Mkuu wa Kibenediktini huko Mt Anselmi:"furaha kwa kuwasili kwa Papa Leo XIV"
Na Alessandro Guarasci –Vatican.
Kanisa la Mtakatifu Anselmi kwenye Kilima cha Aventine, Jijini Roma ni mahali panapohusishwa na "Papa Leo," si tu kwa sababu Papa Provost atatembelea leo, hii tarehe 11 Novemba 2025, saa 11. 00 jioni katika maadhimisho ya Misa inayoadhimisha kumbukumbu ya miaka 125 ya kuwekwa wakfu kwa Kanisa hilo, lakini pia kwa sababu ni Papa Leo XIII aliyelitakasa Kanisa hiko mnamo tarehe 11 Novemba 1900.
Miaka michache iliyopita, Papa wa Rerum Novarum, ambaye alitaka kuunganisha mashirika kadhaa ya Kibenediktini katika Shirikisho linaloongozwa na Mkuu wake Abate wa hapo Mtakatifu Anselmi alikuwa amemkabidhi Askofu Mkuu wa Catania, Giuseppe Benedetto Dusmet, jukumu la kufungua tena Chuo cha kale cha Mtakatifu Anselmi.
Pamoja na Abasia na Athenaeum ya Kipapa, Mtakatifu Anselmi, leo ni kitovu cha kiroho cha kiliturujia na wimbo wa Gregorian. Tangu 1962, imekuwa mahali pa kuanzia kwa maandamano ya toba yanayoongozwa na Papa kila Jumatano ya Majivu.
"Furaha kubwa"
Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican, Mkuu wa Wabenediktini Jeremias Schröder, ambaye ameongoza jumuiya ya Wabenediktini tangu Septemba mwaka 2024, alielezea uwepo wa Papa huko Mtakatifu Anselmi kama "wakati wa furaha kwetu." Kisha akaeleza kwamba Kanisa ni "mahali ambapo asili ya maisha ya Wabenediktini inaoneshwa," ikionyeshwa na Ora et Labora ya Mtakatifu Benediktini.
Mtakatifu Anselmi ni "kitovu ambapo familia zote za watawa kote ulimwenguni zimeunganishwa, na kwa maana hii," alielezea, "kwetu sisi, imekuwa kweli mahali pa utambulisho wa utaratibu wetu."Mkuu wa Wabenediktini anakumbuka kwamba kuna takriban watawa elfu sita wa Wabenediktini na karibu watawa elfu kumi na mbili duniani kote; uwepo muhimu wa kike ambao, anasisitiza, lazima uthaminiwe na kuendelezwa, ikiwa ni pamoja na katika mtaala.
