Papa Leo XIV Nicea:Tukatae vikali matumizi ya dini kuhalalisha vita,vurugu

Papa Leo XIV akiwa İznik,pamoja na Patriaki Bartholomayo na viongozi na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo duniani,waliadhimisha kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa I wa Kiekumeni.Hafla ilikuwa na utulivu na utakatifu,iliyofanyika juu ya magofu ya Basilika ya kale ya Mtakatifu Neophytos.Papa alitoa wito kupinga vikali matumizi ya dini kuhalalisha vita na vurugu,msimamo mkali na ushabiki.Tushinde kashfa ya migawanyika na kukuza umoja.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika eneo ambalo kwa siku therathini Mtaguso wa Kwanza wa Kiekumenj ulifanyika mnamo mwaka 325 huko Nicea, kilomita 70 kutoka Istanbul, katika ule mkutano wa kihistoria ulioitiswha na Mfalme Constantine, ambao ulitoa matokeo mazuri ya Kanuni ya Imani, ambayo hadi leo hii, inatuunganisha Wakristo wote bilioni mbili na nusu duniani kote. Ndiyo ambayo baada ya miaka 1700, imeona wawakilishi wa Makanisa mbali mbali wakiunganika katika eneo hilo kwa kusika, maneno yale yale yakitangazwa chini ya anga wazi sana kiasi kwamba yanachanganyika na mwambao wa matope ya Ziwa la Iznik ambapo katika hafla hiyo ilikuwa tulivu na utakatifu iliyofanyika juu ya magofu ya Basilika ya kale ya Mtakatifu Neophytos.

Wakati wa sala ya  Kiekumene
Wakati wa sala ya Kiekumene   (@Vatican Media)

Hapo kulikuwa na Papa Leo XIV, Maaskofu, Mapatriaki, na viongozi, wawakilishi wa makanisa ya Kikristo duniani, wakithibitisha tena ujumbe wa udugu wa ulimwengu wote na udugu  ulio ndani ya kila dini, na kuomba kwa mara nyingine tena  ili sisi sote tuwe wamoja.  Na hasa zaidi kukataa kwa nguvu matumizi ya dini kuhalalisha vita na vurugu, pamoja na aina yoyote ya ufuasi wa kidini na ushabiki, badala yake kufuata njia za makutano ya kidugu, mazungumzo, na ushirikiano. Katika wakati huo mzuri kwa viongozi hao kwenye mkutano huo wa kidini ambapo waliomba pamoja Baba Mtakatifu Leo alianza hotuba yake  ya Tatu kuwa  “Katika kipindi cha historia kilichojaa ishara nyingi za kusikitisha, ambapo watu wanakabiliwa na vitisho vingi dhidi ya heshima yao, maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza la Nicea ni fursa nzuri ya kujiuliza Yesu Kristo ni nani katika maisha ya wanaume na wanawake leo, na yeye ni nani kwa kila mmoja wetu binafsi. Swali hili ni muhimu sana kwa Wakristo, ambao wanahatarisha kumpunguza Yesu Kristo hadi aina ya kiongozi mwenye karama au superman, upotoshaji ambao hatimaye husababisha huzuni na mkanganyiko.

Sala ya Kiekumeni
Sala ya Kiekumeni   (@Vatican Media)

Papa alisema kuwa kwa kukataa umungu wa Kristo, Arius alimpunguza hadi kuwa mpatanishi tu kati ya Mungu na ubinadamu, akipuuza ukweli wa Utu wa mwili kiasi kwamba Mungu na mwanadamu walibaki wametenganishwa bila kurekebishwa. Lakini kama Mungu hajawa mwanadamu, viumbe vinavyokufa vinawezaje kushiriki katika maisha yake ya kutokufa? Kilichokuwa hatarini huko Nicea, na kilicho hatarini leo hii, ni imani yetu kwa Mungu ambaye, katika Yesu Kristo, alifanyika kama sisi ili kutufanya kuwa "washiriki wa asili ya kimungu" (2 Pet 1:4; tazama Mtakatifu Irenaeus, Ushauri, 3, 19; Mtakatifu Athanasius, De Incarnatione, 54, 3). Kusadiki huku kwa imani ya Kikristo ni wa muhimu sana katika safari ambayo Wakristo wanaifanya kuelekea ushirika kamili. Kwani inashirikishwa na Makanisa na Jumuiya zote za Kikristo ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na zile ambazo, kwa sababu mbalimbali, hazitumii Imani ya Nicea-Konstantinopoli katika liturujia zao.

Papa Leo na viongozi wa kiekumene
Papa Leo na viongozi wa kiekumene   (@Vatican Media)

Papa alisisitiza kwamba  hakika, imani "katika Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana Pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya vizazi vyote…ns  umoja na Baba" (Imani ya Nicea) ni kifungo kikubwa ambacho tayari kinawaunganisha Wakristo wote. Kwa maana hiyo, tukimnukuu Mtakatifu Agostino, katika muktadha wa kiekumeni tunaweza pia kusema kwamba, "ingawa sisi Wakristo tu wengi, katika Kristo mmoja sisi tu tu wamoja" (Maelezo ya Zaburi 127). Kwa hivyo, tukiwa na ufahamu kwamba tayari tumeunganishwa na kifungo hicho kikubwa, tunaweza kuendelea na safari yetu ya kuzingatia zaidi Neno la Mungu lililofunuliwa katika Yesu Kristo, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, katika upendo na mazungumzo ya pande zote.

