Papa Leo XIV asali katika Kaburi la Mt.Charbel:Hakuna Amani bila Wongofu wa Mioyo

Papa Leo XIV alianza siku yake ya pili ya ziara ya Kitume kwenda huko Beirut kwa kufanya hija kwenye monasteri ya Annaya,ambapo alisali kwenye pango linalotunza mabaki ya mtawa:"Watangulizi wangu wangetamani sana."Kutoka mahali hapa ambapo mto wa huruma unapitia,Papa aliomba amani ya dunia.Amani,huzaliwa tu kutokana na uongofu wa mioyo na hivyo Mtakatifu Charbel alinde Lebanon na watu wake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 1 Desemba 2025, ikiwa ni siku yake ya  pili kuwa Nchini Lebanon, katika Ziara yake ya Kwanza ya Kitume, alitembelea Kaburi la Mtakatifu Charbel Annaya, katika Monasteri ya Mtakatifu Maroun. Akiwa katika eneo hilo la kaburi, Papa  akia ndani ya Pango hilo alianza kumshukuru Mkuu wa Shirika kwa maneno yake na kwa makaribisho katika monasteri ya Annaya.  Papa alisema kuwa hata kwa asili ambayo inazungukia nyumba ya sala inavutia na uzuri wake mkali. Papa alimshukuru Mungu ambaye amemwezesha kufika kama mhujaji katika kaburi Mtakatifu Charbel. Kwa watangulizi wake, hasa alimkumbuka Mtakatifu Paulo VI ambaye alimtangaza kuwa mwenyeheri na kuwa Mtakatifu ambaye angetamani kuwa mahali hapo.  Papa Leo XIV aliuliza swali kwamba ni kitu gani anatufundisha leo hii Mtakatifu Charbel? 

Ndani ya Pangopenye kaburi la Mtakatifu Charbel
Ndani ya Pangopenye kaburi la Mtakatifu Charbel   (@Vatican Media)

Ni urithi gani wa mwanaume huyo ambaye hakuandika chochote, na ambaye akiishi amejificha na kunyamaza, lakini akawa maarufu na kuenea katika Ulimwengu wote? Papa alipenda kufupisha kwa namna hii: Roho Mtakatifu alimfunda, kwa sababu anayeishi bila Mungu amfundishe kusali, anayeishi kwa kelele amfundishe ukimya, anayeishi kwa kutaka kujionesha amfundishe kiasi, anayeishi akitafuta utajiri amfundishe umasikini. Hizi zote ni tabia dhidi ya tabia za kisasa, lakini zaidi,  kwa njia hiyosisi tunavutiwa kama maji ya baridi na masafi yanayotiririka katika jangwa.

Kwa namna ya pekee, kwetu sisi maaskofu na wahudumu waliowekwa wakfu, Mtakatifu Charbel anatukumbusha mahitaji ya kiinjili ya wito wetu. Lakini msimamo wake, wenye msimamo mkali na unyenyekevu, ni ujumbe kwa Wakristo wote. Na kisha kuna jambo lingine muhimu: Mtakatifu Charbel hakuacha kutuombea kwa Baba wa Mbinguni, chanzo cha mema na neema yote. Tayari wakati wa maisha yake duniani, wengi walimwendea ili kupokea faraja, msamaha, na ushauri kutoka kwa Bwana. Baada ya kifo chake, haya yote yaliongezeka na kuwa kama mto wa rehema. Kwa sababu hiyo, pia, kila tarehe 22 ya mwezi, maelfu ya mahujaji huja hapa kutoka nchi mbalimbali kutumia siku ya maombi na burudisho la mwili na roho.

Papa akizungumza na watawa wa Monasteri hiyo
Papa akizungumza na watawa wa Monasteri hiyo   (@Vatican Media)

Papa leo XIV aliendelea kusema kuwa “ leo tunataka kumkabidhi Mtakatifu Charbel mahitaji ya Kanisa, Lebanon, na ulimwengu kwa maombezi yake. Kwa Kanisa, tunaomba ushirika na umoja: kuanzia na familia, makanisa madogo ya nyumbani, na kisha katika jumuiya za parokia na majimbo, hadi Kanisa la ulimwengu wote. Ushirika na umoja. Na tunaomba amani duniani kote. Tunaiombea hasa Lebanon na Mashariki ya Kati nzima. Lakini tunajua vizuri, na watakatifu wanatukumbusha, kwamba hakuna amani bila uongofu wa mioyo. Kwa hivyo, Mtakatifu Charbel atusaidie kumgeukia Mungu na kuomba zawadi ya uongofu kwa ajili yetu sote.

Sala mbele ya Kaburi la Mtakatifu Charbel
Sala mbele ya Kaburi la Mtakatifu Charbel   (@Vatican Media)

Papa Leo kwa kuhitimisha alisema kuwa "kama ishara ya nuru ambayo Mungu ameiwasha hapa kupitia Mtakatifu Charbel, nimeleta zawadi ya taa. Kwa kutoa taa hii, ninaikabidhi Lebanon na watu wake kwa ulinzi wa Mtakatifu Charbel, ili waweze kutembea katika nuru ya Kristo kila wakati." Tushukuru Mungu kwa zawadi ya Mtakatifu Charbel! Asante, mnaothamini kumbukumbu yake. Tembeeni katika nuru ya Bwana!"

Kuhusu Monasteri ya Annaya: Katika pango hilo la mawe, lililolindwa na ukuta wa kioo na kuangazwa na mwanga hafifu unaoelekeza kwenye kaburi jembamba la mwerezi, kuna mabaki ya  Mtakatifu Charbel Makluf, mtawa anayechukuliwa kuwa mtakatifu msimamizi wa nchi hiyo. Alitangazwa kuwa mtakatifu na Paulo VI mwaka 1977 na anasifiwa kwa miujiza zaidi ya 29,000 ya uponyaji, mingi kupitia mafuta ambayo tamaduni inasema ilianza kutiririka kutoka mwilini mwake mara tu baada ya kifo chake.

Papa  Leo XIV ndani ya Pango
Papa Leo XIV ndani ya Pango   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV, katika siku yake ya pili katika Nchi ya Mierezi, alisafiri zaidi ya kilomita 40 kutoka Beirut na kupanda hadi urefu wa takriban mita 1,200 ili kufikia mahali hapa ambapo, kama alivyosema, "mto wa rehema" unatiririka, na kuweka taa "ishara ya mwanga ambao Mungu ameuwasha hapa kupitia Mtakatifu Charbel."

 

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

01 Desemba 2025, 10:53