Papa Leo XIV,Hospitali ya wagonjwa wa Akili ya Beirut:Tusiwasahau maskini

Papa Leo XIV alitembelea Hospitali ya De La Croix,inayohudumiwa na Masista wa Wafransiskani wa Msalaba wakiwa na wagonjwa 800 wenye ulemavu wa akili na magonjwa ya akili kila siku.Papa alikaribishwa kwa uchangamfu,akipokea zaidi ya rozari 70 zilizotengenezwa kwa mikono ya baadhi ya wagonjwa.Papa alisema kuwa wao wako moyoni mwake

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV akifungua siku yake ya tatu nchini Lebanon na siku ya mwisho ya Ziara yake ya Kitume, Jumanne tarehe 2 Desemba 2025 alikwenda kutembelea Hospitali ya La Croix huko Jal Ed Dib, mojawapo ya hospitali kubwa zaidi za watu wenye ulemavu wa akili Mashariki ya Kati ambayo ina idadi ya wapatao 800.  Hospitali hii ilianzishwa mwaka 1919 na Padre  Jacques Haddad, na ilibadilishwa kuwa hospitali ya magonjwa ya akili mwaka 1937 na baadaye kuwa hospitali ya watu wenye ulemavu wa akili mwaka 1951. Hawa ni waanaume, wanawake, wazee, vijana, baadhi yao wakiwa wanajaribu kuondokana na madawa za kulevya ambapo(moja ya mabanda matano yametengwa kwa ajili yao), wote walimkaribisha Papa wakiwa na mitandio yao meupe iliyoandikwa nembo ya Papa na uso wa Padre Yaaqoub, na bendera za Lebanon na Vatican.

Katika Hospitali ya De la Croix
Katika Hospitali ya De la Croix   (@Vatican Media)

Papa akianza hotuba yake alitoa salamu za asubuhi kwa wote hata kwa lugha yao Ṣabāḥ al-khayr  baadaye akatoa shukrani kwa makaribisho yao akisema neno kwa kiarabu Shukrán. Papa alionesha furaha kuwa hapo pamoja nao. Papa alisema alivyotaka kufika hapo “kwa sababu Yesu anakaa mahali hapa: ndani yenu mlio wagonjwa, na ndani yenu mnaowatunza wagonjwa,  Masista,madaktari, wafanyakazi wote wa afya na wafanyakazi.” “Zaidi ya yote, ningependa kuwasalimu kwa uchangamfu na kuwahakikishia kwamba mko moyoni mwangu na katika maombi yangu. Asante kwa wimbo mzuri mliouimba! Asante kwa kwaya na watunzi: ni ujumbe wa matumaini kweli!” Hospitali hii ilianzishwa na Baba Mtakatifu Jacques, mtume asiyechoka wa hisani ambaye anakumbukwa kwa utakatifu wa maisha aliouonyesha hasa kupitia upendo wake kwa maskini na wanaoteseka."

Hospitali ya De la Croix
Hospitali ya De la Croix   (@Vatican Media)

Masista Wafransiskani wa Msalaba, ambao waliwaanzisha, wanaendelea na utume huo  na kutekeleza huduma muhimu sana. Asanteni, Masista wapendwa, kwa kazi mnayofanya kwa furaha na kujitolea sana!” Pia Papa alipenda kuwasalimu wafanyakazi wote wa hospitali kwa shukrani za dhati. “Uwepo wenu wenye ujuzi na huruma na utunzaji wenu kwa wagonjwa, ni ishara inayoonekana ya upendo wa rehema wa Kristo. Ninyi ni kama Msamaria Mwema, anayesimama kando ya mtu aliyejeruhiwa na kumtunza, akimwinua na kumtunza majeraha yake.” “Wakati mwingine, unaweza kupata uchovu au kukata tamaa, hasa kutokana na hali ngumu ambazo mara nyingi hufanya kazi." Kwa njia hiyo Papa alisema "Ninawatia moyo msipoteze furaha ya utume huu. Licha ya magumu, wekeni mbele ya macho yenu mema mnayoweza kuyatimiza. Machoni pa Mungu, ni kazi nzuri! Mnachoishi mahali hapa kinasimama kama ukumbusho wazi kwa wote - kwa nchi yenu, lakini pia kwa familia nzima ya wanadamu. Hatuwezi kuwasahau wale walio dhaifu zaidi. Hatuwezi kufikiria jamii inayosonga mbele kwa kasi kamili ikishikilia historia za uwongo za ustawi, huku wakati huo huo ikipuuza hali nyingi za umaskini na udhaifu.”

Hospitali ya De La Croix
Hospitali ya De La Croix   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisema kuwa "kama Wakristo, hasa kama Kanisa la Bwana Yesu, tumeitwa kuwatunza maskini. Injili yenyewe inatutaka hili, na hatupaswi kusahau kwamba kilio cha maskini, kinachosikika katika Maandiko yote, kinatupatia changamoto."  “Katika nyuso zilizojeruhiwa za maskini, tunaona mateso ya wasio na hatia na, kwa hivyo, mateso ya Kristo mwenyewe” (Wosia wa Kitume ya Leo XIV Dilexi Te, 9). Papa aliwaeleza kaka na dawa waliolemewa na magonjwa, kwa “ningependa kuwakumbusha kwamba mko karibu na moyo wa Mungu Baba yetu.  Anawashika mkononi mwake; anawasindikiza kwa upendo; na anawapa huruma yake kupitia mikono na tabasamu za wale wanaowajali.” Kwa kila mmoja wenu, Bwana alisema tena leo: Papa aliwaeleza kuwa “Ninawapenda, ninawajali, ninyi ni watoto wangu. Msisahau hili kamwe. Asanteni nyote. Shukrán! Allah ma‘akum (Asante, na Mungu awe pamoja nanyi)!”

Papa alitembelea Hospitali ya De la Croix
Papa alitembelea Hospitali ya De la Croix   (@Vatican Media)
Hospitali ya De la croix
Hospitali ya De la croix   (@Vatican Media)
02 Desemba 2025, 10:44