Papa Leo XIV katika Msikiti wa Bluu:Roho ya ukimya wa tafakari na kusikiliza
Na Salvatore Cernuzio – Istanbul
Bila viatu, mikono yake ikilegezwa kama kawaida chini na kichwa chake kikiwa kimeelekezwa juu, akitazama vigae 21,043 vya kauri ya zumaridi. Hivi ndivyo Papa Leo XIV alivyoingia katika Msikiti wa Sultan Ahmed wa Istanbul, Jumamosi tarehe 29 Novemba, yapata saa 3:10 asubuhi masaa ya huko. Hiki ni kile kinachoitwa "Msikiti wa Bluu," mojawapo ya Jengo la kumbu kumbu lenye kuchochea hisia zaidi katika jiji kuu la Uturuki, ambalo hapo awali lilitembelewa na Papa Benedikto XVI mnamo 2006 na Papa Francisko mnamo 2014 (siku hiyo hiyo kama ya leo, Novemba 29).
Miongoni mwa tukio katika "Msikiti wa Bluu," huku kukiwa na mwanga ulioundwa na madirisha 260, ni kunguru tu aliyevunja ukimya ulioenea takriban dakika kumi na tano za ziara hiyo. Ziara ambayo, kama Ofisi ya Habari ya vyombo vya Habari Vatican ilivyoripoti kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba, Papa Leo XIV alitumia muda wa"kimya, katika roho ya kukumbuka na kusikiliza, kwa heshima kubwa katika mahali hapo na kwa imani ya wale waliokusanyika hapo katika sala.
![]()
Papa huko Sultan Ahmed, katika Msikiti wa Blu(@Vatican Media)
"Nimeridhika na hali halisi"
Muezzin Aşkın Musa Tunca, ambaye alisindikizana na Papa katika ziara yake kwa kile anachokiita "nyumba ya Mwenyezi Mungu," aliwaeleza waandishi wa habari waliokuwepo kwenye tukio hilo kwamba ameridhika saa kwa hali halisi iliyoonekana kwenye msikiti. Tangu alipofika kwenye ua la Msikiti huo jua lilikuwa tayari limechomoza juu ya minara sita. Huu ni upekee wa Msikiti wa Sultan Ahmed (ambapo kawaida misikiti huwa na minara minne), ulizidi katika suala hili tu na Msikiti wa Kaaba huko Makka, ambao una minara saba. Pamoja na Papa katika hatua hiyo ya awali ya siku yake ya tatu akiwa nchini Uturuki ambayo itaendelea na ziara ya Phanar kumwona Patriaki Bartholomew I na kuhitimisha kwa Misa katika Uwanja wa Volkswagen, walikuwa pia Waziri wa Utamaduni na Utalii, Mehmet Nuri Ersoy Mufti wa Mkoa wa Istanbul, Emrullah Tuncel; na Imamu wa Msikiti wa Sultan Ahmed, Kurra Hafız Fatih Kaya.
Pamoja nao, Papa Leo XIV alitembea kuelekea ukumbi wa maombi, huku kukiwa na maneno ya kunong'ona na paka wawili (wawili kati ya maelfu waliokuwa wakizunguka Istanbul) waliokuwa wakizunguka zulia jekundu. Msafara wa Papa pia ulijumuisha Makardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, na George Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Dini Mbalimbali. Kila mtu alisimama kwa muda mrefu mbele ya mimbari ya muhazain, huku Tunca akielezea usanifu na kazi ya nafasi hii msikitini ambapo waumini wa kiislamu wanaitwa kusali. Kisha Papa alipita mbele ya "Mihrab," sehemu ya marumaru inayoonesha mwelekeo wa Makka, ambayo pia ina Sura 19—inayomrejea Bikira Maria. Aliendelea na ziara yake, akitazama mara kadhaa kwenye kuran na dari yenye urefu wa mita 23.
![]()
Papa katika Msikiti wa Bluu(@Vatican Media)
Mkutano wa faragha na viongozi wa makanisa na jamii za Kikristo
Picha ya kikundi ilihitimisha ziara hiyo. Papa aliondoka Msikiti wa Bluu muda mfupi kabla ya saa 3:25 asubuhi kwa gari hadi Kanisa la Kiorthodox la Mor Ephrem Syriac, lililoko Yeşilköy, upande wa Ulaya wa Istanbul. Kanisa hili lililowekwa wakfu kwa Ephrem wa Syria, lilizinduliwa mwaka 2023, baada ya ujenzi uliodumu kwa takriban muongo mmoja, kuahirishwa mara kadhaa kutokana na janga la Uviko na tetemeko la ardhi.
Ni Kanisa la kwanza na hadi sasa pekee lililojengwa nchini Uturuki tangu kuanzishwa kwa Jamhuri, na hapa Papa Leo XIV alikutana faragha na viongozi na wawakilishi wa makanisa na Jumuiya za Kikristo, ambao baadhi yao walikuwepo Novemba 28 huko Iznik katika sherehe ya kuadhimisha miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea. Kwa hiyo wakiwa hao wameketi kuzungumza meza ya mduara, na aliyemkaribisha Papa alikuwa Patriaki wa Kiekumeni wa Constantinople, Bartholomew I, ambaye atakutana naye tena huko Phanar, kiti cha Upatriaki alasiri, na ambaye atasaini naye Tamko la Pamoja. Kitendo cha mwisho cha siku hiyo kitafanyika baada ya Sala ya pamoja wakati wa ibada katika Kanisa Upatriaki la Mtakatifu George, kabla ya Misa, ambayo kwa sasa inatarajiwa kuwaona waamini wapatao 4,000.
![]()
Meza ya mduara na Papa na viongozi wa Kikristo(@Vatican Media).
Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui
