2026.03.30 Papa akutana na Wanachamawa Mfuko wa Ausilia 2026.03.30 Papa akutana na Wanachamawa Mfuko wa Ausilia  (@VATICAN MEDIA)

PapaLeo XIV:"Vijana ni wahusika wakuu wa mstakabali wao wenyewe"

Jumatatu Machi 30,akipokea wanachama wa Mfuko wa Ausilia,unaowasaidia vijana na kukuza maendeleo ya kijamii,Baba Mtakatifu Leo XIV alihimiza uwekezaji kwa watu katika nyakati hizi zisizo na uhakika.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 30 Machi 2026, alikutana na wanachama wa Mfuko wa Ausilia, mjini Vatican, Mfuko ambao unajihusisha na kuwasaidia vijana,  ambapo katika hotuba yake aliwakaribisha akisema: “mwanzo wa Juma Takatifu,  kipindi cha majaliwa ya Mungu kwa ajili ya kumfuata Bwana Yesu, aliyesulubiwa, akafa  na kufufuka kwa ajili yetu.” Papa Leo XIV aliwashukuru “kwa kujitolea kwao kwa ukarimu kuwasaidia vijana katika njia zao za elimu na kazi.”

Papa alikutana na wanachama wa Mfuko wa Ausilia
Papa alikutana na wanachama wa Mfuko wa Ausilia   (@Vatican Media)

Kuwekeza si katika vitu, bali kwa watu

Papa Leo XIV  alisisitiza kwamba: “Kuwekeza si katika vitu, bali kwa watu, katika ujuzi na uwezo wao, ni nguvu ya kazi yao.” Kwa hiyo vijana wenyewe “wanakuwa wahusika wakuu wa mustakabali wao wenyewe, badala ya kuchukuliwa kama zana tu katika kupanga kampuni au katika mafanikio yake ya kibiashara.”

Papa alikutana na wanachama wa Mfuko wa Ausilia
Papa alikutana na wanachama wa Mfuko wa Ausilia   (@VATICAN MEDIA)

Mzunguko mzuri wa maarifa na ushirikiano

Baba Mtakatifu kadhalika,  aliwahimiza  mwanachama  hao wa Mfuko wa Ausilia, “kuendelea katika mipango wanayohamasisha: hasa katika hali ya sasa ya kutokuwa na uhakika, mzunguko mzuri wa maarifa na ushirikiano wanaohamasisha, kwa  hakika utatoa matunda.”  Kama ishara ya heshima yake. Papa  alifurahi kuwapatia Baraka yake ya Kitume wote waliokuwapo hapo na wapendwa wao.”

PAPA NA MFUKO WA VIJANA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

30 Machi 2026, 12:57