2025.12.04  Papa alikutana na  Khurelsukh Ukhnaa, Rais wa Mongolia 2025.12.04 Papa alikutana na Khurelsukh Ukhnaa, Rais wa Mongolia  (@VATICAN MEDIA)

Papa akutana na Rais wa Mongolia

Papa alikutana na Rais Ukhnaagiin Khürelsükh wa Jamhuri ya Mongolia mjini Vatican,Desemba 4.Katika Majadiliano katika Sekretarieti ya Vaticanyalilenga ushirikiano wa kiutamaduni na mchango wa Kanisa kwa nchi, katika huduma ya afya na elimu.

 Vatican

Tarehe 4 Desemba 2025, Papa Leo XIV alimpokea Rais wa Mongolia, Ukhnaagiin Khürelsükh, katika Jumba la Kitume la Vatican. Baadaye Khürelsükh alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na, na Monsinyo  Mihăiță Blaj, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa.

Mchango wa Kanisa kwa Huduma ya Afya na Elimu

Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Jimbo, taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican inasema, "uhusiano mzuri kati ya Vatican na Mongolia ulijadiliwa, kwa nia ya kuuendeleza pia katika nyanja ya kitamaduni. Mchango chanya ambao Kanisa Katoliki la eneo hilo hutoa kwa jamii ya Mongolia, hasa katika nyanja za elimu na huduma ya afya, pia uliangaziwa."

04 Desemba 2025, 15:47