Papa Leo XIV ameonesha ukaribu kwa waathirika wa kimbunga huko Ufilipino
Na Angella Rwezaula – Vatican
Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 9 Novemba 2025, Baba Mtakatifu leo VI ameonesha ukaribu na watu wa Ufilipino waliokumbwa na kimbuka kikali. Papa amesema “Niko karibu na watu wa Ufilipino walioathiriwa na kimbunga kikubwa: Ninawaombea marehemu na familia zao, waliojeruhiwa na waliokimbia makazi yao.”
Nchini Italia ikiwa ni siku ya kutoa shukrani kwa mwenyezi Mungu Papa Leo XIV alisema kuwa “ Leo Kanisa nchini Italia linaadhimisha Siku ya Shukrani. Ninajiunga na ujumbe wa Maaskofu katika kuhimiza utunzaji wa ardhi kwa uwajibikaji, mapambano dhidi ya upotevu wa chakula, na kupitishwa kwa mbinu endelevu za kilimo. Tumshukuru Mungu kwa "dada yetu mama dunia" (Mtakatifu Francisko wimbo wa sifa kwa viumbe) na kwa wote wanaolima na kuilinda!”
Salamu mbali mbali kwa moyo wote kwanza kabisa Warumi, na mahujaji kutoka pande za Italia na sehemu nyingi za dunia, kwa namna ya pekee vijana Wajesuit kutoka Poland, waamini waliotoka Warsaw na Danzica, Poland, Newark na Carney nchini Marekani, Toledo, ya Galapagar huku Hispania na London na kama ilivyo Kwaya ya Regensburger Domspatzen.
Papa aliendelea kusema kuwa “Salamu kwa Chama cha matendo ya Kitume Katoliki Jimbo Kuu la Genova, na Makundi ya Parokia ya Cava Manara, Mede, Vibomarina, Mtakatifu Malaka Mkuu huko Potenza, Noto, Pozzallo na Avola, Cesenatico, Mercato Mtakatifu Severino, Crespano ya Grappa na Noventa Padovana.” Aidha “Salamu kwa Kundi la maandamano ya kihistoria ya Lazio na watu wa kujitolea wa Meza vya vyakua ambao watakusanya vyakula Jumamos ijayo katika keshoa la Siku ya Maskini Ulimwenguni.”
Papa Leo XIV kadhalika alitoa shukrani zangu za dhati kwa wale katika kila ngazi wanaofanya kazi ya kujenga amani katika maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na vita. Katika siku za hivi karibuni tumewaombea marehemu, na kwa kusikitisha, miongoni mwao wengi wameuawa katika mapigano na mabomu, ingawa walikuwa raia, watoto, wazee, na wagonjwa. Ikiwa kweli tunataka kuheshimu kumbukumbu zao, hebu tusitishe mapigano na tujitoe kwenye mazungumzo.
Nawatakia kila mmmoja Dominika njema!
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui
