamba yanalindwa, yanatangazwa na kuhifadhiwa vya kutosha.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

15 Novemba 2025, 16:34