Basilika ya Laterano. Basilika ya Laterano.  (@Vatican Media)

Papa ataongoza Misa katika Basilika ya Laterano katika kumbukizi ya Kutabarukiwa Kanisa Kuu la Mt.Yohane

Papa Leo XIV ataongoza Misa Takatifu Dominika asubuhi, tarehe 9 Novemba 2025 saa 3:30 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Lateran,kiti cha Askofu wa Roma katifa fursa ya kutabarukiwa kwa Kanisa Kuu hilo kunako mwaka 324 na Papa Slivester ambalo limewakwa chini ya Ulinzi wa Kristo Mkombozi wa Ulimwengu pia chini ya ulinzi wa Mtakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili Yohane.

Vatican News

Kanisa Kuu la Roma pia linaitwa Basilika Kuu ya  Mwokozi Mtakatifu Sana kwa sababu mnamo tarehe 9 Novemba 324, Papa Sylvester I aliliweka chini ya  Ulinzi wa Kristo Mkombozi wa Ulimwengu baada ya ujenzi wake na ufadhili wake na Mfalme Constantine. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jimbo la Roma, inasomeka kuwa "Lateran ilikuwa Kanisa la kwanza ambalo Wakristo waliweza kuadhimisha liturujia zao kwa uhuru na hadharani."

Katika karne ya 9, Papa Sergius III aliongeza kuwekwa wakfu kwa Mtakatifu Yohane Mbatizaji, na katika karne ya 12, Papa Lucius II pia alimjumuisha Mtakatifu Yohane Mwinjili. Jina kamili, kiukweli, Basilika Kuu ya Papa ya “Mkombozi Mtakatifu sana” na ya Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili Yohane huko Lateran. Pia ina jina “Omnium Urbis et Orbis Ecclesiarum Mater et Caput,” ikimaanisha "Mama na Kichwa cha Makanisa yote ya Jiji na Ulimwengu." Kuanzia karne ya 4 hadi mwisho wa kipindi cha Avignon (karne ya 14), Lateran ilikuwa kiti cha pekee cha upapa.

Basilika ya Laterano ni Mama wa Makanisa Yote 

Maadhimish ya Misa Dominika tarehe 9 Novemba kwa hiyo  itaongozwa na kwaya ya Jimbo la  Roma na Kwaya ya Kikanisa cha Sistine. Tiketi za bure zinahitajika, zinazopatikana katika Ofisi ya Liturujia Jimbo la Roma. Na kwa njia hiyo Jimbo lenyewe la  Roma linawaalika mapadre  wanaosherehekea Jubilei, maadhimisho ya miaka kumi, hamsini, na sitini ya kuwekwa wakfu kwao , kusherehekea kwa pamoja. Ni sherehe kubwa kwa Roma kwa sababu ndilo  lilikuwa ni Kanisa la kwanza kujengwa mjini Roma na baadaye, kuanzia mwaka 1565 Makanisa yakaanza kujengwa sehemu mbali mbali. Kanisa hilo ndilo Makao makuu ya Jimbo kuu la Roma, ambalo, Baba Mtakatifu ndiye Askofu wake mkuu. Kwa namna hiyo Katika Jimbo kuu la Roma kuna Maaskofu wanaomsaidia Papa kuendedesha shughuli za kichungaji. Kardinali anayelihudumia Kanisa la aterano ndiye Vika wa Papa.

Papa ataongoza Misa tarehe 9 Novemba huko Laterano
05 Novemba 2025, 10:47