Papa Leo XIV awatembelea Watawa Wakarmeli huko Harissa,Lebanon
Vatican News
Mara baada ya kukutana na mamlaka, mamlaka ya kiraia, wawakilishi wa asasi za kiraia, na kikundi cha kidiplomasia cha Jamhuri ya Lebanon, Dominika jioni, tarehe 30 Novemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alisafiri hadi kwenye Monasteri ya Masista Wakarmeli wa Theotokos yaani wa Mama wa Mungu, huko Harissa. Kulingana na taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican ilibanisha kuwa, "Papa aliwasalimia kila sista mmoja mmoja kabla ya kupokea salamu kutoka kwa wakuu wa jumuiya hizo mbili.
Akiwahutubia watawa hao "Papa Leo XIV aliwakumbusha maneno matatu katika kiini cha wito wao wa kutafakari ambayo ni: unyenyekevu, sala na sadaka."
kwa mujibu wa taarifa ni kwamba "Mkutano huo ulidumu kwa takriban nusu saa na kuhitimishwa kwa kusali sala ya Baba Yetu, na Papa Leo XIV aliwapatia Baraka yake ya Kitume watawa Wakarmeli wa ndani.
![]()
Hatimaye picha ya pamoja na Papa na watawa wakarmeli (@Vatican Media).
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
