Umoja wa Mama Wakuu wa mashirika kimataifa (UISG)unatimiza miaka 60. Umoja wa Mama Wakuu wa mashirika kimataifa (UISG)unatimiza miaka 60.  (© Uisg)

Papa kwa UISG:kuwa mashuhuda wa Injili katika Mipaka ya Dunia!

Katika barua iliyotumwa wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Kimataifa wa Wakuu Mashirika ya Kitawa(UISG),Papa Leo XIV anawahimiza watawa kuwa"mahujaji na wanafunzi wa kimisionari wa matumaini" ili kuponya majeraha ya wale wanaokutana nao.

Vatican News

Papa Leo XIV alirejea "maono ya Mtakatifu Paulo VI," ambaye alihimiza upya maisha ya wakfu katika ulimwengu wa kisasa baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatican. Papa alimtaja Papa Montini katika barua yake, iliyoandikwa tarehe 26 Novemba 2025, kwa Sista Oonah O'Shea, rais wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa katika fursa ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Umoha huo( UISG) mnamo tarehe 8  Desemba 1965.

"Ninashirikishi nanyi katika kutoa  shukrani kwa njia nyingi ambazo UISG imetekeleza utume huu kwa uaminifu na ujasiri," aliandika Papa, huku akikumbuka jinsi, ambavyo katika kipindi cha miaka 60 ya uwepo wake, Umoja huo umekuza nafasi ya mazungumzo kati ya Wakuu kutoka mabara sita, wakishirikishana "utajiri wa karama zao" na vipaji vya Roho Mtakatifu "kwa ajili ya mema ya Kanisa na Ulimwengu."

Wanafunzi Wamisionari wa Matumaini

Papa  Leo katika barua hiyo alisisitiza kwamba wakati huu una sifa ya "mabadiliko ya haraka na mahitaji ya haraka," hivyo kujitolea kwa wanawake wa kitawa katika uwanja wa ushirikiano na utume katika mipaka kunakuwa "ushuhuda wenye nguvu wa Injili. Katika ukweli kwamba maadhimisho haya yanaambatana na Mwaka wa Jubilei ya Matumaini," aliongeza Papa Leo XIV, "ni neema maalum." Kwa hivyo tumaini kwamba katika "wakati huu mtakatifu, wito wa kuwa mahujaji na wanafunzi wa kimisionari wa matumaini utafanywa upya: wanawake ambao, wakiwa wamejikita katika utakaso na kuongozwa na Roho, husaidia "kufufua uaminifu, kuponya majeraha, na kusindikizana na watu wa Mungu kwa huruma na uvumilivu wa furaha." Hatimaye, anakabidhi kwa Maria, "Mama wa Kanisa na kielelezo cha ufuasi mwaminifu."

Mustakabali Utakaoandikwa

"Leo tunasherehekea historia katika mageuzi ya mara kwa mara, yanayotarajiwa kuelekea mustakabali na yaliyo wazi kwa upeo mpya," alisema Sr Oonah O'Shea,  Rais wa UISG katika taarifa yake akitangaza utengenezaji wa makala kuhusu: "Maisha Yaliyowekwa Wakfu, Tumaini linalobadilisha," ambayo inaakisi kujitolea kwa watawa katika pembezoni mwa dunia na maisha. Historia inaonesha uwepo wao pamoja na wahamiaji na wakimbizi, inaandika mapambano yao dhidi ya biashara haramu ya binadamu, ulinzi wao wa hadhi ya binadamu, na kujitolea kwao kulinda uumbaji.

16 Desemba 2025, 17:12