2025.11.03 2°Papa aliongoza ibada ya misa takatifu kwa ajili ya Papa Francisko, makardinali na maaskofu waliokufa ndani ya mwaka huu 2025. 2025.11.03 2°Papa aliongoza ibada ya misa takatifu kwa ajili ya Papa Francisko, makardinali na maaskofu waliokufa ndani ya mwaka huu 2025.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:ni uzoefu wa kifo hasa cha vurugu kinachowaua wasio na hatia na kutuacha tumekata tamaa

Papa aliadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa kumkumbuka mtangulizi wake na makadinali na maaskofu wote waliofariki mwaka huu. Katika mahubiri yake,Papa alizungumzia maumivu na kashfa ya kifo cha "mtu dhaifu" aliyenyakuliwa "kwa ugonjwa au mbaya zaidi na vurugu za kibinadamu."Lakini kwa kukakabiliwa na hili, tumaini la Kikristo linatusaidia kutazama mbali: "Hatuna huzuni kama wengine wasio na tumaini."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba MtakatifuLeo XIV akiongoza misa katika  Madhabahu ya Kiti cha Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuombea pumziko la roho za Papa Francisko na makardinali nane na maaskofu wakuu 134 na maaskofu walifariki katika mwaka huu 2025, Jumatatu tarehe 3 Novemba 2025, alijikita na mada kuu ya Tumaini la Kikristo, tumaini la "Pasaka" la ufufuko. Katika mahubiri yake Baba Mtakatifu alisema, wapendwa Ndugu Kardinali na Maaskofu,  “leo hii tunarudia desturi nzuri, katika fursa ya Ukumbusho ya waamini marehemu wote ya kusherehekea Ekaristi kwa ajili ya kuwaombea Makardinali na Maaskofu waliotuacha mwaka huu unaoisha. Kwa upendo mkubwa, tunatoa kwa ajili ya roho teule ya Papa Francisko, aliyefariki baada ya kufungua Mlango Mtakatifu na kutoa Baraka ya Pasaka kwa Roma na Ulimwengu. Papa aliongeza kusema kuwa “Shukrani kwa Jubilei, sherehe hii, kwangu mimi, ya kwanza, inapata ladha ya kipekee: ladha ya tumaini la Kikristo.

Misa kwa ajili ya Kuombea Marehemu Papa Francisko,Makardinali na Maaskofu
Misa kwa ajili ya Kuombea Marehemu Papa Francisko,Makardinali na Maaskofu   (@Vatican Media)

Neno la Mungu tulilosikia linatuangazia. Kwanza kabisa, linafanya hivyo kwa alama kubwa ya kibiblia ambayo, tunaweza kusema, inafupisha maana ya Mwaka huu Mtakatifu wote: historia ya Luka ya wanafunzi wa Emau (Lk 24:13-35). Inawakilisha waziwazi hija ya matumaini, ambayo hupitia kukutana na Kristo aliyefufuka. Sehemu ya kuanzia ni uzoefu wa kifo, na katika hali yake mbaya zaidi: kifo cha vurugu kinachowaua wasio na hatia na hivyo kutuacha tukiwa tumekata tamaa. Ni watu wangapi, ni “wadogo” wangapi! hata katika siku zetu wanaoteseka na kiwewe cha kifo hiki cha kutisha kwa sababu kimeharibiwa na dhambi. Kwa kifo hiki hatuwezi na hatupaswi kusema “laudato si’,” kwa sababu Mungu Baba hataki, na akamtuma Mwanawe mwenyewe ulimwenguni ili atuokoe kutoka humo. Imeandikwa: Kristo ilibidi ateseke haya ili aingie katika utukufu wake (taz. Lk 24:26) na kutupa uzima wa milele. Yeye pekee ndiye anayeweza kubeba kifo hiki cha uharibifu juu yake mwenyewe na ndani yake mwenyewe bila kuharibiwa nacho.

