Vita ya kwanza ya Dunia Vita ya kwanza ya Dunia 

Papa Leo XIV:Vita vya Kwanza vya Dunia,ni mauaji yasiyo na maana

Katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland wakati wa Katekesi yake Papa alikumbuka kumbukumbu ya miaka ya mwisho wa Vita vya Kwanza vya Dunia,akinukuu usemi maarufu wa Papa Benedikto XV:"Tuilinde kwa moyo uliojikita katika Injili."Katika salamu kwa Kiitaliano,alimtaja Mama Eliswa Vakayil,aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri nchini India.Kwa kujitolea kwake kwa ukombozi wa wasichana maskini zaidi,"uwemsukumo kwa wote wanaofanya kazi,katika Kanisa na katika jamii,kwa ajili wanawake."

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, akiwasalimu waamini wa Poland waliohudhuria Katekesi yake, tarehe 12 Novemba 2025 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, alisisitiza thamani ya amani, akikumbuka kumbukumbu ya mwisho ya "mauaji yasiyo na maana" ya Vita vya Kwanza vya Dunia, kama Papa Benedikto XV alivyoiita, iliyoadhimishwa tarehe 11 Novemba 2025.

Mahujaji
Mahujaji   (@Vatican Media)

Papa Leo alisema "Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya amani," ambayo, kama Mtakatifu Agostino alivyosema, "hakuna kilicho bora zaidi. Tuihifadhi kwa mioyo iliyojikita katika Injili, katika roho ya udugu na upendo kwa nchi yetu." Baba Mtakatifu Leo XIV pia alikumbusha kwamba mwisho wa mgogoro huo, kwa watu wengi, wakiwemo Wapoland, uliambatana na "mapambazuko ya uhuru."

Mama Eliswa Vakayil
Mama Eliswa Vakayil

Akiwasalimu mahujaji wa Italia, Papa Leo XIV alikumbuka mfano wa Mama Eliswa Vakayil, mwanzilishi wa Shirika la tatu la  Watawa wa Karmeli wa Mtakatifu Theresa aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri  Jumamosi,  tarehe 8 Novemba 2025 huko Kochi, katika jimbo la Kerala,  India.

Papa Leo hasa alikumbuka kazi ya mtawa huyo kwa ajili ya wanawake walio pembezoni mwa jamii; kwa hivyo alionesha matumaini kwamba "kujitolea kwake kwa ujasiri kwa ajili ya ukombozi wa wasichana maskini zaidi" kutakuwa "chanzo cha msukumo kwa wote wanaofanya kazi, katika Kanisa na katika jamii, kwa ajili ya heshima ya wanawake."

Maaskofu walioshiriki Katekesi wakimsalimia Papa
Maaskofu walioshiriki Katekesi wakimsalimia Papa   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu pia aliwakumbusha waamini wa Kroatia, hasa wale wa Jimbo la  Gospić-Senj, ambalo inaadhimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwake,wakisindikizwa na Askofu Marko Medo, kwamba "zawadi kubwa zaidi tunayoweza kutoa ni imani hai inayooneshwa kwa kuwajali wengine."

Baada ya Katekesi

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here

 

12 Novemba 2025, 14:17