Desemba 8 Papa Leo XIV ataheshimu Mama Maria Mkingiwa dhambi Asili
Vatican News
Tamaduni na ibada zinaungana katika kuheshimu Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili (Immacolate) wakati wa sherehe hiyo inayoadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Desemba 2025. Kwa njia hiyo Jiji la Roma na mashirika mbalimbali yatasali na kuweka maua kwenye sanamu ya Bikira Maria huko Uwanja wa Mignanelli, ambapo Papa Leo XIV pia atafanya tendo la kiutamaduni la ibada chini ya Miguu ya sanamu ya Maria na kuweka shada la maua. Mwaka ulipitia tarehe 8 Desemba 2024, Papa Francisko alisali miguuni pa Maria na kumkabidhi Jubilei iliyokuwa ifunguliwe katika mkesha wa Kuzaliwa kwa Bwana na, "ujumbe wa matumaini kwa wanadamu uliojaribiwa na migogoro na vita." Kwa hivyo Papa Leo XIV anarudi tena kwa Mama kabla ya kumalizika kwa Mwaka Mtakatifu.
Kuwasili kwa Papa Leo XIV
Katika taarifa, kutoka Vikariate ya Roma ilitangaza kwamba, kulingana na utamaduni, wa kwanza kuweka maua kwenye sanamu ya Bikira Maria watakuwa wazima moto, kwa heshima ya wenzao 220 waliozindua kazi hiyo mnamo tarehe 8 Desemba 1857.
Saa 1:00 asubuhi watapanda juu kuweka shada la maua kwenye mkono wa Bikira Maria. Alasiri, saa 10:00 jioni, Papa atawasili na kukaribishwa na Makamu wa Papa Kardinali Baldo Reina na Meya wa Jiji la Roma Roberto Gualtieri. Atasimama kwa sala chini ya kinara chenye urefu wa mita 12, ambacho juu yake imesimama sanamu ya Mamam, na ataacha taji la maua.
Siku hiyo itaakisi mfululizo wa matukio: saa 2:30 asubuhi, Bendi ya Kikosi cha Ulinzi cha Vatican kitatumbuiza wimbo kwa Maria kisha, parokia ya Mtakatifu Andrea delle Fratte, Shirika la Kijeshi la Malta, Legio Mariae, Udugu wa Mtakatifu Pietro, Chama cha mfuko wa Don Gnocchi, UNITALSI, na shule kadhaa zitaimba.
Saa 9 alasiri Misa itaadhimishwa katika Kanisa la Trinità dei Monti, ikiongozwa na Askofu Francesco Pesce, mwakilishi wa Jimbo wa huduma za kijamii na kichungaji cha wafanyakazi, huku wafanyakazi kutoka makampuni kadhaa ya Roma wakihudhuria.
Novena kwa Maria
Watawa wa Konventuali wa Mtakatifu Francisko wa Kanisa Kuu la Mitume Kumi na Wawili wataongoza siku hiyo. Miongoni mwa mambo mengine, kanisa litaandaa novena ya zamani zaidi ya Kuchukuliwa Mimba Takatifu huko Roma: Kuanzia Novemba 29 hadi Desemba 7, kila siku saa 11:45 jioni, wanasali Rozari na litania kisha, saa 12:30 jioni, kuna misa kwa kuimba "Tota Pulchra," iliyotungwa na Ndugu Alessandro Borroni Mkonventuali katika Kanisa Kuu la Mashahidi kumi na wawili.
Misa zinazoadhimishwa na Makardinali
Kuanzia tarehe 3 Desemba 2025, Misa katika Kanisa kuu la Mitume Kumi na Wawili itaongozwa na Kardinali Angel Fernandez Artime, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Maisha ya Kitume.
Siku ya Alhamisi, tarehe 4 Desmba, Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki;
Siku ya Ijumaa, Desemba 5, Kardinali Rolandas Makrickas, Mkuu wa Kanisa Kuu la Kipapa Mtakatifu Maria Mkuu.
Jumamosi tarehe 6 Desemba, Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu ataongoza misa;
Dominika tarehe 7 Desemba, Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na hatimaye Jumatatu tarehe 8 Desemba, sherehe kuu ya Ekaristi takatifu itaongozwa na Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa Makanisa ya Mashariki.
Asante kwa kusoma makala haya. Ili kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.
