Papa Leo XIV,(Doxolojia):sala ya Yesu,wanafunzi wote wawe kitu kimoja

Katika sala kwenye Kanisa la Mtakatifu George huko Istanbul,Makao Makuu ya Upatriaki wa Kiekumeni,Papa alisali pamoja na Patriaki Bartholomew I na kukumbusha siku ya kihistoria:“Tunatiwa moyo katika kujitolea kwetu kutafuta urejesho wa ushirika kamili miongoni mwa Wakristo wote kwa kazi tunayofanya kwa msaada wa Mungu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ya tarehe 28 Novemba ilikuwa ni siku muhimu ambayo “Tumepitia nyakati za ajabu za neema tukikumbuka,pamoja na kaka na dada zetu katika imani, maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza la Kiekumeni wa Nicea. Ni Maneno  ya Baba Mtakatifu Leo XIV aliyorudiwa tena tarehe 29 Novemba 2025, katika Kanisa la Mtakatifu George, kiti cha Uongozi wa Kiekumeni wa Constantinopoli, katika wilaya ya Phanar huko Istanbul, ambapo alishiriki katika masifu ya sala. Ni katika  Siku ya kuamkia ukumbusho wa kiliturujia wa Mtakatifu Andrea, Msimamizi wa Upatriaki wa  Kiekumeni, siku ambayo, kila mwaka, ujumbe kutoka Kiti Kitakatifu unakuwepo  kwa ajili ya Türkiye (Uturuki), kama sehemu ya ubadilishanaji wa kiutamaduni kwa  ujumbe kwa ajili ya siku kuu husika za watakatifu walinzi  kunako Juni 29, jijini Roma katika sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo na Novemba 30 huko Istanbul kwa ajili ya sherehe ya Mtakatifu Andrea Mtume.

Wakati wa sala
Wakati wa sala   (@Vatican Media)

Katika tafakari yake, Papa  Leo aliomba kuruhusiwa kwanza kutoa shukrani zake za dhati kwa makaribisho yao ya joto na maneno ya Patriaki mazuri ya salamu. Vile vile aliwashukuru washiriki wa Sinodi Takatifu, pamoja na mapadre na waamini, ambao tunashiriki nao sala hii ya jioni. Nilipoingia katika Kanisa hili, nilipata hisia kubwa, kwani ninakumbuka kwamba ninafuata nyayo za Papa Paulo VI, Papa Yohane Paulo II, Papa Benedikto XVI na Papa Francisko.” Na anajua kwamba Patriaki huyo alivyo pata fursa ya kukutana na watangulizi wake wa heshima kibinafsi, na kukuza urafiki wa dhati na wa kidugu nao kulingana na imani ya pamoja na maono ya pamoja ya changamoto nyingi kuu zinazoikabili Kanisa na ulimwengu."

Papa alisema “Nina uhakika kwamba kukutana kwetu pia kutasaidia kuimarisha uhusiano wa urafiki wetu, ambao tayari ulianza kuimarika tulipokutana kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa huduma yangu kama Askofu wa Roma, hasa wakati wa sherehe kuu ya Ekaristi Takatifu, ambapo  Patriaki aliudhuria. Akikumbusha tukio la hafla ya kumbukizi ya Mtaguso iliyofanyika  Novemba 28 huko Nicea, alisema “Jana, na tena asubuhi ya leo, tulipata nyakati za ajabu za neema tulipokuwa tukiadhimisha, pamoja na kaka na dada zetu katika imani, maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza la Kiekumeni wa Nicea.

Wakati wa sala katima Upatriaki
Wakati wa sala katima Upatriaki   (@Vatican Media)

Kwa kukumbuka tukio hilo muhimu sana, na kuongozwa na sala ya Yesu kwamba wanafunzi wake wote wawe kitu kimoja (taz. Yh 17:21), tunatiwa moyo katika kujitolea kwetu kutafuta urejesho wa ushirika kamili miongoni mwa Wakristo wote, kazi tunayofanya kwa msaada wa Mungu. Tukisukumwa na hamu hii ya umoja, pia tunajiandaa kusherehekea kumbukumbu ya Mtume Andrea, mtakatifu Msimamizi wa Upatriaki wa  Kiekumeni. Katika sala ya jioni hii, shemasi alielekeza kwa Mungu ombi "kwa ajili ya utulivu wa Makanisa Matakatifu na kwa ajili ya umoja wa wote."

