Papa Leo XIV:Tuwe wajenzi wa udugu katika dunia inayoteseka!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Chini ya anga lililikowa safi la blu, lenye mawingi meupe asubuhi Jumamosi tarehe 1 Novemba 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa wito wake kabla ya sala ya Malakia wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambapo pamoja na mwengine ya mtazamo wa furaha zaidi ya wakati ujao lakini pia yale ya dharura zaidi ya wakati huu unaomkubwa mwanadamu. Papa alisema “ Siku kuu ya Watakatifu Wote ni kumbukumbu hai, pumzi ya kina ya sherehe kubwa ambayo ubinadamu umekusudiwa. Kinachoizuia, wakati huo huo, ni migogoro na dhuluma za wakati huu, ambazo familia ya wanadamu inaitwa kukabiliana nazo kwa kujenga udugu.”
Utukufu wa leo unaelekeza macho yetu kuelekea "ukweli wa wakati ujao" wa mbinguni, furaha iliyoshirikishwa na Mungu, "iliyopo katika mambo yote katika yote," inayoweza kufichua "uzuri wa nyuso nyingi, zote tofauti na zote zinafanana na Uso wa Kristo." Hili linasimama katika tofauti kubwa na "yenye uchungu" na mikasa ya sasa, ambayo azimio lake limekabidhiwa kwa maombezi ya Bikira Maria na Watakatifu wote.
Kuwasalimia wajumbe wa Kanisa la Uingereza
Katika wito wake wa awali kabla ya sala ya Malaika, Papa aliwakaribisha na kuwasalimia wajumbe wa Kanisa la Uingereza wakiongozwa na Askofu Mkuu Stephen Cottrell wa York. Uwepo unaofufua "furaha" ulishirikishwa siku chache zilizopita katika "mkutano wa maombi ya kihistoria" na Mfalme Charles III wa Uingereza katika Kikanisa cha Kipapa cha Sistine. Matumaini ni kwamba Mwalimu mpya wa Kanisa, Mtakatifu John Henry Newman, "atawasindikiza Wakristo katika safari yao kuelekea umoja kamili."
Mshikamano wa "Mbio za Watakatifu"
Papa Leo XIV kadhalika alitoa salamu zake kwa washiriki vijana katika Mbio za Watakatifu, tukio "linalochanganya michezo na mshikamano na watoto walio katika mazingira magumu zaidi." Sasa katika toleo la mwaka wa kumi na saba na kutangazwa na Utume wa Don Bosco, mbio hizo zinapita katikati ya kituo cha kihistoria cha Roma na njia maalum ya Jubilei, inayounganisha basilika nne za Papa za mji mkuu.
Asante kwa kusoma makala hii.Ikiwa unataka kusasishwa,tunakualika kujiandikisha makala zetu kwa kubonyeza hapa: cliccando qui
