Wijeti mpya ya video yenye habari mpya ya Papa kwa ajili ya mitandao ya Kikatoliki
Vatican News
"Ndugu mpendwa, mpango huu wa Vatican News ni chombo cha uinjilishaji; unatoa fursa ya kuunganisha na kubadilishana zawadi kati ya Roma na Kanisa katika nchi yako. Ni njia kwa parokia na jumuiya zako kupata taarifa kila mara kutoka chanzo kikuu."
Haya ndiyo maandishi ambayo Papa Leo XIV aliandika katika ujumbe kwa Maaskofu wa duniani kote, akiwaalika kushiriki (Widget) Wijeti mpya ya video na habari za Vatican News, chombo kitakachoruhusu kurasa za Tovuti za majimbo, parokia, na vyama na mashirika ya Kikatoliki kupokea video na habari za bure kuhusu Papa na Vatican. Kwa njia hiyo, wale wanaotembelea kurasa za tovuti za majimbo au parokia kupitia kompyuta, Ipad, au simu za mikononi watasasishwa kila mara na habari mpya kuhusu mafundisho na shughuli za Askofu wa Roma na wataweza kushirikisha maudhui ya mitandao ya kijamii kuhusu Papa katika lugha yao wenyewe.
"Itakuwa muhimu kwa kifaa cha video kusambazwa sana kwenye tovuti nyingi iwezekanavyo, ili kusisitiza uhusiano na Askofu wa Roma," alisema Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk. Paolo Ruffini, "na pia kwa sababu ni kifaa muhimu kwa uinjilishaji."
"Usambazaji wa kifaa hiki kipya," alisema mkurugenzi Mkuu wa uhariri wa vyombo vya habari vya Vatican, Dk Andrea Tornielli, " unaweza kusaidia kupambana na hali ya habari za uongo kwa kutoa ufikiaji wa haraka kutoka chanzo asili cha habari na maandishi, kama Baba Mtakatifu alivyosisitiza katika barua yake inayounga mkono mpango huu mpya."
Unaweza kupakua Wijeti kwenye tovuti yoyote kwa kunakili na kubandika msimbo. Ili kuitengeneza katika lugha uliyochagua na kwa ukubwa unaotaka (mpangilio wa mlalo au wima unawezekana, na pia unaweza kuchagua fonti ya maandishi), inatosha kwenda kwenye link hii:https://www.vaticannews.va/widget/embed.html
Baada ya kuingiza vipimo vyote vinavyohitajika, msimbo mpya maalum utatengenezwa ili unakili kwa ajili ya kupachikwa. Hii ni operesheni ya mara moja kwa msimamizi wa tovuti: wijeti ya video itasasishwa kiotomatiki bila kuingilia kati zaidi. Hii itakuruhusu kupokea video fupi zinazoweza kushirikishwa kwa wakati halisi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Papa na Vatican, katika miundo ya mlalo na wima; "reel" yenye habari zinazotolewa mara moja za Vatican News, katika lugha iliyochaguliwa; kiungo cha moja kwa moja kwenye kurasa husika za Vatican.va, ambapo maandishi kamili ya Papa yatapatikana kila wakati. Wijeti hii pia itajumuisha viungo vya moja kwa moja katika Gazeti la Osservatore Romano na Radio Vatican.
NB: Sifa na Matumizi ya Wijeti ni ufikiaji wa Haraka wa habari yoyote kuanzia taarifa mbali mbali, saa, hali ya hewa na mengine mengi...
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
