2025.11.11 Papa ameadhimisha Misa katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi huko kilima cha Aventino,Roma katika kumbukizi ya miaka 125 ya Kutabaruku Kanisa hilo. 2025.11.11 Papa ameadhimisha Misa katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi huko kilima cha Aventino,Roma katika kumbukizi ya miaka 125 ya Kutabaruku Kanisa hilo.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Tunamhitaji Yesu Kristo,Mwana wa Mungu aliye hai&Tumeitwa kuwapeleka wote

Katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Papa Leo XIV,Novemba 11,Roma,katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi,kwa kumbukumbu ya miaka 125 ya kutabaruku Kanisa hilo,katika mahubiri:“Tumeitwa kumtafuta Yesu na kumpeleka kwa wote tunaokutana nao,tukishukuru kwa zawadi alizotupatia na kwa upendo wa waliotutangulia.Tukikabiliwa na changamoto za wakati wetu,Kristo awe kitovu cha uhai wetu.”Ni katika Kanisa lililoanzishwa na Papa Leo XIII.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi, lililoko katika kilima cha Aventine,  Roma, jioni ya tarehe 11 Novemba 2025, katika kumbukizi ya miaka 125 ya Kutabaruku kwa Kanisa hilo. Papa alianza mahubiri yake kwa kusema: "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu" (Mt 16:18). Kaka na dada wapendwa, tumesikiliza maneno haya ya Yesu tunapokumbuka kumbukumbu ya miaka 125 ya Kutabaruku kwa Kanisa hili, lililotamaniwa sana na Papa Leo XIII, aliyehamasisha ujenzi wake. Alikusudia jengo hili, pamoja na lile la Chuo cha Kimataifa kilichounganishwa, kuchangia katika kuimarisha uwepo wa Wabenediktini katika Kanisa na Ulimwengu, kupitia umoja mkubwa zaidi ndani ya Shirikisho la Wabenediktini.

Misa katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi
Misa katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi   (@Vatican Media)

Papa Leo aliendelea,  hili ndilo lengo ambalo Ofisi ya Mkuu wa Watawa ilianzishwa pia. Aliamini kwamba Shirika lao la kale linaweza kuwa na huduma kubwa kwa ustawi wa Watu wote wa Mungu katika wakati mgumu, kama vile mabadiliko kutoka karne ya 19 hadi karne ya 20. Papa Leo alieleza kwamba,  kiukweli utawa, kutoka asili yake, umekuwa ukweli wa "mpaka", ambao umewasukuma wanaume na wanawake jasiri kuanzisha vituo vya sala, kazi na upendo katika maeneo ya mbali na yasiyofikika, mara nyingi hubadilisha maeneo yaliyotengwa kuwa ardhi yenye rutuba na tajiri, kilimo na kiuchumi, lakini zaidi ya yote kiroho.

Misa katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi

Kwa hivyo, Monasteri imejitambulisha zaidi kama mahali pa ukuaji, amani, ukarimu, na umoja, hata katika vipindi vya giza zaidi vya historia. Wakati wetu pia hutoa changamoto. Mabadiliko ya ghafla tunayoshuhudia yanatupinga na kutuhoji, yakiibua masuala ambayo hayakuonekana hapo awali. Kwa njia hiyo Papa alisisitiza kuwa Sherehe hiyo inatukumbusha kwamba, kama Mtume Petro, pamoja na Benedikto na wengine wengi, sisi pia tunaweza kujibu madai ya wito tuliopokea tu kwa kumweka Kristo katikati ya uhai wetu na utume wetu, kuanzia kitendo hicho cha imani kinachotufanya tumtambue kama Mwokozi na kutafsiri katika sala, masomo, na kujitolea kwa maisha matakatifu.

