Papa Leo XIV:Ujumbe wa umoja kwa Wakristo wa Nicea&amani Lebanon
Vatican News
"Nimefurahi sana kuweza kutembelea Lebanon." Hivi ndivyo Papa Leo alivyojibu swali kuhusu safari yake ijayo kwenda(Turkiye)Uturuki na Lebanon. Saa arobaini na nane kabla ya kuondoka kwake kwenda Ankara, Papa alirudi Castel Gandolfo kwa siku yake ya kupumzika ya kila Juma Novemba 25, lakini pia ya kazi, kama alivyowaelezea waandishi wa habari nje ya makazi yake huko Villa Barberini Juma moja iliyopita. Na kama Jumanne iliyopita, Papa alijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliojaa barabarani pamoja na waamini mbalimbali waliomsalimia kwa kelele na nyimbo.
Akizungumzia safari yake ya kwanza ya kitume katika nchi mbili za Mashariki ya Kati, ambayo pia itajumuisha kusimama Iznik kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso Nicea, Papa alisisitiza kwamba ujumbe atakaopeleka utakuwa wa amani na matumaini, hasa wakati wa Jubilei hii. "Nitafurahi sana, kuwasalimu watu wote." Kisha akabainisha kwamba safari hiyo iliundwa kusherehekea maadhimisho ya Nicea. "Siku chache zilizopita, tulichapisha hati inayozungumzia kwa usahihi umuhimu wa umoja katika imani, ambao pia unaweza kuwa chanzo cha amani kwa ulimwengu mzima. Lazima tushuhudie." Pia alikumbuka mikutano yake na Patriaki wa Constantinopoli Bartholomew I na kusema: "Nadhani itakuwa fursa ya kipekee ya kukuza umoja miongoni mwa Wakristo wote."
Silaha Sio Jibu
Kuhusu mashambulizi ya mabomu ya Israeli dhidi ya vitongoji vya Hezbollah huko Beirut, Leo XIV, anayezungumzwa kwa Kiingereza alikiri kwamba "kuna sababu za wasiwasi." Kisha akatoa wito, akiwaalika kila mtu "kutafuta njia za kuachana na matumizi ya silaha kama njia ya kutatua matatizo." Aliwasihi kuheshimiana, kukaa pamoja ili kuanza mazungumzo, na "kufanya kazi ili kupata suluhisho la matatizo yanayotuhusu." Ni muhimu "kuwatia moyo watu wote kutafuta amani," alisema, akimaanisha Israeli na Hezbollah, "kutafuta haki, kwa sababu vurugu mara nyingi ni matokeo ya dhuluma." Kisha Papa alitaka kufanya kazi pamoja kwa ajili ya umoja mkubwa, kwa ajili ya heshima kubwa miongoni mwa watu na kwa dini zote.
Watu bado wanakufa nchini Ukraine
Maswali ya waandishi wa habari yanagusa mambo ya sasa, na Papa aliakisi Ukraine, ambayo iko vitani kwa miaka mitatu, wakati ambapo mpango wa amani uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump unajadiliwa. Lazima tusubiri. Namshukuru Mungu, wanafanya kazi, namshukuru Mungu," Papa Leo XIV aliendelea, "inaonekana wanakaribia zaidi. Kuna matatizo kadhaa katika mazungumzo, lakini ningependa kuwaalika kila mtu kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano, kwa sababu wengi bado wanakufa." Kwa hivyo anazindua tena mazungumzo ili kupata suluhisho.
Mawazo Mapya
Kuhusu janga la ukatili dhidi ya wanawake, katika Siku ya leo(25 Novemba 2025) iliyojitolea kwa mada hiyo, Papa Leo XIV alisisitiza kwamba lazima "tuanze na elimu ya vijana" kwa sababu "kila mtu anastahili heshima" na kila mwanadamu ana utu. Wito wake ni kukomesha ukatili, ambao mara nyingi huathiri hata vijana, kwa kuunda "mawazo tofauti." "Lazima tuwe watu wa amani wanaopenda kila mtu."
Namshukuru Mungu
Hatimaye, Papa Leo alikidhi udadisi wa waandishi wa habari kuhusu jinsi ambavyo yeye, Mmarekani, atakavyosherehekea Siku ya Shukrani, ambayo itaadhimishwa wakati wa safari yake. "Kuna mambo mengi ambayo ninashukuru. Ningependa kuwatia moyo kila mtu, hasa katika hafla ya likizo hii nzuri nchini Marekani, ambayo inawaunganisha watu wa imani tofauti au wale ambao hawana kipawa cha imani, kusema asante, kutambua kwamba sote tumepokea zawadi nyingi, kwanza kabisa zawadi ya uzima, kipawa cha imani, kipawa cha umoja." Kwa hivyo, Papa Leo alihimiza "kukuza amani na maelewano na kumshukuru Mungu" kwa yale aliyotupatia.
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida: cliccando qui
