Papa Leo XIV kuelekea njia ya umoja huko Yerusalemu katika Jubilei ya 2033

Katika mkutano wake wa faragha na viongozi na wawakilishi wa Makanisa na jumuiya za Kikristo,Papa Leo XIV alirudi kwenye ukumbusho wa Nicea,akaelezea matumaini yake ya mikutano zaidi na alikumbusha kwamba mgawanyiko miongoni mwa Wakristo ni kikwazo cha ushuhuda wao.

Vatican News

Sala ya bidii na ya kudumu ili kuendelea kutembea pamoja katika njia ya umoja. Ndiyo ilikuwa uhakikisho wa Papa Leo XIV mwishoni mwa mkutano wa asubuhi, Novemba 29, pamoja na viongozi na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo na jumuiya katika Kanisa la Kiorthodox la Syria YA Mor Ephrem huko Istanbul. Haya yalilipotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican. Mkutano huo ulifanyika baada ya ziara ya Msikiti wa Bluu, wakati Papa Leo XIV aliposafirishwa kwa gari hadi Kanisa la Mor Ephrem, lililoko Yeşilköy, katika sehemu ya Ulaya ya jiji la Turkiye -Uturuki.

Meza ya mduara kwa viongozi wa kidini na Papa Leo XIV

Meza ya mduara kwa viongozi wa kidini na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kanisa hilo la  Mor Ephre, lilizinduliwa mwaka 2023, baada ya ujenzi uliodumu kwa takriban muongo mmoja na kuahirishwa mara kadhaa kutokana na janga la Uviko na tetemeko la ardhi. Ni Kanisa la kwanza na, hadi sasa, pekee lililojengwa Uturuki (Türkiye) tangu kuanzishwa kwa Jamhuri hiyo. Hapo, Baba Mtakatifu Leo XIv  alikutana na wawakilishi wengi wa jumuiya za Kikristo, wote wakiwa wameketi kuzunguka meza ya mduara. Papa alikaribishwa na Patriaki wa Constantinople, Bartholomew I ambaye atakutana naye tena katika Phanar, katika kiti cha Upatriaki, alasiri, na ambaye kwa pamoja watasaini Tamko la Pamoja.

Papa Leone e Bartolomeo I, patriarca di Costantinopoli

Papa Leo XIV na Bartholomew I, Patriaki wa Costantinopoli(@Vatican Media)

Mikutano Mipya na Tangazo la Kerygma

Baadhi ya waliohudhuria pia walikuwa Iznik Novemba 28 katika sherehe ya kuadhimisha miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea. Papa Leo XIV, wakati wa mkutano katika Kanisa la Mor Ephrem, alirejea tukio maalum la sherehe ya kumbukizi ya Novemba 28 huko Iznik, "ambayo kitovu chake kilikuwa Injili ya Umwilisho." Kisha akaelezea matumaini kwamba "mikutano mipya na nyakati kama zile tulizopitia zitatokea, hata kwa Makanisa yale ambayo hayakuweza kuwepo." Kisha "alikumbusha umuhimu wa uinjilishaji na tangazo la kerygma na akakumbuka jinsi ambavyo mgawanyiko miongoni mwa Wakristo ulivyo kikwazo kwa ushuhuda wao."

Safari ya kiroho kwenda Yerusalemu mwaka 2033

Hatimaye, aliwaalika kila mtu kusafiri pamoja katika safari ya kiroho inayoelekea Jubilei ya Ukombozi mnamo mwaka 2033, kwa lengo la kurudi Yerusalemu, kwenye Chumba cha Juu, yaani mahali pa Karamu ya Mwisho ya Yesu na wanafunzi wake, ambapo aliwaosha miguu, na mahali pa Pentekoste, safari inayoongoza kwenye umoja kamili, akitaja kauli mbiu yake ya kiaskofu: "Katika Illo Uno Unum."

Il Papa al termine dell'incontro con i capi delle Chiese cristiane

Mwisho wa Mkutano wa Papa na viongozi wa Makanisa ya kikristo(@Vatican Media)

Kupyaisha Imani Yetu

Katika Kanisa la Mor Ephrem, Papa Leo aliacha ujumbe kwa lugha ya Kiingereza katika Kitabu cha Heshima: “Katika tukio hili la kihistoria, tunaposherehekea maadhimisho ya miaka 1,700 ya Mtaguso wa Kwanza wa Kiekumeni wa Nicea, tunakusanyika ili kupyaisha imani yetu katika Yesu Kristo, Mungu wa kweli na mwanadamu wa kweli, tukisherehekea imani tunayoshirikisha pamoja,” aliandika Papa Leo. “Nawatakia kila baraka wale wote waliokusanyika hapa na jumuiya zote wanazowakilisha.” Tendo la mwisho la siku litafanyika baada ya Sala (Doxology, )wakati wa ibada katika Kanisa la Upatriaki la Mtakatifu George, na kabla ya Misa, ambayo inatarajiwa takriban watu 4,000 kuudhuria.

La firma del Libro d'onore

Papa anatia saini katika kitabu cha heshima (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui

29 Novemba 2025, 14:48