Papa Leo XIV kwa Jumuiya ya Wasalesiani:Endeleeni na huduma yenu katika umaskini na vita
Edoardo Giribaldi – Roma na Angella rwezaula - Vatican.
Nilipokuwa kijana, kabla ya kujiunga na Waagostiniani, pia nilitembelea Jumuiya ya Wasalesiani. Mlikuja katika nafasi ya pili, Samahani! Papa Leo XIV, ndivyo alianza kwa kukiri kuhusu wito wake huku akipokelewa kwa kicheko, kwa wanashirika wa jumuiya iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Bosco, waliyokabidhiwa Basilika ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Castro Pretorio, Roma.
Papa Leo XIV akikutana na wanashirika hao mara baada ya misa aliwapongeza kuwa:"Kiukweli ninyi mnaonesha wasiwasi mkubwa na wa pamoja kuhusu ukaribu, katika sehemu mbalimbali za dunia, pale ambapo kuna vita, pale ambapo kuna migogoro, pale ambapo kuna umaskini, na pale ambapo Yesu anataka kuwepo. Ukaribu wa Kristo na Kanisa ambao pia unaoneshwa katika mitaa ya Roma, katika "moyo wake," kupitia shughuli za mshikamano zinazoendelezwa na Baraza la Wachungaji la Parokia."
Kwa njia hiyo hizi zilikuwa nyakati mbili zilizohitimisha ziara ya kichungaji ya Papa Leo XIV, Dominika tarehe 22 Februari 2026 katika Kanisa lililo la Moyo Mtakatifu wa Yesu umbali mfupi wa kutembea kutoka kituo cha treni cha Termini, mbele ya Kardinali Baldo Reina, Makamu wake wa Jimbo Kuu la Roma na watawa hao kwanza na baadaye Baraza la Kichungaji.
![]()
Papa Leo akutana na Jumuiya ya Wasalesiani (@Vatican Media)
usaidizi wa "wadogo wa Ufalme"
Historia ambayo Papa Leo XIV alishirikisha kuhusu kushindwa kwake kujiunga na Shirika la Wasalesiani kuliakisi utambuzi wa ukaribu na utajiri wa karama ambazo Papa Leo XIV anatambua vema katika familia ya Don Bosco ya: "huduma hii kwa vijana, upendo huu kwa huduma ya elimu, maeneo mengi ambayo wao wanatoa huduma katika nchi nyingi ulimwenguni kote."
Papa anaendelea kuelezea fursa ya kusherehekea imani yetu ya pamoja kama "kubwa," ya kuhisi ukaribu na "mdogo wa Ufalme," ambao katika Castro Pretorio kunaoneshwa kwa vijana, si Waitaliani pekee, ambao wanaweza kupata huduma kama vile shule ya lugha ya Kiitaliano. Kisha Papa alitania tena: "Mapema nilimwambia profesa kwamba mimi pia ningekuwa sehemu ya madarasa yake ya Kiitaliano, ambayo yanaweza kunisaidia kila wakati!"
"Moyo" wa Yesu na wa Jiji
Papa Leo XIV mara baada ya kukutana na wanashirika hao wa Kisalesiani, sehemu ya pili ilikuwa ni ile ya kujumuika na Baraza la Kichungaji la Moyo Mtakatifu. Baada ya kuomba wampigie makofi Paroko wa Parokia, Padre Javier Ortiz Rodriguez, Papa alisisitiza jinsi ambavyo Kanisa hilo linavyowakilisha "nyumba" kwa sababu ya "mto wa mahujaji wanaopita Termini kila siku." "Moyo wa jiji na "Moyo wa Yesu" vinaungana" alisema. Kwa hivyo alirudia maneno yale yale yaliyotumiwa na Padre wakati wa maneno yake mwishoni mwa misa akisisitiza kuwa: "Ni vizuri sana kupata uzoefu wa roho hii si tu ya moyo wa jiji, bali ya moyo wa Yesu, ambao daima umejaa upendo na huruma. Huruma inayojidhihirisha katika huduma nyingi, aina nyingi za upendo, za ukaribishaji, za kusindikiza, za ukaribu wa Kristo, na za ukaribu wa Kanisa kwa watu hawa wote."
![]()
Papa Lei akutana na Baraza la Kichungaji (@Vatican Media)
"Kutembea wote pamoja"
Katika matarajio ya kukutana tena nao katika siku zijazo, Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba Baraza la Wachungaji, jumuiya ya kielimu-kichungaji katika roho ya Wasalesiani, ina asili ya "kisinodi", katika maana yake ya asili ya "kutembea pamoja." Na kwa hivyo ninyi, mnaowakilisha sekta nyingi, jumuiya nyingi, hali halisi nyingi za parokia hii, mliokusanyika hapa pamoja, mkifanya kazi pamoja, pia mnawakilisha mwelekeo huu mzuri wa maisha ya kikanisa. Asante kwa yote mnayofanya," aliwashukuru Papa.
![]()
Papa akutana Baraza la Kichungaji (@Vatican Media)
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
