2025.11.20 Assisi-Mkutano wa Papa na Maaskofu wa Italia(CEI katika Basilika ya Mtakatifu Maria wa Malaika. 2025.11.20 Assisi-Mkutano wa Papa na Maaskofu wa Italia(CEI katika Basilika ya Mtakatifu Maria wa Malaika.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Kuendelea kutazama Uso wa Yesu kunatufanya tuweze kutazama nyuso za ndugu zetu

Maarifa,mapendekezo na maono ya Kanisa lililo hai linaloishi miongoni mwa watu ili kukuza utamaduni wa kukutana,kwa mtindo safi wa sinodi licha ya kuwa huu ni wakati uliowekwa alama na migawanyiko na ambayo,lazima tuwe wasanii wa urafiki na udugu,"yamo katika hotuba ya Papa Leo XIV iliyohitimisha Mkutano Mkuu wa 81 wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia(CEI,)huko Assisi,tarehe 20 Novemba 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katika ziara yake katika mji wa Amani, Alhamisi tarehe 20 Novemba 2025,  aliwasili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika (Santa Maria degli Angeli) yapata saa 3:30 asubuhi masaa ya Ulaya, baada ya kutoa heshima huko Juu ya Kilima katika kaburi la Mtakatifu Francis wa Assisi lililoko chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis. Aliingia ndani ya Basilika hiyo, huku Makofi yakisikika ya Maaskofu Katoliki wa Italia wakiwa katika Hitimisho la Mkutano wao Mkuu wa 81 ambao ulianza tangu tarehe 17 Novemba kwenye Mkoa huo wa Umbria. Baada ya kupita mlango wa Kanisa hilo Papa alielekea katika  Porziuncola, hiki ni kikanisa kidogo kilichomo ndani ya Basilika hiyo, ambacho ni Kanisa la Mtakatifu Francis, Papa alikuwa amebeba shada la waridi za njano na nyeupe.  Ishara hiyo ilielezwa na Wafransikani kwamba  Mapapa wote wamefanya maonesho kwa kukumbuka kilichomtokea Mtakatifu Francis wa Assisi. Mtawa huyo alijitupa kwenye kichaka cha waridi yenye miiba, lakini miiba ilianguka na haikumjeruhi hata kidogo. Ili kushukuru tukio hilo, Mtakatifu Francis, alipeleka waridi zisizo na miiba kwa Mama Yetu Maria wa Malaika.

L'omaggio del Papa alla Porziuncola

Papa akiweka Shada la mawaridi katika Altare ya Kikanisa kidogo kiitwacho Porziuncola  (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Leo XIV mwanzoni mwa hotuba yake alianza kusema kuwa "Wapendwa ndugu katika uaskofu, habari za asubuhi!" Ninamshukuru sana Kardinali akiwa na maana ya Matteo Zuppi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI) kwa maneno yake ya salamu na mwaliko wa “kuwa nanyi leo kuhitimisha Mkutano Mkuu wa 81. Na nimefurahishwa na hili, kituo changu cha kwanza, ingawa ni kifupi sana, huko Assisi, mahali pa muhimu sana kwa ujumbe wa imani, udugu, na amani unaowasilisha, ambao ulimwengu unahitaji haraka. Hapa, Mtakatifu Francis alipokea kutoka kwa Bwana ufunuo kwamba lazima "aishi kulingana na mfano wa Injili takatifu" (Chanzo  2 14: FF 116). Kiukweli, Kristo, "ambaye alikuwa tajiri kuliko yote, alichagua umaskini katika ulimwengu huu, pamoja na Bikira Mwenyeheri Mama yake" (2Lf 5: FF 182).

Papa akitoka kuweka mawaridi
Papa akitoka kuweka mawaridi   (@Vatican Media)

Yesu ni kitovu cha yote 

Kumtazama Yesu ndio jambo la kwanza ambalo sisi pia tunaitwa. Sababu ya kuwa hapa, kiukweli, ni imani kwake, aliyesulubiwa na kufufuka. Kama nilivyowambia mwezi Juni: katika wakati huu, zaidi ya hapo awali, tunahitaji "kumweka Yesu Kristo katikati na, katika njia iliyoelekezwa na Waraka wa Evangelii gaudium, kuwasaidia watu kupata uzoefu wa uhusiano wa kibinafsi naye, ili kugundua furaha ya Injili. Katika wakati wa mgawanyiko mkubwa, ni muhimu kurudi kwenye misingi ya imani yetu, kwenye kerygma”(Discorso ai Vescovi della Conferenza Episcopale Italiana, 17 Juni  2025).

