Bango linaoonesha Papa Leo XIV katika barabara ya Uwanaja wa Ndege wa Beirut nchini Lebanon. Bango linaoonesha Papa Leo XIV katika barabara ya Uwanaja wa Ndege wa Beirut nchini Lebanon. 

Ziara ya Papa Leo XIV nchini Uturuki na Lebanon:Sauti ya amani

Msemaji Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Vatican Matteo Bruni,alielezea ziara ya kwanza ya kitume ya Papa,akizungumzia Ankara,Istanbul na Beirut,huku akisimama Iznik,jina la kisasa la Nicea ya kale,kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso.Hija yenye mielekeo mikali ya kiekumeni,pia ikilenga mazungumzo kati ya dini mbalimbali."Itakuwa fursa ya kuwa karibu na Jumuiya za Kikristo na makundi hayo mawili ya watu.Hatua zote muhimu zimechukuliwa ili kuhakikisha usalama."

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Mazungumzo na umoja miongoni mwa Wakristo wa madhehebu yote, ukaribu na jumuiya zilizoimarishwa na karne nyingi za historia, zilizoathiriwa na mikasa na mivutano ya zamani na ya hivi karibuni, na amani, mada  ambayo ni "karibu na moyo wa Papa" tangu kuonekana kwake kwa mara ya kwanza duniani na katika miezi hii saba ya upapa wake. Msemaji Mkuu wa  Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni, alionesha maelezo na  wakati huo huo, akatoa ufahamu kuhusu Ziara ya Kwanza ya Kitume ya Papa Leo XIV kwenda Uturuki na Lebanon. Kwa hiyo ni ziara yake kwa kwanza ya Papa wa Marekani, yenye mwelekeo mkubwa wa kiekumeni, ilijikita katika fursa ya sherehe huko Iznik (jina la kisasa la Nicea ya zamani kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso, na kwa marejeo muhimu ya matukio ya sasa, pamoja na uwepo wa Mrithi wa Petro katika viunga vya Mashariki ya Kati.

Safari ngumu kwa Nchi Mbili Muhimu

"Safari yenye changamoto kwa nchi mbili muhimu," alisema Dk  Bruni katika mkutano wa Jumanne tarehe 25 Novemba 2025, kwa waandishi wa habari watakaoandamana na Papa Leo XIV katika Ziara  yake kwenye Nchi zenye tamaduni za kale: Uturuki, mahali pa kuzaliwa kwa Mtakatifu Paulo, mahali pa Mitaguso nane ya kwanza, daraja kati ya walimwengu na mabara tofauti; Lebanon, chimbuko la Wafoinike, mahali ambapo wawakilishi wa dini tofauti huishi pamoja na mahali pa kukaribishwa kwa watu wanaokimbia vita na ugaidi. Wakati huo huo, ardhi iliyoharibiwa na umaskini na migogoro mbalimbali, kuanzia mlipuko wa bandari hadi mashambulizi ya Israeli kusini. Tukio la mwisho lilikuwa mnamo tarehe 23 Novemba 2025. Matokeo yake, maswali kadhaa ya waandishi wa habari yalijikita katika masuala ya usalama: "Masuala yote muhimu yameshughulikiwa,"Dk Bruni alisema.

Katika nyayo za watangulizi wake

Papa Leo XIV atajitumbukiza katika hali hizi kwa takriban Juma moja. Atakutana na nyuso, vikundi, na historia, atazungumza faraghani na Marais Recep Tayyip Erdoğan na Joseph Aoun; atawasalimu mamlaka za kiraia, kidini, na mikutano ya kidini; atatembelea misikiti na makanisa yaliyojengwa karne nyingi zilizopita au miaka ya 1990; atasafiri hadi Diyanet ya Uturuki; atasali katika Bandari ya Beirut, akiwakumbuka zaidi ya watu 200 waliokufa katika mlipuko wa 2020. Na zaidi ya yote, katika ziara hii, atafuata nyayo za watangulizi wake: Papa Yohane XXIII, ambaye, kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa Mwakilishi wa Petro, alikuwa mjumbe wa kitume nchini Uturuki; Paulo VI, ambaye alitembelea Uturuki mwaka 1976 na Lebanon akiwa njiani kuelekea India mwaka 1974; tena, Yohane Paulo II ambaye alikwenda Uturuki ili kuimarisha tena kujitolea "kwa umoja wa Wakristo wote" na kwa Lebanon mnamo 1997 (ziara ya ambayo aliunda ufafanuzi wa kihistoria wa "Nchi ya Ujumbe"), akichapisha Waraka wa  kitume Matumaini mapya ya Lebanon.