Misa kwa ajili ya kuwaombea marehemu Papa Francisko, Makardinali na Maaskofu
Misa kwa ajili ya kuwaombea marehemu Papa Francisko, Makardinali na Maaskofu   (@Vatican Media)

Yeye pekee ndiye aliye na maneno ya uzima wa milele (taz. Yh 6:68), tunakiri hili kwa hofu hapa karibu na Kaburi la Mtakatifu Petro na maneno haya yana nguvu ya kuamsha imani na tumaini mioyoni mwetu.Yesu anapochukua mkate mikononi mwake, ambayo ilikuwa imepigiliwa misumari msalabani, anatangaza baraka, anaumeha, na kuutoa, wakati huo macho ya wanafunzi yanafunguka, imani inachanua mioyoni mwao, na kwa imani, tumaini jipya. Ndiyo! Sio tena tumaini walilokuwa nalo hapo awali na walilopoteza. Ni ukweli mpya, zawadi, neema ya Aliyefufuka: ni tumaini la Pasaka. Kama vile maisha ya Yesu aliyefufuka si tena kama yalivyokuwa hapo awali, bali ni mapya kabisa, yaliyoumbwa na Baba kwa nguvu ya Roho, vivyo hivyo tumaini la Mkristo si tumaini la mwanadamu, wala la Wagiriki wala la Wayahudi, halitegemei hekima ya wanafalsafa wala haki inayotokana na sheria, bali kwa ukamilifu kabisa juu ya ukweli kwamba Aliyesulubiwa amefufuka na amemtokea Simoni (tazama Luka 24:34), kwa wanawake, na kwa wanafunzi wengine.

Misa kwa ajili ya kuwaombea Marehemu  Papa Francisko, Makardinali na Maaskofu
Misa kwa ajili ya kuwaombea Marehemu Papa Francisko, Makardinali na Maaskofu   (@Vatican Media)

Ni tumaini ambalo halitazami kwenye upeo wa dunia, bali zaidi ya hapo, kwa Mungu, kwenye kilele na kina ambacho Jua lilichomoza ili kuwaangazia wale waliokaa gizani na kivuli cha mauti (taz.Lk 1:78-79). Hapo, ndiyo, tunaweza kuimba: "Utukuzwe, Bwana wangu, kupitia Dada yetu Kifo cha Mwili." Upendo wa Kristo, aliyesulubiwa na kufufuka, umebadilisha kifo: kutoka kwa adui, amekifanya kuwa dada, amekidhibiti. Na mbele ya kifo, "hatuhuzuniki kama wengine wasio na tumaini" (1 Thes 4:13). Tunahuzunika, bila shaka, mpendwa wetu anapotuacha. Tunashtuka wakati mwanadamu, hasa mtoto, "mdogo," dhaifu, anapochukuliwa na ugonjwa au, mbaya zaidi, na vurugu za kibinadamu. Kama Wakristo, tunaitwa kubeba uzito wa misalaba hii pamoja na Kristo. Lakini hatuna huzuni kama wale wasio na tumaini, kwa sababu hata kifo cha kusikitisha zaidi hakiwezi kumzuia Bwana wetu kukaribisha roho zetu mikononi mwake na kubadilisha miili yetu inayokufa, hata iliyoharibika zaidi, kuwa mfano wa mwili wake mtukufu (Wafilipi 3:21).

Misa kwa ajili ya kuwaombea Marehemu
Misa kwa ajili ya kuwaombea Marehemu   (@Vatican Media)

Kwa sababu hiyo, Wakristo hawaiti mahali pa mazishi kuwa pa "maiti," yaani, "miji ya wafu," bali "makaburi," ambayo kiukweli inamaanisha "mabweni," mahali ambapo mtu hupumzika, akisubiri ufufuko. Kama mtunga Zaburi  alivyotabiri kuwa: "Kwa amani nitajilaza na kulala, / kwa ajili yako pekee, Ee Bwana, unifanye niishi katika imani" (Zab 4:9). Papa Leo XIV kwa njia njiyo alibainisha kuwa Papa Francisko na ndugu zetu Makardinali na Maaskofu, ambao tunawatolea Sadaka ya Ekaristi leo hii, wameishi, wameshuhudia, na kufundisha tumaini hili jipya la Pasaka. Bwana aliwaita na kuwateua kuwa wachungaji wa Kanisa lake, na kupitia huduma yao—kwa kutumia lugha ya Kitabu cha Danieli: “waliwaongoza wengi kwenye haki” (taz. Dan. 12:3), yaani, waliwaongoza kwenye njia ya Injili kwa hekima itokayo kwa Kristo, ambaye amekuwa kwetu hekima, haki, utakaso, na ukombozi (taz. 1 Kor. 1:30). Nafsi zao zisafishwe kutokana na kila doa na zing’ae kama nyota mbinguni (taz. mst. 3). Na faraja yao ya kiroho itufikie sisi, bado wasafiri duniani, katika ukimya wa maombi: “Mtumaini Mungu; nitamsifu tena, wokovu wa uso wangu na Mungu wangu” (Zab. 42:6, 12).

Misa Papa Novemba 3
03 Novemba 2025, 15:24