Kwa njia hii, Papa Leo XIV amesisitiza kuwa sote tunaalikwa kushinda kashfa ya migawanyiko ambayo kwa bahati mbaya bado ipo na kukuza hamu ya umoja ambayo Bwana Yesu aliiombea na kutoa maisha yake. Kadiri tunavyopatanishwa zaidi, ndivyo Wakristo wanavyoweza kutoa ushuhuda wa kuaminika kwa Injili ya Yesu Kristo, ambayo ni tangazo la matumaini kwa wote. Zaidi ya hayo, ni ujumbe wa amani na udugu wa ulimwengu wote unaovuka mipaka ya jamii na mataifa yetu (taz. Francisko, Hotuba kwa washiriki katika Kikao Kikuu cha Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Umoja wa Kikristo, 6 Mei 2022).

Kumbukizi ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea
Kumbukizi ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea   (@Vatican Media)

Leo, hii, Papa Leo XIV alisema, wanadamu wote wanaosumbuliwa na vurugu na migogoro wanaomba upatanisho. Hamu ya ushirika kamili miongoni mwa waamini wote katika Yesu Kristo daima huambatana na utafutaji wa udugu miongoni mwa wanadamu wote. Katika kanuni ya Imani ya Nicea, tunasaidiki imani yetu "katika Mungu mmoja, Baba." Hata hivyo, haingewezekana kumwita Mungu kama Baba ikiwa tungekataa kuwatambua kama kaka  na dada wanaume na wanawake wengine wote, ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu (taz Nostra Aetate, 5). Kuna udugu wa jumla wa wanaume na wanawake bila kujali kabila, utaifa, dini au mitazamo ya kibinafsi. Dini, kwa asili yake, ni hazina ya ukweli huu na zinapaswa kuwatia moyo watu binafsi, vikundi na watu kutambua hili na kulitekeleza.

Zaidi ya hayo, ni lazima tukatae vikali matumizi ya dini kuhalalisha vita, vurugu, au aina yoyote ya msimamo mkali au ushabiki. Badala yake, njia za kufuata ni zile za kukutana kidugu, mazungumzo na ushirikiano. Ninamshukuru sana Bartholomew, kwa sababu ilikuwa kwa hekima na busara kubwa kwamba aliamua kuadhimisha pamoja maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea mahali pale pale lilipofanyika. Vile vile aliwashukuru kwa dhati Wakuu wa Makanisa na Wawakilishi wa Umoja wa Kikristo Ulimwenguni ambao wamekubali mwaliko wa kushiriki katika tukio hilo. Mungu Baba, Mwenyezi na mwenye huruma, asikie sala za dhati tunazomtolea leo, na ajaalie kwamba maadhimisho haya muhimu yaweze kuzaa matunda tele ya upatanisho, umoja na amani.”

Eneo la Mtaguso wa Nicea miaka 1700 iliyopita
Eneo la Mtaguso wa Nicea miaka 1700 iliyopita   (@Vatican Media)

Ujumbe wa Patriaki Bartholomeo

Patriaki Bartholomew alitoa ujumbe wa kukaribisha ulioanza kwa hisia ya kuona ni wangapi wameitikia vyema mwaliko wa kuheshimu kumbukumbu na urithi wa Mtaguso Kwanza la Kiekumeni lililofanyika hapo Nicea miaka 1700 iliyopita. Tangu wakati huo, karne nyingi zimepita, misukosuko mingi, matatizo na migawanyiko mingi, lakini leo yote yako katika İznik: "Tunakaribia ukumbusho huu mtakatifu kwa heshima ya pamoja na hisia ya kawaida ya matumaini.... “Tuko hapa kutoa ushuhuda hai wa imani ile ile iliyooneshwa na Mababa wa Nicea. Turudi kwenye chanzo hiki cha imani ya Kikristo ili kusonga mbele," alisema Patriaki Bartholomew I.

Nicea katika kumbukumbu ya miaka 1700 ya mtaguso
Nicea katika kumbukumbu ya miaka 1700 ya mtaguso   (@Vatican Media)

Nicea, alisema Bartholomew, inatokana na neno la Kigiriki "victoria," na "wakati ulimwengu unapofikiria ushindi, unafikiria nguvu na utawala. Lakini kama Wakristo, tunaambiwa tufikiri tofauti. Ishara yetu ya ushindi wa fumbo, ni ishara isiyoweza kushindwa ya "Msalaba." Huu ni "upumbavu" kwa mataifa, ishara ya kushindwa, lakini kwetu sisi ni dhihirisho kuu la hekima na nguvu za Mungu. Kwa hivyo mahali hapa, ndiyo, ushindi unasherehekewa, lakini ushindi huo "sio wa ulimwengu huu." Ni ushindi wa imani, ambao kupitia huo "udhalimu wa dhambi unafutwa katika maisha yetu, utumwa wa uharibifu unayeyushwa, na dunia inainuliwa mbinguni," alithibitisha Partiaki.

Miaka 1700 ya Mtaguso wa  I wa Nicea
Miaka 1700 ya Mtaguso wa I wa Nicea   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui

28 Novemba 2025, 16:02