2025.05.07 Ingresso in Conclave e il giuramento

Papa Leo atafanya Mkutano Mkuu Maalum wa Kwanza na Makardinali

Mkutano Mkuu Maalumu tafanyika tarehe 7 na 8 Januari 2026.Hii ilitangazwa na Ofisi ya Habari ya Vatican.Itakuwa siku mbili za maombi,tafakari,na kushiriki ili kutoa msaada na ushauri kwa Papa.

Vatican News

Mwaka mpya utaanza na roho ya ushirika, utambuzi, na kushiriki katika Kanisa, kufuatia kumalizika kwa Jubilei ya Matumaini kwa kufungwa kwa Mlango Mtakatifu katika Basilika ya Mtakatifu Petro mnamo  tarehe 6 Januari 2026. Papa Leo XIV, kama ilivyotangazwa Novemba iliyopita, atakutana kwa Mkutano Mkuu wa kwanza maalum wa upapa wake, mnamo tarehe 7 na 8 Januari 2026. Hii ilitangazwa na Ofisi ya Habari ya Vatican.

Katika taarifa hiyo inasomeka kuwa "Mkutano huo, utafanyika kwa siku mbili na utaoneshwa na nyakati za ushirika na udugu, pamoja na nyakati zilizotengwa kwa tafakari, kushiriki, na sala." Hakika, mikutano hii italenga "kukuza utambuzi wa pamoja na kutoa msaada na ushauri kwa Baba Mtakatifu katika kutekeleza jukumu lake kubwa na zito katika kutawala Kanisa la Ulimwengu." Mkutano Mkuu(Consistory) huo unalenga kuimarisha “ushirika kati ya Askofu wa Roma na makardinali, unaoitwa kushirikiana kwa njia maalum katika kujali mema ya Kanisa la ulimwengu.”

MKUTANO MKUU MAALUM

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here

20 Desemba 2025, 13:00