Ratiba ya Maadhimisho ya Baba Mtakatifu kuanzia Aprili hadi Julai 2026. Ratiba ya Maadhimisho ya Baba Mtakatifu kuanzia Aprili hadi Julai 2026.  (@VATICAN MEDIA)

Ratiba ya Maadhimisho ya Papa kwa Mwezi Aprili-Julai yachapishwa!

Ziara ya Kitume kwenda Afrika na Hispania na kisha ziara za kichungaji kwenda Pompei huko Napoli,Lampedusa na Pavia,pamoja na misa mjini Vatican ndiyo ratiba ya Kipapa,iliyochapishwa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa,Jumatatu tarehe 30 Machi 2026. Vatican News

Vatican News

Ofisi ya Liturujia za Kipapa, Jumatatu tarehe 30 Machi 2026 imechapisha ratiba ya Maadhimishi ya Misa na ziara za Papa kuanzia mwezi Aprili hadi Julai 2026. Awali ya yote kuanzia tarehe 13 hadi 23 Aprili 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kwenda Ziara ya Kitume nchini Algeria, Camerun, Angola na Guinea ya Ikweta.

Tarehe 26 Aprili 2026, katika Dominika ya IV ya Pasaka, Baba Mtakatifu Leo XIV ataongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya Kuwaweka daraja la Upadre, Mapadre wa Jimbo Kuu la Roma, saa 3.00 kamili  asubuhi majira ya Ulaya, katika Basilika ya Mtakatifu Petro.

Mwezi Mei 2026

Tarehe 2 Mei 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kuongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya kuwaweka wakfu wa Kiaskofu, Maaskofu wa JimboKuu la Roma katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Laterano, saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya.

Tarehe 8 Mei 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kwenda Ziara ya Kichungaji huko Pompei, Napoli nchini Italia ambapo ataadhimisha Misa Takatifu katika Madhabahu ya Mwenyeheri Bikira Maria wa Rozari, wa Pompei.

Mnamo tarehe 24 Mei 2026, katika Dominika ya Pentekoste, Maadhimisho ya Misa Takatifu itafanyika katika Basilika ya Mtakatifu  Petro, saa 4.00  kamili masaa ya Ulaya.

Mwezi Juni 2026

Kuanzia tarehe 6-12 Juni 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kwenda Ziara ya Kitume nchini Hispania. Wakati  huo tarehe 20 Juni 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV atafanya ziara ya kichungaji huko Pavia nchini Italia  katika Basilika ya Mtakatifu Agostino, ambapo saa 11.00 ataadhimisha Masifu ya Jioni.

Tarehe 29 Juni 2026, ni Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo Mitume ambapo katika Basilika ya Mtakatifu Petro, Misa itaadhimishwa, kwa Baraka na kuvishwa Palium, Maakofu wakuu wapya wa majimbo makuu.

Mwezi Julai 2026

Hatimaye tarehe 4 Julai 2026, Baba Mtakatifu  Leo XIV anatarajia kufanya Ziara yake ya kichungaji huko, Lampedusa, Kusini mwa Italia, ambapo anataadhimisha misa saa 4.00 kamili masaa ya Ulaya.

RATIBA YA PAPA MAADHIMISHO APRIL -JULAI 2026

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

30 Machi 2026, 12:35