Papa akihubiri
Papa akihubiri   (@Vatican Media)

Papa alithibitisha tena katika hilo kwamba hapo,  “haya yote yanatimizwa kwa njia mbalimbali: kwanza katika liturujia, kisha katika Lectio divina,yaani mafundisho ya Neno la Mungu katika utafiti, katika uchungaji, kwa ushiriki wa watawa kutoka ulimwenguni kote na kwa uwazi kwa mapadre, wanaume na wanawake watawa, na watu wa kawaida kutoka asili na hali tofauti zaidi. Monasteri, Athenaeum, Taasisi ya Liturujia, na shughuli za kichungaji zinazohusiana na Kanisa, kulingana na mafundisho ya Mtakatifu Benedikto, lazima zikue zaidi kwa ushirikiano kama "shule halisi ya utumishi wa Bwana" (Mtakatifu Benedikto, Kanuni, Utangulizi, 45).

Waamini watu wa Mungu
Waamini watu wa Mungu   (@Vatican Media)

Kwa sababu hiyo, Papa Leo XIV alibainisha jinsi ambavyo alifikiria ugumu ambao “tunajikuta kama ukweli ambao lazima tutamani kuwa na moyo unaodunda katika mwili mkubwa wa ulimwengu wa Wabenediktini, huku Kanisa likiwa katikati yake, kulingana na mafundisho ya Mtakatifu Benedikto.” Akidadavua Masomo, Papa Leo XIV alisema, “Somo la kwanza (taz. Ezekieli 43:1-2, 4-7a) lilituonesha taswira ya mto unaotiririka kutoka Hekaluni. Picha hiyo inaendana vizuri sana na ile ya moyo ukisukuma damu ya uhai mwilini, ili kila kiungo kiweze kupokea lishe na nguvu kwa manufaa ya wengine (taz. 1 Kor 12:20-27); pamoja na lile la jengo la kiroho ambalo somo la pili lilizungumzia, lililojengwa juu ya mwamba imara ambao ni Kristo (taz. 1 Pet 2:4-9).

Wakati wa Misa
Wakati wa Misa   (@Vatican Media)

Katika kundi la bidii la Mtakatifu Anselmi, hapa ndipo pawe mahali ambapo kila kitu huanza na ambapo kila kitu kinarudi ili kupata uthibitisho, na kina,  mbele za Mungu, kama alivyopendekeza. Mtakatifu Yohane Paulo II( San Giovanni Paolo II, wakati wa ziara yake katika Chuo cha Kipapa,  katika hafla ya kuadhimisha miaka mia moja ya kuanzishwa kwake, alisema, huku akirejea Mtakatifu wake mlinzi kwamba: "Mtakatifu Anselmi anawakumbusha kila mtu [...] kwamba ujuzi wa mafumbo ya kimungu sio ushindi wa akili za kibinadamu, bali ni zawadi ambayo Mungu huwapa wanyenyekevu na waamini,"(hotuba-Discorso, 1°Juni 1986).

Alikuwa akimaanisha, kama ilivyotajwa, mafundisho ya Mwalimu wa Aosta, lakini sisi tunataka kwamba huu pia uwe ni ujumbe wa kinabii ambao Taasisi hii inaleta kwa Kanisa na ulimwengu, kama utimilifu wa utume ambao sote tumeupokea: kuwa watu ambao Mungu amejipatia mwenyewe, ili tuweze kutangaza kazi za ajabu za yeye aliyetuita kutoka gizani kuingia katika nuru yake ya ajabu (taz. 1 Pet 2:9).

Misa na Baba Mtakatifu
Misa na Baba Mtakatifu   (@Vatican Media)

Kutabaruku ni wakati mzito katika historia ya jengo takatifu ambalo limetakaswa kuwa mahali pa kukutania kati ya nafasi na wakati, kati ya mwisho na usio na mwisho, kati ya mwanadamu na Mungu: mlango wazi wa umilele, ambapo roho hupata jibu la"mvutano kati ya muunganiko wa wakati na mwanga wa wakati, wa upeo mkubwa [...] ambao unatufungulia wakati ujao kama sababu ya mwisho inayovutia,"(Waraka wa Papa Francisko wa Evangelii gaudium, 222), katika kukutana kati ya utimilifu na ukomo unaoambatana na safari yetu ya kidunia.

