2025.11.13 Washiriki katika mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Utafiti na Utafiti kuhusu Utoto na Ujana 2025.11.13 Washiriki katika mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Utafiti na Utafiti kuhusu Utoto na Ujana  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Inahitajika mbinu ya kielimu,kimaadili inayowajibika katika AI

Ni kwa kuchukua mbinu ya kielimu,kimaadili nauwajibikaji pekee ndipo tunaweza kuhakikisha kwamba akili una inatumika kama mshirika,na si tishio, katika ukuaji na maendeleo ya watoto na vijana.Alisema hayo Papa Leo XIV Novemba 13,akikutana na washiriki wa mkutano kuhusu "Hadhi ya Watoto na Vijana katika Enzi ya Akili Unde,mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 13 Novemba 2025 2025 mjini Vatican alikutana na  washiriki wa Mkutano kuhusu: “Hadhi ya Watoto na vijana katika enzi ya  Akili Unde, (The dignity of children and adolescents in the age of Artificial Intelligence), ulioandaliwa na Mfuko wa Utafiti na Utafiti kuhusu Utoto na Ujana. Papa  aliwashukuru kwa uwepo wao na kwa michango yao muhimu. “Akili Unde (AI) inabadilisha vipengele vingi vya maisha yetu ya kila siku, ikiwa ni pamoja na elimu, burudani na usalama wa watoto wadogo. Matumizi yake yanaibua maswali muhimu ya kimaadili, hasa kuhusu ulinzi wa heshima na ustawi wa watoto wadogo.”

Watoto na vijana wako katika hatari kubwa ya kudanganywa kupitia mifumo ya kimashine(algoriti) za Akili Unde( AI )ambazo zinaweza kushawishi maamuzi na mapendeleo yao. Ni muhimu wazazi na waelimishaji wafahamu mienendo hii, na kwamba zana zitengenezwe ili kufuatilia na kuongoza mwingiliano wa vijana na teknolojia.” Papa aidha alitoa wito kwamba “Serikali na mashirika ya kimataifa yana jukumu la kubuni na kutekeleza sera zinazolinda heshima ya watoto wadogo katika enzi hii ya AI.)

Washiriki wa Mkutano kuhusu Utoto na Ujana
Washiriki wa Mkutano kuhusu Utoto na Ujana   (@VATICAN MEDIA)

Hii inajumuisha kusasisha sheria zilizopo za ulinzi wa data ili kushughulikia changamoto mpya zinazotokana na teknolojia zinazoibuka, na kukuza viwango vya maadili kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya AI. Papa alisisitiza kwamba “hata hivyo kulinda heshima ya watoto wadogo hakuwezi kupunguzwa kwa sera pekee; pia inahitaji elimu ya kidijitali. Kama mtangulizi wake alivyowahi kusema kuhusu mpango wa ulinzi ulioendelezwa na vyama vitatu vikubwa vya Wakatoliki nchini Italia, watu wazima, lazima wagundue upya wito wao kama "wasanii wa elimu" na kujitahidi kuwa waaminifu wake.” “Kiukweli ni muhimu kuandika na kutekeleza miongozo ya maadili, lakini hiyo haitoshi. Kinachohitajika ni juhudi za kila siku za kielimu zinazoendelea, zinazofanywa na watu wazima ambao wenyewe wamefunzwa na kuungwa mkono na mitandao ya ushirikiano.”

Mchakato huu unahusisha kuelewa hatari ambazo matumizi ya AI na ufikiaji wa kidijitali wa mapema, usio na kikomo na usiosimamiwa unaweza kusababisha kwa mahusiano na maendeleo ya vijana. Ushauri wa Papa Leo XIV anabainisha kwamba,  “Ni kwa kushiriki tu katika ugunduzi wa hatari hizo na athari kwenye maisha yao binafsi na kijamii, ndipo watoto wanaweza kusaidiwa katika kuukaribia ulimwengu wa kidijitali kama njia ya kuimarisha uwezo wao wa kufanya maamuzi yenye uwajibikaji kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya wengine.

Mkutano kuhusu Utoto na Ujana
Mkutano kuhusu Utoto na Ujana   (@VATICAN MEDIA)

Hili lenyewe ni zoezi muhimu katika kulinda uhalisi na muunganiko wa binadamu, ambalo lazima liongozwe kila wakati na heshima kwa utu wa binadamu kama thamani ya msingi. Ni kwa kuchukua mbinu ya kielimu, kimaadili na uwajibikaji pekee ndipo tunaweza kuhakikisha kwamba akili ude inatumika kama mshirika, na si tishio, katika ukuaji na maendeleo ya watoto na vijana. Baba Mtakatifu aliwatakia mkutano wenye matunda, utakaosaidia kuweka msingi imara wa huduma yetu inayoendelea kwa watoto, vijana, na kwa jumuiya nzima ya kikanisa na ya kiraia. Kwa ajili yao katika kazi yao, aliomba baraka za Bwana na ahatimaye akawashukuru.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

 

13 Novemba 2025, 16:37