Papa akitoka katika kikanisa kidogo ili kuanza hotuba yake
Papa akitoka katika kikanisa kidogo ili kuanza hotuba yake   (@Vatican Media)

Na hii inatuhusu sisi kwanza kabisa: kuanzia tendo la imani linaloturuhusu kumtambua Kristo kama Mwokozi na linalooneshwa katika nyanja zote za maisha ya kila siku. Kukazia macho yetu kwenye Uso wa Yesu kunatuwezesha kutazama nyuso za kaka na dada zetu. Ni upendo wake unaotusukuma kuelekea kwao (taz. 2 Kor 5:14). Na imani kwake, amani yetu (taz. Efe 2:14), inatuomba tuwape kila mtu zawadi ya amani yake. Tunaishi katika wakati uliojaa migawanyiko, kitaifa na kimataifa: ujumbe na lugha ambayo mara nyingi huchanganywa na uadui na vurugu huenea; mbio za ufanisi huwaacha walio hatarini zaidi; uweza wa kiteknolojia hukandamiza uhuru; upweke huondoa matumaini, huku kutokuwa na uhakika kwingi kuna uzito kama mambo yasiyojulikana kuhusu mustakabali wetu. Hata hivyo, Neno na Roho bado vinatuhimiza kuwa mafundi wa urafiki, udugu, na uhusiano wa kweli katika jamii zetu, ambapo, bila kusita au hofu, lazima tusikilize na kuoanisha mivutano, tukiendeleza utamaduni wa kukutana na hivyo kuwa unabii wa amani kwa ulimwengu. Mfufuka anapowatokea wanafunzi, maneno yake ya kwanza ni: "Amani iwe nanyi" (Yh 20:19, 21). Na mara moja anawatuma, kama Baba alivyomtuma (Yh 20, 21): zawadi ya Pasaka ni kwa ajili yao, lakini ili iwe kwa kila mtu!

Papa akihutubia Baraza la Maaskofu Italia
Papa akihutubia Baraza la Maaskofu Italia   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kusema kuwa “Katika mkutano wetu uliopita nilielezea miongozo kadhaa ya kuwa Kanisa linalowakilisha Injili na ni ishara ya Ufalme wa Mungu: kutangaza Ujumbe wa wokovu, ujenzi wa amani, kukuza utu wa binadamu, utamaduni wa mazungumzo, maono ya Kikristo ya anthropolojia. Leo ningependa kusisitiza kwamba madai haya yanahusiana na mitazamo iliyoibuka katika Safari ya Sinodi ya Kanisa nchini Italia. Sasa ni juu yenu, Maaskofu, kuelezea miongozo ya kichungaji kwa miaka ijayo, kwa hivyo ningependa kuwapa tafakari ili roho ya sinodi ya kweli ikue na kukomaa katika Makanisa na miongoni mwa Makanisa ya nchi yetu.

Kardinali Zuppi akitoa hotuba yake
Kardinali Zuppi akitoa hotuba yake   (@VATICAN MEDIA)

Sinodi maana yake ni wakristo wanaotembea pamoja na Kristo

Kwanza kabisa, tusisahau kwamba sinodi maana yake ni "Wakristo wanaotembea pamoja na Kristo na kuelekea Ufalme wa Mungu, katika muungano na wanadamu wote." (Documento finale della Seconda Sessione della XVI Assemblea Generale Ordinaria del Sinodo dei Vescovi, 28). Kutoka kwa Bwana tunapokea neema ya ushirika inayohuisha na kuunda uhusiano wetu wa kibinadamu na wa kikanisa. Ni matumaini kila mtu atajitolea kushughulikia changamoto ya ushirika wenye ufanisi, ili uso wa Kanisa la Baraza Kuu uweze kuchukua sura, kushiriki hatua na chaguzi za pamoja. Kwa maana hii, changamoto za uinjilishaji na mabadiliko ya miongo ya hivi karibuni, ambayo yanaathiri nyanja za idadi ya watu, kiutamaduni, na kikanisa, yanatutaka tusirudi nyuma kutoka katika suala la muunganiko wa kijimbo, hasa pale ambapo mahitaji ya ujumbe wa Kikristo yanatualika kuvuka mipaka fulani ya eneo na kufanya utambulisho wetu wa kidini na kikanisa kuwa wazi zaidi, kujifunza kufanya kazi pamoja na kufikiria upya shughuli za kichungaji kwa kuunganisha nguvu.

Papa mbele ya Maskofu
Papa mbele ya Maskofu   (@Vatican Media)

Wakati huo huo, kwa kuzingatia sura halisi ya  Kanisa nchini Italia, iliyo katika maeneo mbalimbali, na kwa kuzingatia ugumu na wakati mwingine mkanganyiko ambao chaguzi hizo zinaweza kusababisha, ni matumaini kwamba Maaskofu wa kila Jimbo watafanya utambuzi makini na, labda, waweze kupendekeza mapendekezo halisi kwa baadhi ya Jimbo ndogo zenye rasilimali watu wachache, ili kutathmini kama na jinsi wanavyoweza kuendelea kutoa huduma yao. Kinachojalisha ni kwamba, katika mtindo huu wa sinodi, tunajifunza kufanya kazi pamoja na kwamba katika Makanisa mahususi sote tunajitolea kujenga jumuiya za Kikristo zilizo wazi, zenye ukarimu, na zenye kukaribisha, ambapo mahusiano hutafsiriwa kuwa uwajibikaji wa pamoja kwa ajili ya kutangaza Injili.

Il saluto del Papa al cardinale Zuppi, presidente della Cei

 Papa akimsalimia Kardinali Zuppi, Rais wa CEI (@Vatican Media)

Kanisa linalotembea pamoja linahitaji kujirekebisha kila mara  

Sinodi, ambayo ina maana ya utekelezaji mzuri wa ushirika, haihitaji  ushirika kati yenu na mimi, tu, bali pia kusikiliza kwa makini na utambuzi wa kina wa maombi yanayotoka kwa watu wa Mungu. Kwa maana hiyo, uratibu kati ya Baraza la Maaskofu na Balozi wa Kitume, kwa madhumuni ya uwajibikaji wa pamoja, lazima uweze kukuza ushiriki mkubwa katika mashauriano ya uteuzi wa Maaskofu wapya, pamoja na kuwasikiliza Maaskofu walio katika hutuma kwenye Makanisa mahalia na wale wanaojiandaa kuhitimisha muda wao. Katika suala hili la mwisho pia, niruhusu niwapatie mwongozo. Kanisa la kisinodi, linalotembea katika historia huku likishughulikia changamoto zinazojitokeza za uinjilishaji, linahitaji kujirekebisha kila mara. Lazima tuhakikishe kwamba, hata kwa nia njema, hali ya kutojali haipunguzi kasi ya mabadiliko yanayohitajika.

Maaskofu wa CEI
Maaskofu wa CEI   (@VATICAN MEDIA)

Kuheshimu miaka 75 ya kustaafu kwa Maaskofu

Katika suala hilo, sote lazima tukuze mtazamo wa ndani ambao Papa Francisko aliuita "kujifunza kusema kwaheri," yaani mtazamo muhimu tunapojiandaa kuondoka ofisini. Ni muhimu kuheshimu kanuni ya miaka 75 ya kuhitimisha huduma ya Kichungaji katika majimbo, na ni katika hali ya Makardinali pekee ndipo mwendelezo wa huduma yao unaweza kuzingatiwa, labda kwa miaka mingine miwili. Papa alifafanua kuwa: tukirudi kwenye upeo wa utume wa Kanisa nchini Italia, ninawasihi mkumbuke njia iliyopitishwa tangu Mtaguso wa Pili wa Vatican, ulioakisiwa na mikutano ya kitaifa ya Kanisa. Na ninawasihi mhakikishe kwamba jumuiya zenu, za kijimbo na parokia, hazipotezi kumbukumbu hii, bali iendelee kuwa hai, kwa sababu hii ni muhimu katika Kanisa: kukumbuka safari ambayo Bwana anatuongoza kupitia wakati wa jangwani (taz Kum 8). Kwa mtazamo huo, Kanisa nchini Italia linaweza na lazima liendelee kukuza ubinadamu kamili unaosaidia na kuunga mkono safari za kuwepo kwa watu binafsi na jamii; hisia ya ubinadamu inayoinua thamani ya maisha na utunzaji wa kila kiumbe, na ambayo huingilia kinabii katika mijadala ya umma ili kueneza utamaduni wa uhalali na mshikamano.

I vescovi in ascolto delle parole del Papa

Maaskofu wa Italia wakisiliza maneno ya Papa Leo XIV  (@VATICAN MEDIA)

Changamoto za kidijitali

Katika muktadha huu, tusisahau changamoto inayoletwa na ulimwengu wa kidijitali. Huduma ya kichungaji haiwezi kuzuiliwa tu kwa "kutumia" vyombo vya habari, lakini lazima iwafundishe watu kuishi katika vyombo vya habari vya kidijitali kwa njia ya kibinadamu, bila kuruhusu ukweli kupotea nyuma ya kuenea kwa miunganisho, ili intaneti iweze kuwa nafasi ya uhuru, uwajibikaji, na udugu. Kutembea pamoja, kutembea na kila mtu, pia kunamaanisha kuwa Kanisa linaloishi miongoni mwa watu, linakaribisha maswali yao, linatuliza mateso yao, na kushiriki matumaini yao.

Kusikiliza maneno ya Papa
Kusikiliza maneno ya Papa   (@VATICAN MEDIA)

Kuwa karibu na familia vijana,wazee na wapweke

Endeleeni kuwa karibu na familia, vijana, wazee, na wale wanaoishi peke yao. Endelea kujitolea kuwatunza maskini: Jumuiya za Kikristo zilizojikita sana katika eneo hilo, wafanyakazi wengi wa kichungaji na watu wa kujitolea na mashirika ya Caritas  jimbo na parokia tayari yanafanya kazi nzuri katika suala hili, na ninawashukuru.!

Kujali wadogo na walio katika mazingira magumu

Katika njia hizi za utunzaji, ningependa pia kupendekeza umakini kwa wadogo na walio katika mazingira magumu zaidi, ili utamaduni wa kuzuia aina zote za unyanyasaji uweze pia kuendelezwa. Kuwakaribisha na kuwasikiliza waathiriwa ni sifa halisi za Kanisa ambalo, katika ubadilishaji wa pamoja, hutambua majeraha na kujitahidi kuwaponya, kwa sababu "mahali palipo na maumivu makubwa, tumaini linalotokana na ushirika lazima liwe na nguvu zaidi."(Veglia del Giubileo della Consolazione, 15 Septemba 2025).  Ninawashukuru kwa yale mliyoyafanya tayari, na ninawatia moyo kuendelea na kujitolea kwenu kuwalinda watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu.

Papa Leone offre la sua riflessione che chiude la 81.a Assemblea generale della Cei

Papa katika tafakari yake ya kina wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 81 wa Maaskofu Italia(@Vatican Media)

Kuchagua kuishi Mtindo wa Kisinodi

Ndugu wapendwa, katika mahali hapa, Mtakatifu Francis na watawa wa kwanza waliishi kikamilifu kile, ambacho kwa lugha ya leo, tunachokiita "mtindo wa kisinodi."Kiukweli, kwa pamoja, walishiriki hatua mbalimbali za safari yao; pamoja walimtembelea Papa Innocent III; pamoja, mwaka baada ya mwaka, waliboresha na kuimarisha maandishi ya awali yaliyowasilishwa kwa Papa, yaliyotungwa, kama Thomas wa Celano asemavyo, "zaidi ya maneno yote kutoka katika Injili" (1Cel 32: FF 372), hadi ikawa kile tunachokijua leo hii kama Kanuni ya kwanza. Chaguo hili la udugu, ambalo ni moyo wa karama ya Wafransiskani pamoja na wachache, liliongozwa na imani thabiti na inayodumu. Kwa mfano wa Mtakatifu Francis pia utupatie nguvu ya kufanya maamuzi yaliyoongozwa na imani halisi na kuwa, kama Kanisa, ishara na shuhuda wa Ufalme wa Mungu duniani. Asante!

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

20 Novemba 2025, 12:51