Wakati wa misa
Wakati wa misa   (@VATICAN MEDIA)

Mtaguso wa Pili wa Vatican(Concilio Vaticano II ),unaelezea haya yote katika mojawapo ya vifungu vyake vizuri zaidi, unapofafanua Kanisa kama "la kibinadamu na la kimungu, linaloonekana lakini lililojaa uhalisia usioonekana, lenye bidii katika matendo na lililojitolea kutafakari, lipo duniani lakini ni msafiri; […] kwa njia ambayo, hata hivyo, kile kilicho cha binadamu ndani yake kimepangwa na kuwekwa chini ya umungu, kinachoonekana kwa kisichoonekana, kitendo cha kutafakari, uhalisia wa sasa kwa mji ujao, ambapo tunaelekea,”(Katiba Sacrosanctum Concilium, 2).

Ni uzoefu wa maisha yetu na maisha ya kila mwanamume na mwanamke katika ulimwengu huu, Papa Leo XIV alisisitiza kwamba,  tukitafuta jibu hilo la mwisho na la msingi ambalo "mwili wala damu" haziwezi kufichua, ila Baba aliye mbinguni pekee (taz. Mt. 16:17); Hatimaye tunamhitaji Yesu, "Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mt 16, 16). Tumeitwa kumtafuta, na kwake tumeitwa kuwapeleka wote tunaokutana nao, tukishukuru kwa zawadi alizotupatia, na zaidi ya yote kwa upendo alioutanguliza (taz. Rm. 5:6). Hekalu hili litazidi kuwa mahali pa furaha, ambapo tunapata uzoefu wa uzuri wa kushirikisha na wengine kile ambacho tumepokea bure (taz. Mt. 10:8).

Papa alibusu Msalaba
Papa alibusu Msalaba   (@Vatican Media)

Katika ibada hiyo takatifu, iliyohuishwa na nyimbo za Gregorian, katika mahali pa ibada palipotamaniwa sana na Papa Leo XIII, aliyehimiza ujenzi wake. Iliwekwa wakfu mnamo tarehe 11 Novemba 1900, ikiwekwa taji la kuanzishwa kwa Chuo cha Kipapa cha Kimataifa cha Mtakatifu Anselmi  mnamo 1887 na kuzaliwa kwa Shirikisho la Wabenediktini  mnamo tarehe 19 Aprili 1893, kufuatia mwaliko wa Papa Pecci(Papa Leo XIII)  kwa Mashirika  kadhaa ya Kibenediktini kuungana.

Aliingia Kanisani akiwanyunyizia maji ya Baraka
Aliingia Kanisani akiwanyunyizia maji ya Baraka   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV aliingia kanisani, ambapo kumbukumbu ya mwanga uliowekwa wakfu kwa Mtakatifu Hildegard wa Bingen ilioneshwa kwa mara ya kwanza, pamoja na Kardinali Lorenzo Baldisseri, mkuu wa Kanisa,  kulikuwa na Sebastian Edavazhickal Paul, Abate wa Mtakatifu Anselmi, Abate  Jeremias Schröder, na Mapadre  wengine wa Kibenediktini. Alivuka Kanisa  katiti akiwanyunyizia waamini maji ya baraka, kisha alisimama kusali kwenye madhabahu ya Sakramenti Takatifu, mwishoni mwa Kanisa hilo kulia, ambapo picha ya Golgotha​​​​ ya  Kristo Aliyesulubiwa, Maria na Yohane zinaoneshwa.

Mapadre walioshiriki misa
Mapadre walioshiriki misa   (@Vatican Media)
Papa kwa wabenediktini

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here

 

 

11 Novemba 2025, 20:19