Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Katekesi ya tarehe 10 Desemba 2025. Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Katekesi ya tarehe 10 Desemba 2025.  (@Vatican Media)

Papa:"Wakati wa Noeli,tuepuke kununua vitu kwa nguvu nyingi;tuwaalike maskini au wapweke"

Papa Leo XIV alijibu katika kurasa za jarida la "Piazza San Pietro"kwa mwanasaikolojia anayesimulia uzoefu wake wa kufanya kazi na vijana na familia katika wakati wa misukosuko,hofu,ukosefu wa usalama na upweke.Papa alitualika katika kipindi cha Noeli kiwe muafaka na kuishi upendo halisi na alitoa mfano wa Mtakatifu John Henry Newman,ambaye anaweza "kusaidia kupambana na giza la ubatili"na kujengaustaarabu wa kweli wa amani."

Vatican News

Katika Toleo jipya la jarida “la Piazza San Pietro,” yaani “Uwanja wa Mtakatifu Petro” lililohaririwa na Padre Enzo Fortunato, limetengwa kwa ajili ya kipindi cha  Noeli kama wakati wa kusikiliza, kukaribisha, na kujali. Toleo hili maalum limetengwa kwa ajili ya Usiku Mtakatifu duniani kote, Noeli iwe ya kutoa na kutumia, bila kuwasahau maskini, na mada ya Amani na kwamba  Mungu Hataki Vita na Vurugu." Hili ni Jarida la kila mwezi linaloanza kwa barua kwa Papa Leo XIV huku akimjibu Antony, mwanasaikolojia wa miaka arobaini kutoka Pagani, katika jimbo la Salerno nchini Italia, na ikiwa ni majibu ya Papa Leo XIV katika Noeli yake ya kwanza akiwa katika Mtumbwi wa Mtume Petro.

Antony anasimulia maisha aliyoishi pamoja na walio hatarini zaidi, akiongozwa na Mtakatifu Alphonsi Maria de' Liguori na Mtakatifu Francis wa Assisi. Na alifanya hivyo kwa kushirikishana na Papa ahadi yake ya kila siku kwa vijana na familia, katikati ya "msukosuko, hofu, na utafutaji wa kupindukia wa kutambuliwa" ambao mara nyingi huficha ukosefu wa usalama na upweke. Kwa upande wake anaona wakati ambapo "kukosea ni uhalifu na kushindwa ni kushindwa kabisa," lakini pia kijana mwenye kiu ya Mungu, "hitaji la wale wanaoamini, tumaini kwa wale wasioamini." Katika hali hii ya uchovu ulioenea, Antony anatambua katika babu na bibi yake "sifa ya kutokamilika" na anawakumbusha kila mtu "zawadi isiyopimika ya upekee wetu." Kwa hivyo ombi lake kwa Papa kwa neno ambalo linaweza "kugusa mioyo" wa vijana wengi anaowasindikiza.

Jibu la Papa

Katika jibu lake, Papa Leo XIV alizungumzia mada kuu tatu za Noeli. Kwanza, alikumbuka umuhimu wa ushuhuda wa Kikristo kama njia ya vijana kukutana na Kristo: ushuhuda rahisi, wa kweli, uliokomaa katika sala, maisha ya kijamii, na ufahamu wa "kupendwa na Mungu kila wakati." Kisha Papa alitoa mwaliko ili kwa wote  kuwa na wakati mzuri wa Noeli  kama wakati wa viburudisho rahisi lakini pia kwa ajili ya hali halisi katika upendo: "Tuepuke kununua vitu vingi," anaandika, ambavyo hubadilisha zawadi kuwa vitu vya matamanio badala ya kufanya ishara za uzuri na matumaini.” Na alipendekeza ishara inayoweza kurejesha maana ya kipindi cha mapumziko la Noeli kuwa: "Tualike familia maskini au hata mtu mmoja tu kwenye chakula chetu cha jioni cha Noeli.”  Kwa upande wa Papa, “umaskini wa kimwili na wa kuwepo halisi, unabaki kuwa "jambo la dharura ambalo haliwezi kuahirishwa," kama ilivyokumbukwa pia katika Wosia wake wa  Kitume wa “ Dilexi te.”

Mfano wa Newman

Hatimaye, Papa Leo XIV aliwaelekeza vijana kwenye mwanga wa mfano wa Mtakatifu John Henry Newman, ambaye hivi karibuni alitangazwa kuwa Mwalimu  wa Kanisa. Papa alithibitisha kuwa, “mtaalamu wa mazungumzo na elimu, anaweza kusaidia kupambana na giza la ubatili na kujenga ustaarabu wa kweli wa amani.”  Papa anamalizia kwa kumhakikishia  Anthony kuhusu maombi yake, huku akimtia moyo asikatishwe tamaa katika utume wake kwa vijana, na aliwatakia Noeli  Njema wasomaji wote wa jarida la “Piazza San Pietro.” Jarida la toleo la Mwezi Desemba la “Piazza San Pietro” yaani Uwanja wa Mtakatifu Petro pia  limejitolea kwa ajili ya watoto na mawazo ya Papa Leo XIV kwa ajili yao, kufuatia tangazo, la  mwezi Novemba 19 iliyopita, la Siku ya Pili ya Watoto Duniani, iliyopangwa kufanyika Roma kuanzia  tarehe 25-27 Septemba 2026.

15 Desemba 2025, 16:10