Ombi hili hili pia Papa Leo XIV alisema “litarudiwa katika Liturujia Takatifu ya kesho(tarehe 30 Novemba 2025). Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, atuhurumie na kweli atimize ombi hilo.” Papa alishukuru tena kwa makaribisho ya  kidugu, na alipendaa kutoa matashi mema ya dhati kwa Patriaki huyo na kwa wote waliokuwapo wakati wa kusheherekea siku kuu ya Mtakatifu Msimamizi wao  Mtakatifi Andrea.

Papa alitoa tafakari
Papa alitoa tafakari   (@Vatican Media)

Salamu za Patriaki Bartholomew I

Patriaki Bartholomew, vile vile alizungumza kwa lugha ya kiingereza wakati wa sala hiyo.  Patriaki wa Kiekumeni, wakati wa kuanza alimwita “mpendwa katika Kristo” kuwa Kanisa Kuu la Kristo, linamkaribisha kwa furaha kubwa na shangwe siku hiyo, katika roho ile ile ya upendo wa kidugu ambao watangulizi wake mashuhuri, Mapapa wa kumbukumbu nzuri Paulo VI, Yohane  Paulo II, Benedikto XVI, na Francisko, walikaribishwa." Patriaki alikumbusha kwamba mapapa wanne "wamechangia sana, kila mmoja kwa njia yake mwenyewe, kwa karama yake mwenyewe, kwa muunganiko wa Makanisa yetu dada kupitia mazungumzo ya upendo na ukweli."

Wakati wa sala katika Kanisa la Mtakatifu George
Wakati wa sala katika Kanisa la Mtakatifu George   (@Vatican Media)

Patriaki alikumbuka ahadi ambayo yeye na Francisko walitoa "kufanya hija ya pamoja katika jiji la kihistoria la Nicea wakati wa maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza la Kiekumeni, Mtaguso wa umoja katika imani ya kitume, sauti moja ya Kanisa lililoungana." Aliita Ziara  ya kwanza ya Papa Leo XIV, utimilifu wa ahadi hii, "baraka kwa upapa wake." Sawa na Padre ambaye, katika utamaduni wa liturujia ya Kikristo ya Kiorthodox, kabla ya kushiriki katika Ekaristi Takatifu, "ilisomwa sala inayojulikana kama Kairos na kuheshimu picha ya Kristo  na kuheshimu watakatifu kama njia ya kupokea baraka zao za kutumikia Liturujia," Patriaki Bartholomew aliweza kusema kuwa Papa "alifika kuteka Kairos, nguvu, na ushujaa kutoka mahali patakatifu pa Nicea anapoanza huduma yake ya upapa, inayooneshwa na hamu ya kutumikia wito wa Bwana kwa umoja wa Kikristo. Ni jukumu letu sote kujitahidi kuwa na moyoni 'umoja wa roho kupitia kifungo cha amani,'" alihitimisha Patriaki wa Kiekumeni.

Hitimisho la sala

Baada ya salamu ya Papa Leo XIV, waliali sala ya Baba Yetu kwa Kilatini, kwa kuhitimisha kwa baraka kutoka kwa Papa  Leo XIV, pia kwa Kilatini, na kutoka kwa Patriaki Bartholomew kwa Kigiriki. Nyimbo na sala zaidi zilifuata, wakati Papa na Patriaki wakitoka nje ya Kanisa nyimbo za, sifa ya Mungu zilimalizika kwa kumsifu Roho Mtakatifu,chanzo cha hekima, hofu, na uelewa.

Papa Leo wakitoka ndani ya Kanisa
Papa Leo wakitoka ndani ya Kanisa   (@Vatican Media)
29 Novemba 2025, 15:43