Kadhalika kuna Papa Benedikto XVI, ambaye alitembelea nchi zote mbili, moja karibu na mwanzo wa upapa wake na nyingine miezi mitano kabla ya kujiuzulu kwake. Hatimaye, Papa Francisko, ambaye alitembelea Uturuki mwaka 2014 na alikusudia kurudi  huko mnamo Mei 2025 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 1700 ya Nicea, lakini hakuweza kutembelea Lebanon, hamu aliyokuwa nayo hadi mwisho wa siku zake. Na kutoka kwa mtangulizi wake Francisko, Papa Leo XIV  anachukua kijiti cha "hija" hii ya kwanza hadi katikati ya Mashariki ya Kati: "Akirithi ahadi hizi, akizifanya kuwa zake," kama inavyoonesha katika barua ya kitume aliyochapisha katika fursa hiyo: “unitate fidei,”- katika umoja wa imani,” Dk. Matteo Bruni alisisitiza. "Nchi mbili zilizojaa historia, zilizotembelewa na Mapapa wanne, na sasa mmoja wa tano umeongezwa."

Umoja wa Kikristo na ukaribu na vijana

"Zaidi ya yote, kuna mwelekeo wa kiekumeni katika ziara hii," alisema msemaji wa Vatican; Kisha kuna "ukaribu" na Wakristo wa madhehebu yote ambao "wanatambua" Mtaguso wa Nicea: "Historia changamano, ya kale, iliyoundwa na migawanyiko na majeraha, ya kuungana tena na mikasa  inayohusiana na matukio ya kihistoria." Pia kuonesha ukaribu wake na "jumuiya ndogo" za Wakatoliki, ambao baadhi yao "wanapitia nyakati ngumu katikati ya uhamiaji na mvutano." Na, kwa maana hiyo, safari hiyo pia itapewa kipaumbele kikubwa na Walebanon walio ughaibuni. Hotuba nyingi zitaelekezwa kwa Papa. Maneno ya matumaini katika Mwaka huu wa Jubilei; "maswali mengi kuhusu mustakabali" kutoka kwa vijana "katika wakati wa kushindwa katika ulimwengu wa watu wazima." Na vijana wa Lebanon, wakiwa wamelemewa na changamoto mbalimbali lakini wakiwa na uwezo mkubwa wa ustahimilivu na uvumilivu, Papa atapata moja ya nyakati muhimu zaidi na mkutano katika uwanja mbele ya Upatriaki wa Kimaronite ya Antiokia huko Bkerké.

Tukio huko Nicea

Miongoni mwa matukio muhimu, Dk Bruni alisisitiza, akielezea mpango huo, ni sherehe ya kiekumeni huko Nicea pamoja na Papa Leo XIV  na Patriaki wa Constantinople, Bartholomew I katika maandamano kando ya ziwa kuelekea magofu ya Basilika ya Mtakatifu Neophytos, iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi. Kisha kutakuwa na nyimbo na sala pamoja na mapatriaki wengine na wawakilishi wa makanisa ya Kikristo katika nusu duara mbele ya sanamu za Kristo na Baraza, na kuwashwa kwa mshumaa.        

Mazungumzo na Dini Nyingine

Mbali na umoja wa kidini, mazungumzo kati ya dini pia yatakuwa sehemu muhimu. Mnamo tarehe 27 Novemba 2025, Papa atatembelea Diyanet, Urais wa Masuala ya Kidini, mipango ambayo baadaye itaongezwa kwenye programu ya awali. Pia atakutana na Mkuu wa Kiyahudi wa  Uturuki na kukutana faraghani na viongozi wa Jumuiya  za Waislamu na Wadruze katika Baraza la Wawakilishi huko Beirut. Pia kuna nyakati nyingi za kukumbukwa kutoka kwa safari hii ya siku sita: Papa akiweka shada la maua chini ya safu iliyowekwa wakfu kwa Mkataba wa Kitaifa katika Kaburi la Atatürk, "katika kutafakari," chini ya maghala na vigae vya majolica vya "Msikiti wa Bluu," na miongoni mwa waamini 4,000 wanaotarajiwa kuudhuria Misa katika Uwanja wa Volkswagen wa Istanbul. Au Papa akipanda mwerezi katika bustani ya Jumba la Rais huko Beirut, akisali kwenye kaburi la tuff na jiwe la mtawa mponyaji Mtakatifu Charbel, au chini ya sanamu nyeupe na dhahabu ya shaba ya Mama Yetu wa Lebanon, ambayo inaonekana kuilinda Mashariki ya Kati yote.

Mkutano na waandishi wa habari

Papa Leo XIV atafanya ziara kadhaa katika gari la wazi katika nchi zote mbili. "Gari linalofaa zaidi litachaguliwa kulingana na hali," Dk Bruni alifafanua. Msafara wa Papa, pamoja na ujumbe wa kawaida, unajumuisha Makardinali Kurt Koch, Mwenyekiti  wa Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Umoja wa Wakristo; Kardinali George Koovakad, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini; na  Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki. Papa atazungumza kwa Kiingereza katika safari yote nchini Uturuki na kwa Kiingereza nchini Lebanon wakati wa mikutano rasmi, na kwa Kifaransa wakati wa sherehe za kiliturujia. Mkutano na waandishi wa habari ndani ya ndege ya Papa  Leo XIV kwa sasa umepangwa kwa ajili ya mkutano wa kawaida wa waandishi wa habari mwishoni mwa safari yake.

25 Novemba 2025, 16:42