2025.05.30 Patriaki  Bartholomew I. 2025.05.30 Patriaki  Bartholomew I.  (@Vatican Media) Tahariri

Ziara ya kwanza ya Kitume ya Papa Leo XIV katika njia za umoja na amani

Papa Leo XIV anapojiandaa katika Ziara yake ya kwanza ya Kitume,ambayo inampeleka Ankara,Istanbul na Iznik huko Türkiye na Beirut nchini Lebanon kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 2,Mwariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawalisiliano ametoa maoni juu ya ziara hiyo kama ishara ya umoja na amani kwa Mashariki ya Kati.

Na Andrea Tornielli

Kama ilivyokuwa kwa Papa Benedikto wa XVI katika Siku ya Vijana Duniani huko Cologne mnamo 2005, na kama ilivyokuwa kwa Papa Francisko kwa Siku ya Vijana(WYD) huko Rio de Janeiro mnamo 2013, Ziara ya  kwanza ya Papa Leo wa XIV inampeleka kwenye eneo ambalo tayari lilipangwa na mtangulizi wake. Atatembelea Iznik, huko Uturuki(Türkiye,) katika fursa ya kuadhimisha miaka 1,700 tangu Baraza la kwanza la Nicea, na Lebanon iliyokumbwa na vita, ili kutimiza ahadi iliyotolewa na Papa Francisko, ingawa vita na magonjwa vilimzuia kuitimiza.

Ziara ya kwanza ya Kitume ya Papa imekusudiwa kuadhimisha upapa wake. Papa Paulo wa VI, ambaye mnamo Januari 1964 alifanya hija ya kihistoria katika Nchi Takatifu, alimkumbatia Patriaki wa Constantinople, Athenagoras. Papa JYohane  Paulo wa II alifanya ziara  yake ya kwanza kwenda Puebla, Mexico. Na Papa Francisko aliwakumbatia mamilioni ya vijana nchini Brazil. Kwa bahati ya kipekee, Ziara inayoanza Alhamisi ambayo itampeleka Papa Leo awali  huko Ankara, Istanbul, na Iznik, kisha Beirut, inawakilisha karibu mchanganyiko wa kijiografia wa mada kuu mbili ambazo zimeibuka katika miezi hii ya kwanza ya upapa wake: umoja na amani. Umoja ndio kiini cha hatua ya kwanza, ili kuadhimisha Baraza la Nicea, ambalo liliweka alama ya kudumu historia ya Kanisa kwa kutangaza imani katika Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

Hakuna haja ya kuificha: tunahitaji kuzingatia mkutano wa Nicea kwa kuzingatia jeraha la Kanisa lililogawanyika, jeraha linaloendelea kutokwa na damu na ambalo katika miaka ya hivi karibuni limeona mipasuko mipya ikionekana. Kurudi na kumbukumbu hai wakati Makanisa yalipoungana, kwenye baraza ambalo pia lilifanywa ili kuunganisha tarehe ya Pasaka, ni ishara ya matumaini. Kutafakari umoja wa Kanisa, umoja kati ya Makanisa, mazungumzo ya kiekumene, kurudi kwenye mizizi ya Injili, ya Mababa, ya mabaraza ya kwanza, ni njia ya kujiruhusu kujeruhiwa na maneno ya Yesu: “ili wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami nilivyo ndani yako, nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” Umoja wa waamini katika Kristo una thamani isiyohesabika, si tu kwa ajili ya kutangaza Injili. Pia una thamani ya amani duniani.

Amani hii bado haipo katika nchi ambayo Yesu aliishi maisha yake ya kidunia, hasa katika maeneo ya Israeli na Palestina, na Lebanon, akipigwa mabomu na jeshi la Israeli ili kuwapiga wanamgambo wa Hezbollah. Hatua ya pili ya Safari ya Kitume inampeleka Papa Leo XIV katika eneo lililojaa migogoro ambayo imegharimu idadi kubwa ya maisha ya wanadamu, hasa raia, hasa watoto. Papa Leo alijiwasilisha kwa ulimwengu kwa maneno ya kwanza yaliyosemwa na Yesu baada ya Ufufuko: “Amani iwe nanyi nyote!” Sasa, anakwenda kuchunguza majeraha ya watu ambao hawajajua amani kwa miongo kadhaa. Anakwenda kupeleka ushuhuda wake kwa asiye na silaha mahali ambapo, hata katika siku za hivi karibuni, mngurumo mbaya wa mabomu umesikika, ili kusema 'hapana' kwa kile kinachodhaniwa kuwa hakiepukiki cha vita, chuki, na vurugu.

Anakwenda kuwafariji Wakristo wanaoishi katika nchi hiyo na katika nchi jirani na ambao wanajaribiwa kuacha ardhi yao, kuwakumbusha jinsi ya uwepo wao ulivyo wa thamani, na jinsi ushuhuda wao wa udugu na kuishi pamoja kwa amani na wale wa dini zingine ulivyo wa thamani.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

26 Novemba 2025, 16:20