Papa Leo XIV:Wazee ni hekima ya watu,hazina kwa wajukuu,familia na jamii!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV , Ijumaa tarehe 28 Novemba 2025 ikiwa ni siku ya Pili ya Ziara yake ya Kwanza ya Kitume nchini Türkiye- (Uturuki,) baada ya kukutana na Maaskofu, Mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume na wahudumu wa kichungaji, katika Kanisa Kuu la Rogo Mtakatifu, alikwenda kutembelea Nyumba ya Wazee iliyopo nje kidogo mwa mji wa Istanbul inayohudumiwa na watawa wa Dada Wadogo wa maskini.
Akianza hotuba yake Baba Mtakatifu Le XIV aliawasalimia na kushukuru maneno ya Sista kwa kumkaribisha na kuwakaribisha wazee, kwa ukarimu wanaooneshwa na wote. "Ukarimu ni zawadi ya nyumba hii!“ Papa aliongeza, "Kiukweli ni zawadi inayotoka kwa Mungu na inatekelezwa na masista Wadogo wa Maskini, wafanyakazi, wafadhili, na pia na wakazi wote, katika maisha yenu ya kila siku pamoja. Asante kwa kila mtu!” Baba Mtakatifu alipenda kushirikishana nao tafakari mbili fupi. "
Papa alisema "Ya kwanza limeongozwa na jina la watawa wenyewe wapendwa, kwa maana wao ni "Dada Wadogo wa Maskini." Hili ni jina zuri, na linalotufanya tufikiri! Ndiyo, Bwana amewaita si tu kuwasaidia au kuwasaidia maskini, bali pia amewaita kuwa "dada" zao”. Kwa namna hiyo Papa aliongeza: “Mnapaswa kuwa kama Yesu, ambaye Baba alimtuma kwetu si tu kutusaidia na kututumikia, bali pia kuwa ndugu yetu. Siri ya upendo wa Kikristo ni kwamba kabla ya kuwa kwa ajili ya wengine, lazima kwanza tuwe na wengine katika ushirika unaotegemea udugu," Papa alishauri.
Tafakari ya pili Papa alisema imetokana wazee hao " wakazi wapendwa wa nyumba hii." Papa aliongeza "Ninyi ni wazee. Neno hili, "wazee," leo lina hatari ya kupoteza maana yake halisi. Katika miktadha mingi ya kijamii, ambapo ufanisi na ubinafsi vinatawala, hisia ya heshima kwa wazee imepotea. Kwa upande mwingine, Maandiko Matakatifu na tamaduni njema zinatufundisha kwamba, kama Papa Francisko alivyopenda kurudia kusema kwamba: “wazee ni hekima ya watu, hazina kwa wajukuu zao, familia na jamii kwa ujumla.
Kwa hivyo, shukrani mara mbili kwa nyumba hii, ambayo inawakaribisha watu kwa jina la udugu, na hufanya hivyo hasa kwa wazee. Tunajua kwamba hii si rahisi kwani inahitaji uvumilivu mwingi na maombi. Kwa hivyo sasa, hebu tumwombe Bwana awasindikize na kuwategemeza. Kwa nyote, ninawaombea baraka za Mungu.”
Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui
