Papa Leo XIV:Ulimwengu wa kidijitali unaleta changamoto hata kwa Watawa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu akikutana alasiri Jumatano tarehe 26 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Sinodi wa Vatican, aliwahutubia takriban washiriki 160 wa Mkutano wa 104 wa Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa ya Kiume (USG). Mkutano huo, wenye kauli mbiu: "Imani Iliyounganika: Maombi Hai katika Enzi ya Kidijitali," unafanyika huko Sacrofano nje ya Roma. Katika hotuba yake Papa alisisitiza kwamba itakuwa ni kutoona mbali kupuuza fursa za ajabu za teknolojia zinazotoa kwa ajili ya ushirika na utume, na kutuwezesha kuwafikia watu walio mbali hata wale ambao, kwa njia za kawaida, wanajitahidi kukaribia jumuiya zetu."
Papa Leo XIV mwenyewe hivi karibuni alitumia fursa hizo alipowasiliana kupitia matangazo ya moja kwa moja kutokea Vatican na vijana 16,000 waliohudhuria Mkutano wa Kitaifa wa Vijana Wakatoliki katika Uwanja wa Lucas Oil huko Indianapolis, Marekani. Hata hivyo, aina hii ya ushiriki, Papa Leo alionya, inaweza pia kushawishi sana na sio kila wakati kuwa njia bora yaani njia yetu ya kujenga na kudumisha mahusiano. Alisema, kuna jaribu la kweli, "kubadilisha mahusiano halisi ya kibinadamu na miunganisho ya mtandaoni tu," hasa wakati kinachohitajika ni "uwepo, uvumilivu na usikilizaji wa muda mrefu, na kushiriki mawazo na hisia kwa undani." Alitumia tena ushauWatraka wa Kitume wa Papa Francisko wa Christus vivit yaani 'Kristo anaoishi' kuweza kusisitiza kwamba vyombo vya kiutamaduni ni vya ushirika.
Mikutano mikuu, Mabaraza, Ziara za Kikanoni na mikutano ya malezi, haviwezi kuachwa kwenye ulimwengu wa kidijitali. Papa Leo alizidi kuonya dhidi ya kuweka kipaumbele urahisi na ufanisi wakati utunzaji wa kichungaji uko hatarini. Lazima tupinge dhana kwamba sisi ni wasimamizi wa huduma nyingi,"au kwamba tunaweza kujiruhusu kushangazwa na mwangaza wa ufanisi, kuzidiwa na moshi wa maelewano. Hatari ni kwamba tunasimama, au vinginevyo tunageuza safari yetu ya mhujaji kuwa mbio ya haraka na yenye kuchosha, tukisahau chanzo chake na mwisho wake. Kilicho muhimu, ni kutembea pamoja kama jumuiya, kama ndugu.
Papa Leo alinukuu barua ya Papa Francisko ya Fratelli tutti, ambayo inatoa mwaliko wa “kukutana katika 'sisi' ambayo ina nguvu zaidi kuliko mkusanyiko wa nafsi ndogo za kibinafsi, na kugundua na kuwasilisha fumbo la kuishi pamoja." Kanisa ni fundisho la kijamii na kihistoria la kisinodi, kiumbe ambacho vifungo hubadilishwa kuwa vifungo vitakatifu, kuwa njia za neema." Uhusiano ni muhimu zaidi ili kukuza ni wetu na Mungu. Hii ndiyo maana sala ni muhimu katika maisha ya kila mtu aliyewekwa wakfu ambayo uwzesha nafasi ya uhusiano moyo hufunguka kwa Bwana, kujifunza kusali na kupokea kwa uaminifu.
Papa Leo alisisitiza tena kwamba katika sala, tunashuhudia sisi ni nani hasa: viumbe wanaohitaji kila kitu, walioachwa mikononi mwa Mungu mwenye huruma wema. Kwa kutazama zana za kidijitali na mahusiano halisi kuwa pamoja kuzungumza na kusikiliza, katika usawa wa nuru na kivuli, Papa aliwasihi watawa hao kukumbatia changamoto ya kuunganisha nova et vetera, yaani mapya na ya zamani, ili kuhifadhi na kukuza uhusiano na Mungu na sisi kwa sisi, bila kupuuza au kuzika, kutokana na uvivu au hofu, vipaji vipya ambavyo Bwana anaweka mikononi mwetu”.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
