Papa Leo XIV akutana na Waziri Mkuu wa Malta
Vatican News.
Papa Leo XIV Jumatatu tarehe 15 Desemba 2025 alikutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Malta, Bwana Robert Abela, ambapo mara baada ya mkutano huo alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican imebaininisha kuwa “Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mzuri wa pande mbili na ushirikiano wenye matunda kati ya Vatican na Serikali ya Malta ulisisitizwa.”
Kadhalika “Masuala ya maslahi ya pande zote, kama vile uhamiaji pia yalijadiliwa, mada ambayo Vatican na Serikali ya Malta wamejitolea sana. Mazungumzo yaliendelea, kwa kuzingatia hasa hali ya Ulaya na kimataifa, kwa kuzingatia hasa Ukraine na Mashariki ya Kati.”
